Pinda awapasha Wazanzibari (Muungano aulazimisha)

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,006
Pinda awapasha wazanzibari

Written by Bigfather // 29/04/2011 // Habari // 17 Comments

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewatolea uvivu Wazanzibari kwa kuwaeleza kuwa, wanaotaka kuvunja Muungano au kutaka kujiunga na jumuiya za kimataifa nje kama nchi wajaribu na wataona matokeo yake.

Pinda leo ametoa majibu yanayoashiria kuwa haridhishwi na namna baadhi ya watu wakiwamo wabunge na viongozi wa Zanzibar wanavyojaribu kutaka kupata uwakilishi wa kimataifa nje bila kuihusisha Tanzania.
Kwa namna alivyojibu bungeni,wanaochokonoa Muungano kwa visingizio mbalimbali vikiwamo vya mgawanyo wa rasilimali pia wanamuudhi.

Ametoa msimamo huo wakati anajibu swali la papo kwa hapo la Mbunge wa Chwaka, Yahya Kassim Issa ikiwa ni utaratibu wa Bunge kila Alhamisi kabla ya kipindi cha maswali na majibu.

"Si mjaribu basi huko mnakotaka kwenda, kisha tujajua kama mmepata au la" amesema Waziri Mkuu.
Wakati anauliza swali hilo, Mbunge huyo alieleza kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inazungumzia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kama mwakilishi wa masuala ya nje, lakini vipi Zanzibar isiwe na uwakilishi wake?

Waziri Mkuu amesema, "sijui Mheshimiwa Yahya anataka nini kwa swali hili? Kama ni nje tunawakilishwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Wizara hii ni kiungo cha nchi yetu na mataifa mengine."

Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii (CCM), alisema kazi ya Mbunge ni kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na hivi karibuni kumekuwa na kauli zinazoashiria uchochezi wa kuvunja muungano kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar na hakuna kiongozi ye yote mwandamizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Rais wala Waziri Kiongozi aliyetoa kauli, hivyo alitaka kupata kauli ya Waziri Mkuu, Pinda.

Pinda alisema, "nilikuwa nikisubiri sana swali hili, nilijua litakuja kutoka kwa akina Mnyaa (Mohamed Habib, Mbunge Mkanyageni), lakini wamekaa kimya kama wameshabikia yale yaliyotokea."

Waziri Mkuu alisema msingi wote wa mjadala huo wa wabunge wa Baraza la Wawakilishi ni suala la mafuta na gesi, ambalo aliongeza kuwa Rais Jakaya Kikwete alishalitolea kauli katika hotuba yake ya miezi michache iliyopita kwa Taifa.

Waziri Mkuu alisema suala la mafuta na gesi limekuwapo katika mambo ya Muungano tangu mwaka 1968, lakini kutokana na kauli ya Rais, suala hilo halipaswi kuwagawa Watanzania kwa sababu mafuta yenyewe hayajagundulika; hivyo hakuna sababu ya kutupiana maneno makali.

"Pia suala hili halina tatizo, ni moja ya mambo yaliyoonekana yazungumzwe kwenye Kamati ya Pamoja chini ya Makamu wa Rais. Tukateua Mshauri Mwelekezi ambaye Juni 27 mwaka huu, alikabidhi ripoti yake kwa pande mbili… ingekuwa vyema kupitia hiyo taarifa na kuona jinsi ya kushughulikia suala hili katika Muungano," amesema Waziri Mkuu.

Alimshukuru kwa dhati Selelii kuuliza swali hilo, akisema ametiwa simanzi na kauli za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliotoa kauli kama "Wakoloni" na "wezi wa mchana" ambazo Waziri Mkuu alieleza kuwa zimemshangaza.

"Ni mawazo yangu kuwa Muungano ni mzuri…ipo siku tutafarakana… otherwise(vinginevyo) muwe tayari kujua ni upande gani utaathirika zaidi," amesema Waziri Mkuu akihitimisha kujibu swali la Selelii.

Hivi karibuni, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walitangaza kuwa suala la mafuta na gesi linaondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano na Zanzibar itasimamia yenyewe masuala hayo.
 
Inaonekana viongozi wamekosa hoja,sasa kilichobaki kulazimishana,lakini hajui yakuwa Pinda hajengi bali anabomoa,kama munakumbuka kauli yake ambayo alitamka zanzbar sio nchi,wazanzibar wakaja juu,na badala yake kufanya maridhiano ili wananachi kuwa pamoja,na kubadilisha vipengele ili kupa hadhi zanzbar kikatiba.

Jee na hili jee kauliyake nyengine wazanzbari wataichukuliaje ?
 
Hawa Wazanzibar naona wamezidi kututishia watu wazima nyau, wao wanadhani bado kuna uwezekano wakula hela ya mwaarabu kupitia mashirika ya kidini. Kama wao wanao vipi si wajikate tu bwana sio kutafuta vijisababu kila siku. Mbona sisi Tanganyika hatuna Rais wao wanaye na tumewanyamazia na hela yangu ya kodi kutoka Kigoma inakwenda mpaka kwao.

Mafuta yana watoa roho na hela za dhahabu tumekula wote kila siku hawa waende tu hawana issue , japo mtoto wa mkulima ni kilaza lakini kwa hili nampa pongezi waende wakajaribu tuone nani mwenye hasara au faida
Inaonekana viongozi wamekosa hoja, sasa kilichobaki kulazimishana, lakini hajui ya kuwa pinda hajengi bali anabomoa.

Kama mnakumbuka kauli yake ambayo alitamka Zanzbar sio nchi, Wazanzibar wakaja juu, na badala yake kufanya maridhiano ili wananachi kuwa pamoja, na kubadilisha vipengele ili kuipa hadhi zanzibar kikatiba.

Jee na hili jee kauliyake nyengine wazanzbari wataichukuliaje ?
 
huyu mzee maropokaga sana...anawajua sana wazazibar walivyo na mdomo watam taiti aaanza kulia lia ...shauri zake
 
Amenishangaza kusema Mafuta bado hayajapatwa na pia Vunjeni Muungano Muone Nani ataumia...

Kuna Siri Wananchi hatuijui? We need to know all before we started discussing about our Constituency (including our Union)
 
Just a moment, ... hii habari ya Nipashe ni ya 29 April lakini ananukuu maswali ya papo kwa hapo bungeni! Uandishi wa aina hii mara nyingi unakuwa sponsered, sijui Nipashe wana agenda gani?
 
Kakalende said:
Just a moment, ... hii habari ya Nipashe ni ya 29 April lakini ananukuu maswali ya papo kwa hapo bungeni! Uandishi wa aina hii mara nyingi unakuwa sponsered, sijui Nipashe wana agenda gani?
Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii (CCM), alisema kazi ya Mbunge ni kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na hivi karibuni kumekuwa na kauli zinazoashiria uchochezi wa kuvunja muungano kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar na hakuna kiongozi ye yote mwandamizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Rais wala Waziri Kiongozi aliyetoa kauli, hivyo alitaka kupata kauli ya Waziri Mkuu, Pinda.
Ukilejea swali lililoulizwa na Lucas Selelii (Mb.) utagundua hii habari ni ya mwaka jana (2010) au miaka ya nyuma kwani Selelii si mbunge katika Bunge la sasa (2010-2015). Nadhani ni kosa la gazeti au mbandikaji wa habari.
 
Hii habari ilishapita, alichotakiwa kufanya muanzishaji wa hii thread ni kutoa taarifa kuwa anapenda kurudia tamko la Pinda, angetuambia kabla sababu ya kuirudia habari hii, badala ya kuitoa kama ndiyo breaking news.
 
Mtoa taarifa anania gani? maana hii habari inamseto husiopikika chungu kimoja!
 
Kama hayo ndiyo majibu ya Pinda, basi naamini kuwa ndiyo majibu ya serikali. Mimi naona kuwa Pinda kachemsha, kama suala la mafuta lipo tangu 1968, muungano wetu ni wa mwaka 1964 basi atueleze hilo la mafuta liliingia vipi wakati makubaliano ya awali yapo katika vipengele 11 tu ya mkataba wa muungano. Tusionekane kama walowezi na wapenda kupora vitu vya watu, tuiache zanzibar iendeshe raslimali zake na TZ bara ina raslimali zake. Sielewi kwanini tunaling'ang'ania suala la mafuta? Pinda ametetea zoezi la kuweka viraka kwenye mkataba wa muungano jambo ambalo watanzania wengi hawaliafiki kwa kuwa hawakushilikishwa.
 
Namsapoti sana mtoto wa mkulima katika hili.Muungano haulazimishwi na mtu yoyote,kama waZenji wameushiba wawe huru kukitoa.
Hii habari ni ya siku nyingi kidogo na mtoa hoja naona kairudia tu.
Sisi waTanganyika hatuna haja na hao wanaotaka kujitoa, na waende zao ili warudi na kuingia kwetu kwa passport.
Madhumuni makuu ya muungano wakati ule ni kuilinda Zanzibar isitwaliwe na wahuni maana ilikuwa kama ptoto aliyezaliwa jana.Sasa wahuni hawapo na hawauhutaji tena muungano mie naona poa tu, wakitoe.
 
Mleta hoja hana tatizo hata kama ni habari ya zamani lakini ni debatable kwa vile haijapatiwa ufumbuzi kama tunavyo jadili masuala ya Dowans ya mwaka 2006, afterall Pinda bado ni kiongozi wa nafasi ileile wakati anatoa hii statement. Kwa kifupi naungana na Pinda kuwa wajaribu kujitenga waone, leo wazanzibari wana sauti kwa sababu wako ndani ya muungano lakini wakitoka nje hatutasikia sauti za mzanzibari tutaanza kusikia sauti za wawekezaji hasa waarabu watakaokuwa wamewekeza humo.
 
LET THEM GOOOOO..........................

Na hapo tutaona tunavyokufa kwa njaa maana jamaa wanaamini kuwa bila mafuta yao, Tanganyika kwishieni.
 
Hili dubwana muungano limeshanichosha sijui kwanini tunalazimisha wacha Zanzibar ijitenge nina hakika hata mchango wa EAC utawashinda hawana hisani bora wachape mwendo.
 
Pinda awapasha wazanzibari

Written by Bigfather // 29/04/2011 // Habari // 17 Comments

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewatolea uvivu Wazanzibari kwa kuwaeleza kuwa, wanaotaka kuvunja Muungano au kutaka kujiunga na jumuiya za kimataifa nje kama nchi wajaribu na wataona matokeo yake.

Pinda leo ametoa majibu yanayoashiria kuwa haridhishwi na namna baadhi ya watu wakiwamo wabunge na viongozi wa Zanzibar wanavyojaribu kutaka kupata uwakilishi wa kimataifa nje bila kuihusisha Tanzania.
Kwa namna alivyojibu bungeni,wanaochokonoa Muungano kwa visingizio mbalimbali vikiwamo vya mgawanyo wa rasilimali pia wanamuudhi.

Ametoa msimamo huo wakati anajibu swali la papo kwa hapo la Mbunge wa Chwaka, Yahya Kassim Issa ikiwa ni utaratibu wa Bunge kila Alhamisi kabla ya kipindi cha maswali na majibu.

“Si mjaribu basi huko mnakotaka kwenda, kisha tujajua kama mmepata au la” amesema Waziri Mkuu.
Wakati anauliza swali hilo, Mbunge huyo alieleza kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inazungumzia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kama mwakilishi wa masuala ya nje, lakini vipi Zanzibar isiwe na uwakilishi wake?

Waziri Mkuu amesema, “sijui Mheshimiwa Yahya anataka nini kwa swali hili? Kama ni nje tunawakilishwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Wizara hii ni kiungo cha nchi yetu na mataifa mengine.”

Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii (CCM), alisema kazi ya Mbunge ni kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na hivi karibuni kumekuwa na kauli zinazoashiria uchochezi wa kuvunja muungano kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar na hakuna kiongozi ye yote mwandamizi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Rais wala Waziri Kiongozi aliyetoa kauli, hivyo alitaka kupata kauli ya Waziri Mkuu, Pinda.

Pinda alisema, “nilikuwa nikisubiri sana swali hili, nilijua litakuja kutoka kwa akina Mnyaa (Mohamed Habib, Mbunge Mkanyageni), lakini wamekaa kimya kama wameshabikia yale yaliyotokea.”

Waziri Mkuu alisema msingi wote wa mjadala huo wa wabunge wa Baraza la Wawakilishi ni suala la mafuta na gesi, ambalo aliongeza kuwa Rais Jakaya Kikwete alishalitolea kauli katika hotuba yake ya miezi michache iliyopita kwa Taifa.

Waziri Mkuu alisema suala la mafuta na gesi limekuwapo katika mambo ya Muungano tangu mwaka 1968, lakini kutokana na kauli ya Rais, suala hilo halipaswi kuwagawa Watanzania kwa sababu mafuta yenyewe hayajagundulika; hivyo hakuna sababu ya kutupiana maneno makali.

“Pia suala hili halina tatizo, ni moja ya mambo yaliyoonekana yazungumzwe kwenye Kamati ya Pamoja chini ya Makamu wa Rais. Tukateua Mshauri Mwelekezi ambaye Juni 27 mwaka huu, alikabidhi ripoti yake kwa pande mbili… ingekuwa vyema kupitia hiyo taarifa na kuona jinsi ya kushughulikia suala hili katika Muungano,” amesema Waziri Mkuu.

Alimshukuru kwa dhati Selelii kuuliza swali hilo, akisema ametiwa simanzi na kauli za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliotoa kauli kama “Wakoloni” na “wezi wa mchana” ambazo Waziri Mkuu alieleza kuwa zimemshangaza.

“Ni mawazo yangu kuwa Muungano ni mzuri…ipo siku tutafarakana… otherwise(vinginevyo) muwe tayari kujua ni upande gani utaathirika zaidi,” amesema Waziri Mkuu akihitimisha kujibu swali la Selelii.

Hivi karibuni, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walitangaza kuwa suala la mafuta na gesi linaondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano na Zanzibar itasimamia yenyewe masuala hayo.

Mbona hii habari inaonekana outdated ama ni macho na mawazo yangu?
 
Redio | Mzalendo.net

Naomba wazalendo watanzania mufungua hapo juu kuna mahojiano baina ya mzee Nassor Moyo ambaye aliekuwa waziri wakati ule wakati wa muungano utawala wa karume.

Pia mahojiano ya ZITO KABWE,

Ni radio ya ujerumani,sikilizeni taarifa hiyo ya 15:00-16:00 jioni.
 
Inaonekana viongozi wamekosa hoja,sasa kilichobaki kulazimishana,lakini hajui yakuwa Pinda hajengi bali anabomoa,kama munakumbuka kauli yake ambayo alitamka zanzbar sio nchi,wazanzibar wakaja juu,na badala yake kufanya maridhiano ili wananachi kuwa pamoja,na kubadilisha vipengele ili kupa hadhi zanzbar kikatiba.

Jee na hili jee kauliyake nyengine wazanzbari wataichukuliaje ?

Zanzibar sio nchi kisheria, nani anabisha?
 
huyu mzee maropokaga sana...anawajua sana wazazibar walivyo na mdomo watam taiti aaanza kulia lia ...shauri zake

Wazenj hawana jipya, kila siku mafuta, mafuta! Wayachimbe basi wajipake kama walivyoahidi!
 
Hili dubwana muungano limeshanichosha sijui kwanini tunalazimisha wacha Zanzibar ijitenge nina hakika hata mchango wa EAC utawashinda hawana hisani bora wachape mwendo.

Hakuna Mzanzibari aliyelazimishwa kuungana, ndio maana wameajiriwa hata kwenye idara zisizo za Muungano wamekubali, wanaishi na kujimwaga Tanzania Bara bila wasiwasi wowote!
 
Back
Top Bottom