Pinda awaomba radhi Wakatoliki

Nafikiri ingekua busara zaidi kama anaona ipo haja ya kuomba radhi kwa taasisi za dini, basi angefanya hivyo kwa dini zote, kwani sidhani kua kuna ambae hakuguswa na vurumai za uchaguzi. Inawezekana asingeweza kufanya hivyo pale kulingana na mazingira lakin anaweza akafanya hivyo ktk nyakati tofauti.

Vingenevyo inaweza kuleta hisia kama kua taasisi moja ina influence kubwa ktk nchi kuliko nyingine jambo ambalo sidhani kua lina maslahi hata na kanuni zenyewe za uongozi bora.
 
kwani walifanya nini? na kanisa katolini ni nini? si dini kama dini zingine tu? kitendo gani cha ajabu walifanya haswa?

Jazba!!!teh teh teh ,ukristu utaendelea kuwepo utake usitake!!!
 
Mtu mwenye sababu ya kuomba msamaha kwa niabaya ya CCM ni Katibu Mkuu wa chama hicho; na msamaha huu unatakiwa uende kwa dini zote kwani kama nilivyosema awali udini uliletwa na CCM kwenye uchaguzii mkuu..
 
Jazba!!!teh teh teh ,ukristu utaendelea kuwepo utake usitake!!!
mimi ni mkristo, nilikuwa nauliza wamefanya nini ambacho pinda anaomba msahama? na anaomba msamaha kisiasa au kiimani kwasababu kiimani mtu anatakiwa yeye mwenyewe binafsi ndo aomba msamaha kwa Mungu..mwana wa adam anayo mamlaka ya kusamehe dhambi duniani....wapige goti mbele za Yesu kama walimkosea Mungu...ndo maana nilikuwa nauliza wamefanya kosa gani? na ccm yenye watu mafisadi na watu wa dini mbalimbali, wanaomba msamaha ka wakatoliki au kwa Mungu? kama ni kwa mungu kwa mungu yupi? allah au Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo?
 
well said sir.

Na Pinda mwenyewe amewaomba radhi wanasumbawanga kwa uchakachuaji wa kura alioufanya yeye mwenyewe?

unapokashfu au kumtukana Mungu linakuwa suala binafsi, hao walioutukana UTATU ambao ndio msingi wa imani ya Wakristo wamemwomba nani msamaha na ni nani amewaongoza sala ya toba na kuwaombea?
 
Mtu mwenye sababu ya kuomba msamaha kwa niabaya ya CCM ni Katibu Mkuu wa chama hicho; na msamaha huu unatakiwa uende kwa dini zote kwani kama nilivyosema awali udini uliletwa na CCM kwenye uchaguzii mkuu..

Pinda anajua alichofanya Sumbawanga kiasi kwamba kwa sasa hakubaliki tena sumbawanga, ndiyo maana alikwenda yeye mwenyewe.
 
Kwa kweli Pinda hakutakiwa kuomba msamaha kwa niaba ya waliotenda hilo kosa, wao wenyewe ndio waombe Msamaha na sio kwa askofu bali kwa Mungu kwa kuwa huyo ndie waliemkashifu. Hakika wanatakiwa watubu!
 
Imeandikwa kisasi ni kwa BWANA wa Majeshi si kwetu. Tena imeandikwa usiposemehe hauwezi kusamehewa. Futa kauli yako kama wewe ni Mkristo.

Kumbuka pia BWANA ni mwingi wa hasira kiasi hupatiliza hata vizazi vinne. Mwanadamu huwezi kujiita Mungu Baba, Mungu Mwana (Yesu), Mungu Roho Mtakatifu na usitake kutubu utegemee chama kiombe radhi.

Chama kama chama maana si nafsi iliyo hai haiwezi kutubu, bali kuomba radhi nikimaanisha kuwa chama kama chama kimeomba radhi kwenye taasisi, lakini waumini wanapaswa kutubu dhambi waliyoifanya maana wengi wao wanakiri kuwa walitenda dhambi kwa kufanya kile walichofanya. Na kwa maadili ya kikristo mtu kama hajatubu dhambi (kwa dhamiri yake yeye mwenyewe binafsi) aliyotenda anaendelea kutengwa.

Pinda amejipeleka maana anajua dhambi aliyoitenda yeye mwenyewe kwa Mungu na kwa wana-Sumbawanga na kwa kanisa lililomsomesha Kaengesa Seminari na kumlea mpaka alipofika.
 
Let God himself settle that case,its for him to avenge not us!Mungu ndo anaweza jua yuko sincere na hao waliofanya hivyo na si wanadamu.Kama walikufuru na hawajutii hilo na kutubu,Mungu analo la kuwafanya,hatuna uwezo wa kuona unyenyekevu wa mioyo yao.Tusonge mbele kuna mengine yaliyoko ndani ya uwezo wetu ya kufikiria na kupangia mikakati great thinkers!
 
Msamaha unaoombwa kwa Kanisa Katoliki si wa kuongea mbele ya wazee au waandishi wa habari. Ni msamaha ambao unafanyika katika ibada au misa maalum ambapo kila muumini aliyefanya kosa kubwa kama hilo la kumkashifu roho wa Bwana anapita na kula kiapo cha kumkana shetani na mambo yake yote.

Sana sana Pinda angewaombea msamaha kwa Mungu huku akimuomba Mungu awape ujasiri wa kukiri makosa na kufanya kitubio.

CRUSADERS!!!!!!!!!!!!!!! KANISA LINALOONGOZWA KWA MISINGI YA SHETANI UTALIJUA TU.
kwanza linapenda kujikweza na kujiona lenyewe ndio bora kuliko hata waumini na pengine kuliko hata kristo yesu........
KATOLIKI KITU GANI BWANA?????????????????? nani asiyejua kuwa utawala wa ndani wa Vatican unaongozwa na MAFIA MOB???????

mliendekeza sana udini katika uchaguzi mkuu uliopita kwa kigezo cha kuwafundisha waumini wenu elimu ya uraia, watu wamewastukia dhamira yenu mnawageuzia kibao kuwa eti wao ndio wadini..
hamkuwa na ruhsa toka kwa mungu na dhamira yenu ilikuwa ni ya kishetani na ndio maana mungu hakuwasimamaia. Mpango wenu wa kusimika utawala wa kikanisa ndani ya tanzania hautafanikiwa.
Na yeyote kati yenu asijitie ujinga wa kudhani kuwa mko huru na nguvu ya kufanya chochote mnachotaka. uhuru huo hamna na nguvu hizo hamna. HII nchi ni yetu sote na wala haitawaliwi naMAMA ASKOFU OOOH SORRY BABA ASKOFU
 
Dhambi zote utasamehewa ila siyo KUFUKURU/KUMFUKURU ROHO MTAKATIFU. Pinda wakati wa uchaguzi alielezwa hilo tatizo akashindwa kuwakemea sasa wamepita na wametengwa ndo anakuja kuomba msamaha kwa nini hakufanya wakati ule? Pamoja na hayo nakupa big up kwa kuomba msamaha maana kuomba msamaha inaonyesha ww ni kiongozi unayejua pale ulipokosea. Lakini mtoto mwenzangu wa mkulima kwa nini huwa inaonekana kama vile unatumiwa? Maana unaongea vizuri sana na mimi naamini una nia nzuri na yale unayoongea tatizo lako huna matendo, au wanakupuuza? Kama wanakupuuza then kuwa na meno kama ulivyofanya kweli nyumbani kwa mkwere kwa kuwaajibisha kurugenzi ya bagamoyo, kwa nini hurudii tena na madudu kama hayo yako mengi sana. Au mkwere alikuweka sawa maana ulimshika pabaya?
 
mimi ni mkristo, nilikuwa nauliza wamefanya nini ambacho pinda anaomba msahama? na anaomba msamaha kisiasa au kiimani kwasababu kiimani mtu anatakiwa yeye mwenyewe binafsi ndo aomba msamaha kwa Mungu..mwana wa adam anayo mamlaka ya kusamehe dhambi duniani....wapige goti mbele za Yesu kama walimkosea Mungu...ndo maana nilikuwa nauliza wamefanya kosa gani? na ccm yenye watu mafisadi na watu wa dini mbalimbali, wanaomba msamaha ka wakatoliki au kwa Mungu? kama ni kwa mungu kwa mungu yupi? allah au Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo?

Mkuu umesema sawa. Namshangaa Pinda kwani ninavyojua kwa imani ya kikristo, Mtu huwa anaomba msamaha kwa utashi wake mwenyewe. Ndo maana tunashauriwa tutubu dhambi zetu tukiwa bado na nguvu kwa sababu ukikata kauli kabla hujasuluhisha imekula kwako.

Pinda asuluhishe ya Chama chake na kanisa ila hao waumini wakasuluhishe wenyewe.
 
Na Sammy Kisika, Sumbawanga

WAZIRI Mkuu, Bw. Mizengo Pinda amewaomba radhi viongozi wa dini hasa Kanisa Katoliki kutokana na kitendo cha baadhi ya wafuasi na wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutumia kauli zinazokinzana na imani zao wakati wa kampeni za uchaguzi uliopita.

Bw. Pinda ambaye pia Mjumbe wa halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM, aliomba radhi hiyo katika kikao baina yake na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini na baadhi ya wazee maarufu wa mjini hapa jana, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Libori mjini Sumbawanga.

"Najua tulimkwaza Mhashamu Baba Askofu (Damian Kyaruzi), tumekejeli imani ya dini yake, tunaomba radhi. Mimi naomba radhi kwa niaba ya CCM na serikali. Si hapa tu (Sumbawanga) lakini ni maeneo mengi nchini kama vile majimbo ya uchaguzi ya Hai na Same ambapo baadhi ya wagombea katika kuomba kura ya ndiyo, walilazimika kutumia baadhi ya maneno yanayotumika katika Injili.

"Uchaguzi mkuu uliopita haukuwa laini kama ilivyotarajiwa na kutazamiwa, lakini badala yake ulikuwa na changamoto nyingi ikiwemo tofauti za kimtizamo na kiimani, hivyo kwa yale yaliyojitokeza ya baadhi ya waliokuwa wagombea kugusa imani za dini za watu, halikuwa lengo lao kufanya hivyo na tunaomba mtusamehe kwa yote yaliyojitokeza na kukwaza imani za dini zenu," alisema Bw. Pinda.

Kauli hiyo ya Bw. Pinda imekuja wakati Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga likiwa limewasimamisha na kuwatenga baadhi ya waumini kwa kukashifu Utatu Mtakatifu kwa kuufananisha na kaulimbiu ya mafiga matatu, yaani rais, mbunge na diwani; wakifananishwa na Mungu, Yesu Kristo na Roho Mtakatifu wakati wa kampeni.

Vile vile waumini hao ambao ni wafuasi wa CCM wanadaiwa kukashifu alama ya kanisa, msalaba, kwa kuuzika wakati wa kushangilia ushindi wa mgombea wao.

Wakati Bw. Pinda akikiri makosa hayo na kuomba radhi, baadhi ya viongozi wa CCM mkoani humo wamekuwa wakissitiza kuwa waumini hao wametengwa kutokana na kushabikia chama hicho na mgombea wake wa Ubunge, na hivyo kutofautiana na mgombea wa CHADEMA wanayedai alikuwa anaungwa mkono na kanisa hilo.

Akitoa maoni ya jumla ya uchaguzi huo, Bw. Pinda alisema kuwa kutokana hali iliyojitokeza, CCM na Serikali yake imepata fundisho, na hivyo kuomba katika chaguzi zijazo viongozi wa dini, serikali na vyama vya siasa wakae pamoja na kuweka angalizo ili wagombea wajiepushe na kukejeli imani za dini za watu wengine.

Waziri Mkuu aliwasihi viongozi hao wa dini nchini nzima kuanza ukurasa mpya na kutumia muda mrefu kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo.

Akizungumzia suala la rushwa, alikiri kukithiri kwa vitendo hivyo katika uchaguzi mkuu uliopita na kuongeza kuwa ipo haja ya kuangali upya mfumo wa uchaguzi kuanzia ndani ya CCM ambayo inajiandaa kwa uchaguzi wa viongozi wake mapema mwakani, ili kuhakikisha hautatoa mianya ya rushwa.

Aliwaomba viongozi wa madhehebu ya dini na wazee kukemea kwa nguvu zote vitendo vya rushwa.

"rushwa ni rushwa tu, hakuna haja ya kusema kuna rushwa ndogo hata mtu anapotaka kutimiza haja zake fulani kwa kutoa kitu kidogo bado ni rushwa. Pia kwa mgombea anapotoa doti ya khanga ili apigiwe kura hilo ni tatizo, hivyo naiomba CCM ibadilike, najua ni jambo gumu lakini lazima tupigane nalo kikamilifu. Wagombea nao taabu tu, hasa kwenye chama, safari hii tujirekebishe," alisema Pinda.

Akitoa neno la shukrani, Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo Tanzania mkoa wa Rukwa, Mchungaji Israel Moshi alisema kuwa madhehebu ya dini yamesamehe, na kuwataka viongozi kusameheana kwa kuwa wote ni binadamu.
Someni hapo kwenye red, wahusika wenyewe waliokuwa ndani ya tukio wanasema kuwa kanisa liliwafukuza kwa kuwa walikuwa hawawaungi mkono chadema, sasa nyinyi mnabisha nini? red btn the line.
Halafu eti JK awaombe msamaha! kwa lipi? kumpigia kampeni slaa kanisani? au? Mtengeni na yeye basi ili asije hapo kanisani kuombewa, kwani naye ni muumini wenu! huu kama si uchizi nini?
 
CRUSADERS!!!!!!!!!!!!!!! KANISA LINALOONGOZWA KWA MISINGI YA SHETANI UTALIJUA TU.
kwanza linapenda kujikweza na kujiona lenyewe ndio bora kuliko hata waumini na pengine kuliko hata kristo yesu........
KATOLIKI KITU GANI BWANA?????????????????? nani asiyejua kuwa utawala wa ndani wa Vatican unaongozwa na MAFIA MOB???????

mliendekeza sana udini katika uchaguzi mkuu uliopita kwa kigezo cha kuwafundisha waumini wenu elimu ya uraia, watu wamewastukia dhamira yenu mnawageuzia kibao kuwa eti wao ndio wadini..
hamkuwa na ruhsa toka kwa mungu na dhamira yenu ilikuwa ni ya kishetani na ndio maana mungu hakuwasimamaia. Mpango wenu wa kusimika utawala wa kikanisa ndani ya tanzania hautafanikiwa.
Na yeyote kati yenu asijitie ujinga wa kudhani kuwa mko huru na nguvu ya kufanya chochote mnachotaka. uhuru huo hamna na nguvu hizo hamna. HII nchi ni yetu sote na wala haitawaliwi naMAMA ASKOFU OOOH SORRY BABA ASKOFU

If you have nothing to say you sabathian then dont say it here.
 
pole sana kanisa katoliki linautaratibu wake, waliotengwa hawajazuiwa kwenda sehemu yoyote ya ibada ila si katoliki, kama wanafikili kanisa katoliki linahitaji wingi wa watu kujaa katika makanisa yake wamepotea, linahitaji wafasi wanaofata utaratibu, na linamisimamo yake. narudia tena halihitaji ubabaishaji wote waliofanya kufuru lazima watubu kama hawajatubu mmoja mmoja wasitegemee kuwa kuomba radhi kwa pinda kutawasaidia, kanisa katoliki si chombo cha siasa
 
Pia kama mko Serious acheni kushabikia Manchester kwani walipoifunga Arsenal they did the same as what was done by Sumbawanga pipo
 
Imeandikwa kisasi ni kwa BWANA wa Majeshi si kwetu. Tena imeandikwa usiposemehe hauwezi kusamehewa. Futa kauli yako kama wewe ni Mkristo.

Wanasamehewa wanaojua wamekosa na wanaomba wasamehewe. Sasa wahusika wanasema Kanisa ndilo litubu ikiwa na maana kuwa wao hawajakosa wasamehewe nini?
 
mimi ni mkristo, nilikuwa nauliza wamefanya nini ambacho pinda anaomba msahama? na anaomba msamaha kisiasa au kiimani kwasababu kiimani mtu anatakiwa yeye mwenyewe binafsi ndo aomba msamaha kwa Mungu..mwana wa adam anayo mamlaka ya kusamehe dhambi duniani....wapige goti mbele za Yesu kama walimkosea Mungu...ndo maana nilikuwa nauliza wamefanya kosa gani? na ccm yenye watu mafisadi na watu wa dini mbalimbali, wanaomba msamaha ka wakatoliki au kwa Mungu? kama ni kwa mungu kwa mungu yupi? allah au Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo?

Mzozo uliopo unahusu mgombea ubunge CCM na wafuasi wake na viongozi wa Kanisa Katoliki Sumbawanga - pamoja na kuwa walifanya kinyume na mafundisho ya dini yao, waliwadhihaki na kuwachafua viongozi wa dhehebu hilo. Ni kama mtu pamoja na kutukana imani yako akutukane na wewe pia akitaja jina au cheo chako.
 
kwani walifanya nini? na kanisa katolini ni nini? si dini kama dini zingine tu? kitendo gani cha ajabu walifanya haswa?

Well inaelekea hujui nn kilichotokea. Inshu hapa si kanisa katoliki ni nini wala si kufanya kitendo cha ajabu. Unachotakiwa kuelewa ni kwamba kila dini inahitaji kuheshimiwa. That is why we always insists on religious tolerance, respect and freedom of worshiping.

Kitendo cha kufananisha Rais, mbunge na diwani kama utatu mtakatifu yaani Mungu baba, Mungu mwana na Mungu roho mtakatifu, ni kitendo cha dharau kwa imani ya kikristo let alone Roman Catholic. halikadhalika kitendo cha kuuzika msalaba ambao ndio alama kuu ya kanisa na inayobeba imani nzima ya kanisa lolote la kiristo duniani. Kibaya zaidi ni kwamba katika hao wapo pia wakristo wakiwamo wakatoliki, hivyo kwa utaratibu wa Kanisa watu hawa wamedharau mafundisho ya kanisa kwa kudharau the holy trinity and the cross. Imani ya kikristo inasema dhambi zote husamehewa isipokuwa dhambi ya kumkashifu roho mtakatifu. Kwa msingi huu wakristo hawa waliotanguliza mbele ushabiki wa kisiasa na kwenda kinyume na imani ya kanisa si tu wanastahili kutengwa bali pia kufutwa kabisa katika orodha ya waumini wa kanisa.

Unaweza ukasema kwamba nahukumu!; la hasha!, here we go....Viongozi wa kanisa wamepewa mamlaka toka juu ya kufunga na kufungua....The bible tells in Mathew 16:19 and 18:18 about Jesus giving authority of "binding and loosing"to the apostles/disciples.

"Whatever you bind on earth will be bound in heaven, and whatever you loose on earth will be loosed in heaven"

Kwa maana hii kanisa linayo authority ya kutoa hukumu kwa waumini wake kwa kadri ya misingi ya kanisa/biblia. This authority, not on exactly the same level as during the apostolic era, still resides in the leaders of the local church. Wanaweza wasipokee same kind of supernatural guidance as the apostles did, but they possess the entire New Testament along with the direction of the Holy Spirit. Therefore, when church leaders discipline a church member who promotes incorrect doctrine or is involved in evil behavior, they act with divine approval. They are carrying out God's will, and what they do is ratified in heaven. Since their authority is not ultimately derived from their personal qualities or their office but from Scripture and the instruction of the Holy Spirit, they should exercise it humbly and prayerfully.

Pinda hawezi kuwa msuluhishi dhidi ya ghadhabu ya Mungu eti by virtue of Autority vested upon him by the Gvt ...Kama ningepata nafasi ya kukutana na Mh. Pinda, ningemshauri apishe ghadhabu ya Mungu. Asisimame katikati ya Mungu na Wakosaji kwa sababu ghadhabu hii itampata yeye and he will not like it. Kama nae alishiriki basi atubu kwa nafsi yake ila hawezi kutubu kwa ajili ya wengine...He is not Jesus neither the holy spirit nor is he the High priest in heavenly places. So akae pembeni.

My advice:
Tuheshimu utaratibu na imani za wenzetu, kwamba RC ni nani sio swali linalotuhusu kama sisi sio RC. Kanisa katoliki limewachukulia hatua wale walio wake (waumini wa Kikatoliki) na haijawagusa wenye imani nyingine kwa maana haina mamlaka nao.

Mbona yule aliyechambua aya za shetani kutoka katika Quran, kichwa chake kinatafutwa kwa udi na uvumba hata sasa?...Vipi na yule mwandishi aliyechora picha ya Mtume Mohamad? jamii ya kiislamu inamsaka hata kesho. Wapo pia mamia kwa maelfu ya minority Christians wanaouwawa katika nchi za Kiislamu kwa kisingizio cha kwenda kinyume na sharia. Hawa si waislamu, hivyo hawakutakiwa kuchukuliwa hatua zozote kwa maana hawafungwi na sheria za dini isiyo yao. Je haya hatuyaoni hata tupige kelele dhidi ya kanisa linalotoa adhabu kwa watu wake kwa kadri ya misingi ya imani yao?

Back
Top Bottom