Pinda atimua watumishi Bagamoyo

Na nyie mmezidi bwana, hakuna zuri kwenu? Mlitaka awaache hata kama wamekosea? Ni vizuri pia mjue kwamba Pinda siyo Rais, ni Rais pekee mwenye mamlaka ya kumtimua yeyote katika nafasi yoyote. Lakini si waziri mkuu anayeweza kumfukuza Ndulu. Ya kupongeza tupongeze, na ya kuponda tuponde. sasa nyie yote mnaponda tu, kwani nyie wapinzani?

Watu hawaoni tena uzuri wowote kwa waziri mkuu wao na serikali yake kwa kua watu wameshaona viongozi wao na serikali kwa ujumla haiwathamini na inazidi kuwafanyia mzaha na usanii. Dalili ya kuchoshwa, sio lazima ni wapinzani bali ni watu wanapenda nchi yao.
 
Kama Pinda ana ushahidi wa kutosha wa kuwatimua kazi sawa. Lakini sio watu waje kwenda Mahakamani washinde kesi then muwalipe mihela kibao ya kodi za wananchi. Hizi sio enzi za Mwalimu za serikali ya ujamaa na kujitegemea hii ni serikali ya kibepari kwa hiyo sheria inafanya kazi. Si mmeona na kusikia wauwaji wanashinda kesi mahakamani?

Pesa zinakwenda kwa mahesabu na wataalamu wa mahesabu kwa kushirikiana na wanasheria wapo inabidi kuwa makini sana kabla ya kufukuza watu kazi. Kama ni kuliwa pesa zitakuwa zimeliwa siku nyingi sana, lakini wakati huu ndio wa kutafuta kura ndio mambo mengi sana ya kujisafisha yatatokea ili kutusahaulisha na maufisadi ya mabilioni ya pesa ili tuwape tena kura waendelee ulaji na ufisadi mwingine wa miaka mitano.

Sio kwamba nawatetea hao wa Bagamoyo ila natoa maoni ili serikali iwe makini sana na ijue tuna mengi moyoni ya kusema. Kwanza siamini kabisa kwamba hela za EPA zilirudishwa kama walivyokuwa wanatutangazia, ule ulikuwa ni usanii tuu na inaonekana watuhumiwa wote wataachiwa huru.
 
Midanganyika imeshadanganyika na kumsifia eti kafanya kazi nzuri. Huu ni uhuni mtuuup! Uchaguzi ndio huooooooooooo! Gari la Longido kwenda Ngorongoro Mhe. Kasusa kukabidhi maana wananchi wa longido waliahidiwa sijui angesemaje wakati wa kampeni za uchaguzi kama lingeenda ngorongoro sio kwamba anawapenda ameogopa kwenye kampeni angesemanini. Pinda sio kwamba amewaona wameiba, ni kuridhisha umma, na hayo ndio watasema wakati wa kampeni. Kama yuko serious, aanze na MRAMBA, YONA, JEETU PATEL, IDRISA, BENO, ETC ETC
 
Habari kuwa waziri mkuu Mizengo Pinda kuwatimua kazi watumishi wa halmashauri ya wilaya ya bagamoyo kwa upande wangu nimeipokea kwa hisia tofauti.

Kwanza, ni taarifa ya kutia faraja kwani huenda itakuwa imefungua njia kuelekea kule tunakoota kila siku kwenye maadili na uaminifu kazini. Kwani hadithi ya ufujaji wa fedha za umma na hasa katika halmashauri ni hadithi ya muda mrefu sana na nina imani hata serikali itakuwa imepata hasara ya ajabu.

Jambo la pili, sielewei kama uamuzi wa waziri mkuu kuwatimua kazi watumishi wale ni sehemu ya utendaji wake au ni mkakati mchafu wa kisiasa. Hapa nina maanisha kuwa tuko katika kuelekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba, mara nyingi siasa huwa naichukulia kama mazingaombwena hasa kwa hapa kwetu Tanzania. Sitashangaa kama kitendo cha kuwafukuzisha kazi watumishi wale ni ni sehemu ya CCM kujitengenezea mazingira ya kuwajaza ujinga watu wetu kuwa imekuwa mstari wa mbele kukemea maovu katika utumishi wa umma.

Sitaona ajabu kesho tukisikia na mkuu wa kaya nae akawatoa kafara watumishi sehemu nyingine na nyingine ili ikifika wakati wa uchaguzi wanapopanda majukwaani kutuomba kura ili wakale vizuri wakapata pa kusimamia.

Na ndio maana nadiriki kusema kuwa uammuzi wa Pinda kuwatimua kazi watumishi wale umechelewa mno. Halmashauri ni moja ya maeneo ambayo yana ubadhirifu wa fedha za umma katika kiwango cha kutisha. Ripoti ya ukaguzi katika manunuzi (Procurement audit report ) iliyofanywa na PPRA kwa mwezi wa Juni na Julai 2009 ulionyesha kuwa kuna msururu wa halmashauri takribani 30 zenye ripoti chafu kwa upande wa manunuzi. Manunuzi yanafanywa bila kufata sheria ya Public Procurement Act (PPA) of 2004 and regulations of 2005. Kama kweli Pinda anataka kuzisafisha hizi halmashauri ni jambo zuri sana lakini ajue kuwa uozo uko wa kutisha kwenye halmashauri zetu kwa hiyo akaze buti na timu yake.....
 
Code:
Hawajatimuliwa...ila wamesimamishwa uchunguzi ufanyike,kama watakutwa na hatia wataadhibiwa kama vinginevyo wanarudi kazini na fidia juu..tatizo sio ubadhirifu DC na DED walikuwa hawasalimiani kwa hiyo wakikubali kusalimiana yanaisha
Code:
Nasikia DC aliomba "mzigo" kwa DED DED akachomoa ndo visa vilipoanzia. Mmoja ni prezidensho apointiiiii mwingine kaungaunga kwenye maintavyuu akapewa ulaji, sasa ndo hapo utakapoona siasa zilivyo SI-HASA
 
Code:
Pinda amesema kuwa wametumia report ya CAG ya 2008 ambayo ilionesha kuwa wameshindwa kuthibiti matumizi ya pesa i.e wanatumia vibaya pesa za halmashauri. Kwani CAG aliitaja Bagamoyo peke yake? Nadhani kuna mambo zaidi ya hilo. Haiwezekana ufisadi ufanywe na kila idara ya serikali lakini wawajibishwe Bagamoyo tu!
Code:

SAFI SANA, NIMEKUPA SENKI MKUU
Nasikia DC aliomba "mzigo" kwa DED DED akachomoa ndo visa vilipoanzia. Mmoja ni prezidensho apointiiiii mwingine kaungaunga kwenye maintavyuu akapewa ulaji, sasa ndo hapo utakapoona siasa zilivyo SI-HASA
 
Pinda asafisha nyumbani kwa JK

Thursday, 21 January 2010 07:21

*Amtimua mkurugenzi, mweka hazina Bagamoyo
*Ni kwa tuhuma za ubadhirifu, kutowajibika


Na Edgar Nazar, Bagamoyo

WAZIRI Mkuu, Bw. Mizengo Pinda amegeuka mbogo na kuwavua madaraka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Mweka Hazina na maofisa wengine wa halmashauri hiyo kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa fedha za maendeleo ya umma na kushindwa kuwajibika ipasavyo.

Mbali ya hatua hiyo, Bw. Pinda alitoa onyo kuwa atakuwa mkali na asingependa kuona yaliyojitokeza katika halmshauri hiyo, ambayo ndio nyumbani kwa Rais Jakaya Kikwete, yakitokea kwingineko na kuwataka wakuu wa wilaya na mikoa kuzitizama halmashauri zao kwa jicho la karibu na kuwabana watendaji ambao wanaonekana kuwa walaji wa fedha za serikali.

Kama hiyo haitoshi, Bw. Pinda pia aliwaonya madiwani kuacha kupenda kuchukua posho kutoka kwa wakurugenzi wa halmashauri zao, hali ambayo inawafanya kuwa sehemu ya wakurugenzi na kushindwa kuwabana wanapoona kuwa wanakwenda kinyume, hivyo aliwataka kuwa wakali kama wabunge wanavyokua katika ukumbi wa bunge.

Hatua hizo za Bw. Pinda zilizoonekana jana alipokutana na viongozi na watendaji wa wilaya hiyo, zimetokana na mapendekezo ya ripoti ya uchunguzi uliofanywa Septemba na Oktoba mwaka jana na Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Serikali (CAG) uliobaini ukiukwaji mkubwa wa kanuni za fedha, uzembe na kushindwa kuwajibika na matokeo yake kuzorota kwa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo.

Watendaji walioshukiwa na Bw. Pinda ni pamoja na Bi. Rhoda Nsemwa (Mkurugenzi Mtendaji), Mweka hazina Bw, Carlo Wage, Mkaguzi wa Mahesabu wa Ndani, Bw, Abdul Mwinyi, Afisa Kilimo, Mifugo na Ushirika, Bw. Anaftal Remtulah pamoja na Ofisa Mipango, Bw. Aloyce Gabriel.

Akizungumza kwa ukali, Bw. Pinda alisema kuwa amechukizwa sana baada ya kupitia ripoti ya CAG na kugundua kuwa kuna matatizo katika kila kona, hali ambayo inaonesha wazi kuwa watendaji wakuu wa halmashauri wanahusika kwa kiasi kikubwa.

"Hawa watendaji ambao nimewavua madaraka kuanzia leo na saa hii, watachunguzwa na kama itathibitika kuwa na makosa ya jinai wanaweza kufukuzwa kazi au hata kupelekwa mahakamani na kushtakiwa au hata kushushwa vyeo walivyokuwa navyo kwa uzembe wa kutofuatilia shughuli za maendeo au kula fedha za serikali," alisema Bw. Pinda.

Watendaji wengine waliopitiwa na panga la Bw. Pinda ni pamoja na Mhandisi wa Ujenzi, Bw. Felix Ngomano, Mhandisi wa Maji, Bw. Galson Rafael ambaye ameondolewa katika nafasi hiyo na kubaki mtendaji wa kawaida baada ya kubainika kuwa hana sifa kushika nafasi hiyo.

Alisema kuwa baada ya kutokea kutokuelewana kati ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bw. Mugesa Mulongo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, Bi. Rhoda Nsemwa juu ya kuwepo miradi hewa, serikali iliamua kuwaleta wakaguzi ili kujua ukweli ambao sasa umebainika wazi.

Alisema kuwa katika ripoti hiyo kumebainika mapungufu makubwa yanayotokana na uzembe wa ufuatiliaji wa masuala ya maendeleo ya watu wa Bagamoyo, Baraza la Madiwani kutokuwa na nguvu ya kuhoji masuala yanayohusu maendeleo ya wananchi wao, hali ambayo imesababisha kuwepo kwa ubadhirifu katika miradi mingi ya maendeleo.

Kwa upande wa Ofisa Elimu wa Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Cheka Omar, yeye amewekwa chini ya usimamizi mkali na kama atabainika ameshindwa kazi kutokana na sekta ya elimu katika Wilaya ya Bagamoyo kuwa na matatizo makubwa naye atavuliwa madaraka aliyonayo.

Bw. Pinda alisema kuwa amewavua madaraka viongozi hao kuanzia jana kwa mujibu wa kanuni ya 37 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003 na watakuwa watendaji wa kawaida, huku wakiwa katika ukaguzi mkuu wa kuangalia kila sekta kama wataonekana kuwa wamefanya ubadhirifu wa makosa ya jinai sheria itafuata mkondo wake.

Bw. Pinda aliwataja watakaouchukua nafasi za watendaji walioondolewa kuwa ni Bw. Samuel Saiyanga kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya akitokea Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Vijijini, Bw. Fidelis Nenetwa atakuwa Mweka Hazina, akitokea Shinyanga.

Wengine walioteuliwa ni Fidelica Gabriel Myovelo, kutoka Wilaya ya Iringa ambaye atakuwa Ofisa Kilimo, Mifugo na Ushirika, Felista Chuki Masamba kuwa Mkaguzi wa Ndani kutoka Wilaya ya Lindi na Prudence Mtiganzi kuwa Mhandisi wa Maji kutoka Wilaya ya Kilombero, Ofisa Mipango mpya atakuwa Bw. Lucas Mweri kutoka Moshi.

Amesema kuwa watendaji hao wanatakiwa kufika mjini Bagamoyo haraka iwezekanavyo na kufanya shughuli za maendeleo kwa ufanisi kwani ana imani na watendaji hao hivyo, watafanya kazi zao kwa uadilifu mkubwa ili kuiendeleza Bagamoyo.

Gazeti hili lilipomfuata aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Bi. Nsemwa alisema kuwa ameridhika na uamuzi huo na kushukuru, huku akisema kuwa angeweza hata kutolewa roho yake kwa kuwa alikuwa anasakamwa sana.

Kauli hiyo ilienda sambamba na ile ya aliyekuwa Mweka Hazina, Bw. Wage ambaye alidai ameridhishwa na maamuzi hayo, ambayo yanamfanya kuwa na amani sasa, bila kufafanua alikuwa akimaanisha nini.
 
tena huyo Abdul Mwinyi mwizi mkubwa sana maana ndio alikua internal audit, limenenepa kwa wizi na ubadhirifu wa pesa za halmashauri ya bagamoyo. Lina roho mbaya sana na kila wakati kujisifia tu mimi ndio Internal audit wakati hata elimu yake ni ya kuunga unga na hastahili kwenye hiyo position. Sasa Mizengo imempindua chaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Eti wamechukua planning officer toka manispaa ya moshi? Mi nadhani kubadili teamwork kama ipo na inafanya vizuri ni vibaya, na kutegemea kuwa mtu ataperforme vizuri kama alivyofanya wakati yupo na team nzuri sawa na akiwa peke yake ni kujidanganya
 
Kutimua kazi siyo adhabu tosha kwa mtu aliyeiba mali ya umma! Kwanza kuweni makini kwa vile mliyemtimua anaweza kuwashitaki kwa kumtimua bila kufuata masharti ya mkataba wa ajira.
 
Matarajio yangu ni kuwa uwajibishaji wa wafanyakazi wabovu unatakiwa kuwa zoezi endelevu ndani ya mfumo rasmi wa utumishi wa umma. Kufanya operesheni sehemu (wilaya) moja tena inayovumishwa na media ilihali uozo umetanda kila mahali inakuwa kama kuendesha serikali kwa mtindo wa bahati nasibu. Kutuambia unatumia ushahidi wa ripoti ya CAG ambayo wakati mwingine hupuuza na wananci kudaiwa walete ushahidi wa ufisadi badala ya kupiga kelele amounts to an insult. How effective can that be? It's a questionable move. Only fools can be impressed!
 
Tunapenda mazingaombwe kweli!!

Mheshimiwa yale sio mazingaombwe, kazi ilikuwa ifanywe na waziri anaowasimamia. Lakini waziri akawa anayeyusha afanyi kazi aliyotakiwa kufanya. Na hao wafanyakazi wa halmashauri walishakuwa na uhakika wa kuwa waziri wao hatawafanya chochote.

Washikaji walikuwa wanachota fedha mradi, ukakuzi ukija wanachukua mafungu kwenye acc zingine na kuweka kwenye acc ya mradi, ukaguzi ukipita tu na hizo ndio chakula.

Mkuu wa wilaya aliposhitukia hiyo kuomba ushauri kwa mkuu wa wilaya fulani akaambia azifreeze hizo acc mpaka uchunguzi utakapokamilika, waziri anaehusika akamlima barua mkuu wa wilaya mshauri kwa kuingilia wilaya za watu. Mtoto wa mkulima akamwambia waziri atume barua ya kuondoa karipio hilo, waziri akatekeleza hivyo mkuu wa wilaya hiyo ametoa copy nakala kwa kila jirani hata kama uhusiki.

Muheshimiwa waziri huyo aliambiwa awawajibishe akawa anazungukazunguka, akamplekea mtu mkoani barua awawajibishe wakati hiyo ni kazi ya waziri, yule mtu akarudisha majibu kwa waziri kuwa hiyo ni kazi ya waziri. hata baada ya kupata hiyo barua bado akawa anacheza makidamakida.

Mtoto wa mkulima akaomba pande kutoka kwa muheshimiwa, ilipopigwa krosi akacheka na nyavu kwa kutumia vifungu vilevile alivyopaswa kutumia waziri husika.

Kwa kifupi mradi wa soko Bagamoyo kwenye makaratasi umeisha lakini ukweli hata msingi haujawekwa ndio maajabu ya halmashauri hayo.

Sasa sijui ndio ilikuwa mambo ya mzee hela ya msingi wa soko tumechukua mgao wako angalia kwenya acc yako, maana haya mambo ya halmashauri mazuri sana.

Maana kuna mtu alishawahi kusema mimi kazi halmashauri hata wakisema hatuwalipi mshahara mfanyekazi bure bila kulipwa, kazini hataacha kwenda.
 
Good Pinda, haya afuate boss wa PCCB ili tujue kweli umedhamiria. Najua tu utasema huyo hayuko chini yako yuko chini ya raisi. Mshauri raisi basi hadharani tujue kweli unataka aende kwa kuudanganya umma
 
Back
Top Bottom