Waziri Mkuu Pinda asitisha utekelezaji wa agizo la Magufuli la Bomoa bomoa

Kwani ukweli ni upi?
BORA NIKUELIMISHE WEWE UNAYETAKA KUJUA KULIKO BAADHI YA WATU AMBAO MAGUFULI AKISHASEMA HATA KAMA NI PROPAGANDA WAO WANAAMINI.

Ibara ya 2 ya Kanuni za Sheria ya barabara (Tangazo la Serikali Namba 161 la tarehe 5/5/1967) inatamka kuwa hifadhi ya barabara kuu zote hapa nchini (Trunk roads) ni Futi 75 kutoka katikati ya barabara. Vivyo hivyo Ibara ya 29 ya Kanuni za Sheria mpya ya barabara namba 13 ya 2007 (Tangazo la Serikali namba 21 la Tar 23 Januari 2009) (a) inatamka kuwa eneo la hifadhi ya barabara zote Kuu (Trunk Roads) za njia moja (Single Carriage way); na (b) kwa njia mbili (Dual Carriage ways) eneo la hifadhi barabara litakuwa ni Mita 60, yaani Mita 30 kila upande kutoka katikati ya barabara.

Ibara ya 27 ya Kanuni za sheria mpya ya barabara zilizotajwa hapo juu zinatamka kuwa upana wa njia moja ya barabara (lane) kwa barabara ya njia moja utakuwa si chini ya Mita 3.25 kwa njia moja ya kuelekea upande mmoja. Hivyo katika upanuzi wa barabara ya Morogoro, Mita 60 za hifadhi ya barabara zilizotengwa kama ilivyoelezwa hapo juu, zina uwezo wa kuzalisha njia 18 za barabara zenye upana uliotajwa hapo juu, yaani njia 9 za barabara za kutoka DSM kwenda Kibaha, na 9 za kutoka Kibaha kuja DSM.

Hivyo madai ya Wizara ya Miundo Mbinu kuwa msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro katika DSM na Kibaha husababishwa na wananchi waliojenga nyumba za makazi katika eneo lililo nje ya Mita 60, zilizotengwa kama hifadhi ya barabara hayana ukweli wowote. Eneo lililo nje ya Futi za 75 kutoka katikati ya barabara kwa mujibu wa Kanuni zilizotajwa hapo juu za 1967 liligawiwa kwa wananchi wakati Serikali ya awamu ya kwanza ilipokuwa kitekeleza sera ya Operesheni Vijiji.

Kimsingi Kanuni za Sheria ya barabara ya 1967 zilizokuwa zikitenga upana hifadhi ya barabara unaozidi Futi 75 (kati ya Mita 90 hadi 120) kati ya eneo la Ubungo hadi Kibaha zilikoma baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungo wa Tanzania kupitisha kwa Sheria inayolinda ugawaji wa ardhi uliofanyika chini ya operesheni vijiji kati ya Tar 01 Januari 1970 hadi kuanza kutumika kwa Sheria ya Ardhi namba 5 ya 1999 (Vifungu 15 na 16 vinatamka kuwa ugawaji wa ardhi uliofanywa mahali popote katika kijiji chini ya operesheni vijiji hata kama ni kwa kukiuka sheria yoyote ni halali na wenye kutoa haki ya wagawiwa kumiliki ardhi husika………).

Hivyo kitendo cha Wizara ya Ujenzi kuingia ndani ya ardhi na makazi ya wananchi Mita 90 hadi 120 pande zote mbili za barabara uliofanyika mwaka 2001, kati ya eneo la Ubungo hadi Kibaha na kupanda wa mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara ya Morogoro pasipo kushirikisha ngazi za Mkoa, Wilaya, Manispaa na Serikali za Mitaa ambazo zinzwafahamu na kuwatambua wananchi wanaohusika na sheria ya ardhi ya vijiji iliyotajwa hapo juu ulifanyika kimakosa na kusababisha athari kubwa sana za kijamii na kiuchumi kama vile kuwakosesha wananchi maeneo ya kutengeneza fursa za ajira, kujiajiri, huduma kama vile za kibenki, ATM n.k.

Mwaka 2010,ikiwa ni miaka 9 tokea uingiaji huo haramu, kitendo cha TANROAD kwa maagizo ya Wizara ya Miundo Mbinu kuingia ndani ya ardhi na makazi ya wananchi zaidi ya Futi 75 au Mita 22.86 na kufanya maendelezo yoyote ikiwemo ni pamoja na kuweka alama za X katika nyumba za wananchi ni haramu na ni cha kuwanyanyasa wananchi.
 
Pumba za serikali ya JK.Baraza la ki commed.

Tuwakaribishe TBC1 wajumuike na Kina masanja tuwaone siku ya alhamisi
 
Hii tabia ya kila kiongozi wa serikali kutoa tamko namna anavyoona yeye tena vikao vya barabarani inaonyesha kuwa kuna tatizo kubwa la uongozi (leadership) kwenye serikali kwa sasa.

Kibaya zaidi ili tatizo litaigharimu sana nchi na wananchi wake kwa sababu kila kiongozi atafanya lile ambalo anaona linafaa kwake yeye binafsi na hii ni hasara kubwa kwa taifa.

Leadership ni kitu muhimu sana mahali popote pale panapokuwa na watu au viumbe zaidi wa mmoja. Hata wanyama, wadudu, ndege wa angani, samaki wa baharini wana kiongozi wao na wanafuata kila kile kiongozi anacho fanya. Kiongozi si jina tu bali ni matendo. Kiongozi lazima kweli aonekane ni kiongozi na wale wanafuata watambue kuwa kuna kiongozi na watufuate njia zake.

Hii tabia ya viongozi wa serikali tena mawaziri kila mmoja kuja na kauli tofauti kwenye jambo moja kwa kweli inakera na kuchanganya sana wananchi.
 
Barabara zipite juu ya nyumba?
tunalalamika miundombinu hafifu, ikitaka kujengwa Pinda analeta siasa, basi kaeni kimya mpitishe magari na njia nyingine za usafiri juu ya hizo nyumba zenu, watu wa chato fikirieni mbele zaidi ya vibanda vyenu vya biashara, pisheni ujenzi wa barabara ili mfanye biashara kwa ufanisi zaidi kwani pale mtakapojengewa barabara, mtaweza kusafirisha na kununua bidhaa na hatimaye mtapata mafanikio zaidi ya mpatayo sasa
 
tunalalamika miundombinu hafifu, ikitaka kujengwa Pinda analeta siasa, basi kaeni kimya mpitishe magari na njia nyingine za usafiri juu ya hizo nyumba zenu, watu wa chato fikirieni mbele zaidi ya vibanda vyenu vya biashara, pisheni ujenzi wa barabara ili mfanye biashara kwa ufanisi zaidi kwani pale mtakapojengewa barabara, mtaweza kusafirisha na kununua bidhaa na hatimaye mtapata mafanikio zaidi ya mpatayo sasa

Ibara ya 2 ya Kanuni za Sheria ya barabara (Tangazo la Serikali Namba 161 la tarehe 5/5/1967) inatamka kuwa hifadhi ya barabara kuu zote hapa nchini (Trunk roads) ni Futi 75 kutoka katikati ya barabara. Vivyo hivyo Ibara ya 29 ya Kanuni za Sheria mpya ya barabara namba 13 ya 2007 (Tangazo la Serikali namba 21 la Tar 23 Januari 2009) (a) inatamka kuwa eneo la hifadhi ya barabara zote Kuu (Trunk Roads) za njia moja (Single Carriage way); na (b) kwa njia mbili (Dual Carriage ways) eneo la hifadhi barabara litakuwa ni Mita 60, yaani Mita 30 kila upande kutoka katikati ya barabara.

Ibara ya 27 ya Kanuni za sheria mpya ya barabara zilizotajwa hapo juu zinatamka kuwa upana wa njia moja ya barabara (lane) kwa barabara ya njia moja utakuwa si chini ya Mita 3.25 kwa njia moja ya kuelekea upande mmoja. Hivyo katika upanuzi wa barabara ya Morogoro, Mita 60 za hifadhi ya barabara zilizotengwa kama ilivyoelezwa hapo juu, zina uwezo wa kuzalisha njia 18 za barabara zenye upana uliotajwa hapo juu, yaani njia 9 za barabara za kutoka DSM kwenda Kibaha, na 9 za kutoka Kibaha kuja DSM.

Hivyo madai ya Wizara ya Miundo Mbinu kuwa msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro katika DSM na Kibaha husababishwa na wananchi waliojenga nyumba za makazi katika eneo lililo nje ya Mita 60, zilizotengwa kama hifadhi ya barabara hayana ukweli wowote. Eneo lililo nje ya Futi za 75 kutoka katikati ya barabara kwa mujibu wa Kanuni zilizotajwa hapo juu za 1967 liligawiwa kwa wananchi wakati Serikali ya awamu ya kwanza ilipokuwa kitekeleza sera ya Operesheni Vijiji.

Kimsingi Kanuni za Sheria ya barabara ya 1967 zilizokuwa zikitenga upana hifadhi ya barabara unaozidi Futi 75 (kati ya Mita 90 hadi 120) kati ya eneo la Ubungo hadi Kibaha zilikoma baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungo wa Tanzania kupitisha kwa Sheria inayolinda ugawaji wa ardhi uliofanyika chini ya operesheni vijiji kati ya Tar 01 Januari 1970 hadi kuanza kutumika kwa Sheria ya Ardhi namba 5 ya 1999 (Vifungu 15 na 16 vinatamka kuwa ugawaji wa ardhi uliofanywa mahali popote katika kijiji chini ya operesheni vijiji hata kama ni kwa kukiuka sheria yoyote ni halali na wenye kutoa haki ya wagawiwa kumiliki ardhi husika………).

Hivyo kitendo cha Wizara ya Ujenzi kuingia ndani ya ardhi na makazi ya wananchi Mita 90 hadi 120 pande zote mbili za barabara uliofanyika mwaka 2001, kati ya eneo la Ubungo hadi Kibaha na kupanda wa mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara ya Morogoro pasipo kushirikisha ngazi za Mkoa, Wilaya, Manispaa na Serikali za Mitaa ambazo zinzwafahamu na kuwatambua wananchi wanaohusika na sheria ya ardhi ya vijiji iliyotajwa hapo juu ulifanyika kimakosa na kusababisha athari kubwa sana za kijamii na kiuchumi kama vile kuwakosesha wananchi maeneo ya kutengeneza fursa za ajira, kujiajiri, huduma kama vile za kibenki, ATM n.k.

Mwaka 2010,ikiwa ni miaka 9 tokea uingiaji huo haramu, kitendo cha TANROAD kwa maagizo ya Wizara ya Miundo Mbinu kuingia ndani ya ardhi na makazi ya wananchi zaidi ya Futi 75 au Mita 22.86 na kufanya maendelezo yoyote ikiwemo ni pamoja na kuweka alama za X katika nyumba za wananchi ni haramu na ni cha kuwanyanyasa wananchi.
 
Mbona serikali haieleweki? Kuna haja gani ya kwenda kutangaza kwa wananchi badala yakumweleza waziri mwenye dhamana kisha yeye awatangazie wananchi? Me naona kama PM amemdhalilisha Magufuli kwamba alichofanya sio sahihi. Ina maana katika utendaji hakuna mipaka? imekuwa kila mtu achukulie anavyoweza? Na je! kauli mbiu ya CCM si ilikuwa ARI ZAIDI,NGUVU ZAIDI NA KASI ZAIDI? Sasa iweje Magufuli aonekane amekuja kwa Kasi zaidi kisha azimwe? Huko suio kumpandikizia chuki kwa wananchi? Au Serikali hua haina uhakika na kauli zake?Sio kwamba napinga kauli ya Pinda ila amekurupuka!alitakiwa atumie utaratibu unaotakiwa!
 
Utendaji wa serikali umekuwa wa aina ya Muziki wa mipasho wa kusubiri mwenzako aseme hiki nawe ujibu hivi! Kuna mambo mengi ya kuweka sawa...mabango hayakuwekwa jana barabarani,yanalipiwa ushuru as well...ujenzi usiofuata taratibu haukuanza mwaka jana,si Magufuli,si Waziri mkuu atayekwepa lawama katika hili,kwa kutambua hili ni busara kukutana wenyewe na kumaliza tofauti zenu huko kabla hamjaja na matamko yenu...tunataka mabadiliko si matamko!
 
Mbona serikali haieleweki? Kuna haja gani ya kwenda kutangaza kwa wananchi badala yakumweleza waziri mwenye dhamana kisha yeye awatangazie wananchi? Me naona kama PM amemdhalilisha Magufuli kwamba alichofanya sio sahihi. Ina maana katika utendaji hakuna mipaka? imekuwa kila mtu achukulie anavyoweza? Na je! kauli mbiu ya CCM si ilikuwa ARI ZAIDI,NGUVU ZAIDI NA KASI ZAIDI? Sasa iweje Magufuli aonekane amekuja kwa Kasi zaidi kisha azimwe? Huko suio kumpandikizia chuki kwa wananchi? Au Serikali hua haina uhakika na kauli zake?Sio kwamba napinga kauli ya Pinda ila amekurupuka!alitakiwa atumie utaratibu unaotakiwa!

(Me naona kama PM amemdhalilisha Magufuli kwamba alichofanya sio sahihi.) MAWAZIRI WAKU WAWILI LOWASSA NA PINDA HUKO NYUMA WAMEWAHI KUTOA MAAGIZO KUWA SUALA LA WAANCHI KUISHI KATIKA OAD RESERVE SERIKALI INA MCHANGO, HIVYO LITAKUWA LIKISHUGHULIKIWA ON CASE BY CASE BASIS PALE TU BARABARA FULANI INAPOTAKA KUJENGWA AU KUPANULIWA. KITENDO CHA MAGUFULI KUWELA X NCHI NZIMA NI DHARAU KWA MAWAZIRI WAKUU NA WANANCHI NCHI NZIMA WALIKUWA NA WAIS WASI HIVYO NI SAHIHI ALICHOFANYA PINDA KUWATOA WANANCHI HOFU.

Ina maana katika utendaji hakuna mipaka? imekuwa kila mtu achukulie anavyoweza? MAGUFULIA NDIO ALIKIUKA MIPAKA KWA KUINGILIA HALAMSHAURI ZA MIJI NA WILAYA NA KUINGILIA ARDHI NA MAKZI YA WANANCHI PASIPO KUTOA TAARIFA AU KUSHIRIKISHA NGAZI ZA MKOA, WILYA, MANASPAA AU SERIKALI ZA MITAA. IKAWA KAMA VILE SERIKALI YA ATZANIA NI MAGUFULI ANAWEZA KUFANYA CHOCHOTE NA MAISHA YA WATU ATAKAVYO.

Na je! kauli mbiu ya CCM si ilikuwa ARI ZAIDI,NGUVU ZAIDI NA KASI ZAIDI? Sasa iweje Magufuli aonekane amekuja kwa Kasi zaidi kisha azimwe? Huko suio kumpandikizia chuki kwa wananchi? IALANI YA CCM INASEMA ARI ZAID, NGUVU ZAIDI NA KASI ZAIDI KATIKA KUJENGA NA SIO KUBOMOA. YEYE KILA SIKU AKIAMKA NI KUBOMOA KUBOMOA KUBOMOA TU ILI AJIJENGEE SIFA KUTKA KWA WANANCHI. MWAKA 2001 ALIBOMOA PETROL STATION MWANZA AMBAPO SERIKALI ILILAZIMIKA KULIPA BILIONI 3 NDIO MAANA SAFARI HII PINDA KAWA MAKINI. KAMA NI CHUKI ANAJIJENGEA MWENYEWE KWA WANANCHI PALE ANAPOGEUZA SHERIA KUWA KAMA "MENU" KATIKA MIGAHAWA, ALIKUWEPO BUNGENI WAKATI SHERIA YA ARDHI NAMBA 5 INAPITISHWA MWAK 1999 NA ANAHAFAMU KUWA VIFUNGU 15 NA 16 VINAWALINDA WANACHI WALIOKUWA WAKIISHI NA WANAOENDELEA KUISHI VIJIJINI IWEJE MWAKA 2001 AINGIE MITA 120 NDANI YA ARDHI NA MAKZI YA WANANCHI? IWEJE 2010 AAGIZE NYUMB HIZO ZIBOMOLEWE?

Sio kwamba napinga kauli ya Pinda ila amekurupuka!alitakiwa atumie utaratibu unaotakiwa KWA KUWA MAGUFULI ALIKIUKA MAAGIZO YA MAWAZIRI WAKUU WAWILI PINDA ALICHOFANYA KAMA KIRANJA MKUU NI SAHIHI, KABISA LA SIVYO KWA JINSI MAGUFULI ALIVYO DIKTETA WIKI HII UNGESIKIA NYUMBA ZA WATU ZINABOMOLEWA; AU ULITAKA ASUBIRI MAPAKA MAANDAMANO YA WAATHIRIKA. ALIVUYOFANYA PINDA KWENDA KUMWAMBIA NYUMBANI KWAKE CHATO NI SAHIHI KABISA KWANI HATA WAO AMEWAONEA SANA, WALIKUWA HAWANA PA KUSEMEA TU.
 
Nafikiri hili agizo la Boss Pinda litachukuliwa kama agizo lake kuhusu mashangingi, kwa jinsi Mh. magufuli alivyo ataendelea tu kutekeleza aliyo yaanzisha.
 
Hivi viongozi wetu wamesomea wapi? Wana vyeti halali kweli? Maana nilitegemea wangeambiana wenyewe,Magufuli angekuja kusawazisha mwenyewe jukwaani.

Japo namuunga mkono PM (katika hili tu )kusawazisha huu uozo wa Magufuli kabla haujafanyiwa kazi, eti angevunja na jengo la tanesco..

sikubaliani na wewe katika hiyo haya ya red, kupisha ujenzi wa barabara sio uozo, kwani jengo la tanesco pale ubungo lina faida gani wakati umeme hatuuoni? jengo liko ndani ya ifadhi ya barabara hivyo halina budi kupisha, na kupisha kwake ni kubomolewa tu. by the way usafiri ni shida sana moro road, kwani traff jam yake ni kubwa sana, hivyo ni bora barabara likapanuliwa.
 
HTML:
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mohamed Babu, ampatie orodha ya wafanyabiashara wanaonunua sukari kutoka katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera, ili ajue sababu za kuuza bidhaa hiyo kwa bei ya juu.

Source - Mwananchi

WM wetu ni kama employee tu anayefanya kazi ili mradi kusubiri ujira mwisho wa mwezi! Mara nyingi anatoa statements zinazoishia hewani tu .... na zingine hazina mantiki kama hiyo hapo juu.
ni kwaida yake mkuu, sijui anataka nini kwa wananchi, si wakati wa kuagiza na kutoa matamko tunataka maendeleo
 
ili maendeleo yawepo mahali popote pale lazima baadhi ya watu wataadhirika na hapo ndipo sasa wanasiasa wapenda sifa hujitokeza na kutoa matamshi yao yakilenga kumponda yule anayetaka kufanya vitu vya maana kwa jamii kubwa. Sasa hii tanzania ya leo kuna sehemu utake kujenga barabara, kiwanja cha ndege ama soko la kisasa bila kubomoa au kuharibu mashamba ya watu!! Mi nadhani siasa ikizidi wakati mwingine inachelewesha maendeleo.
 
Hii serikali bogus kabisa, yaani wanaandaa mpango wa kupinda sheria walizotunga wao, na ndo maana miji mingi imejengwa hovyo sababu watu wanajua serikali itapindisha sheria tu. Bogus. I love Dr. Magufuli hate Pinda.
 
ufanisi? Ni ule uliosababisha serikali kulipa fidia ya bilioni 3 kwa kubomoa petrol station jijini mwanza kwa madai kuwa imejengwa katika hifadhi ya barabara au upi?<br />
<br />)

Jatropher usilete chuki zako kuhalalisha upuuuzi kama huo!, usihadae wana jf kwa kurejea kesi ambazo serikali ilipoteza! Nani hajui kama ''law'' ni ''art''? Mbona mkataba dowans ulisitishwa kihalali lakini kesi tukapoteza?, nani hajui kama Zombe na wenzake waliua lakini wako mtaani wanakula kuku?, nani hajui kama babu seya na wanae hawakubaka lakini wako wanaendelea kunyea debe?, sheria ni sanaa na hapa tanzania inaongozwa na rushwa, na kama ujuavyo serikali haitoi rushwa kwa hiyo haishindi kesi nyingi!, hilo unalijua. Magufuli ni mchapa kazi na anafuata sheria. Sio ndugu yako huyo anakurupuka kusema wanaoua arubino wauawe halafu analia mwenyewe! PM AMECHEMKA, usitetee ujinga eti kisa magufuli aligusa interest zako! Koma
 
Ukikaa na kundi la wajinga hata wewe unakuwa jinga: haya niliyategemea kwa Pinda! Hata hivyo hawa nao wanang'ang'ania nini CCM kama siyo wezi tu' eeehh huyo SITA na MAGUFULI hata Mwakyembe???? nashindwa kuwavumilia ama watoke huko CCM ama nao waendelee kuwa wabaya wa wapenda maendeleo Tanzania
 
Pinda ni waziri mkuu dhaifu kabisa nchi hii kuwahi kuwa nae?!! hafai hata kidogo anajifanya mtu wa huruma kama hivo mbona hajakamata hata mtu mmoja wa Kagoda?!!!
 
jatropha anavyojitahidi kuhadaa watu kuonesha mapungufu ya magufuli nadhani ataku na mrema aliekua tanroads!
 
Huyu pinda unafiki umemzidia, mbali na kusema uongo bungeni kwenye mambo mengi ya msingi ambapo alipaswa kuonyesha uzalendo sanasana ataishia kulia ili aonewe huruma. Eti huyu ndiye anaamuru mitambo ya DOWANS iwashwe huku akijua suala liko mahakani na kabla hata juma halijaisha anasimamisha kubomoa. Sheria ziko wapi jamani!!!! HUYU JAMAA SASA ANADHIIRISHA KUWA NI ZIGO AMBALO HATUKULITEGEMEA KABISA! nchi iendelee kuwa slums tu!!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom