Mpasuajipu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2010
- 836
- 49
Ama kweli choo hakiachi kunuka hata kisafishwe kwa detol
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wazee nimesikia kwenye taarifa ya habari usiku huu kupitia RFA kwamba Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesitisha ubomoaji wa majengo yaliyojengwa ndani ya hifadhi ya barabara nchini kote. Najua ubomoaji huo ulikuwa unafanywa kwa amri ya Mhe. Pombe Magufuli. Hii amri ya Pinda, imekaaje wazee? Au ndiyo mwendelezo wa tabia ile ile ya serikali yetu ya sasa ambapo kila kiongozi anafanya kazi na kutoa statements kadri anavyojisikia? Mhe. Magufuli atajisikiaje?
Ku over-rule amri ya waziri wake hadharani ni jambo baya sana. Kwa nini wasingejadiliana halafu akamuacha Magufuli asitishe? Hii inaonesha kuwa CCM na serikali yake imechanganyikiwa, kila mtu atakuja na lake irimradi kujisafisha kumbe wanatibuana na kuadhiriana. Kama hakujadiliana na Magufuli mi nashauri Magufuli ajiuzulu tu, maana kafanywa hajui kazi.
Ndicho kinachonishangaza. Serikali inayoendeshwa kwa umakini na ustaarabu, haiwezi kuwa na statements za viongozi wake waandamizi kama mawaziri zinazokinzana. Nionavyo mimi nadhani Pinda ilikuwa vizuri na hekima kumwita Mhe. Magufuli na kujadiliana nae kuhusu zoezi hilo la bomoabomoa. Baada ya majadiliano, kama ingeonekana ni muhimu zoezi lisitishwe basi amri ya kusitisha angeitoa Mhe. Magufuli mwenyewe na siyo Pinda. Njia hiyo isingejenga taswira mbaya mbele ya wananchi na kwa Magufuli mwenyewe.