Pinda ashtushwa na umaskini uliokithiri ukerewe, ashangaa mkurugenzi kukosa ubunifu.

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Mwandishi wetu, Ukerewe-Mwanza Yetu

MKURUGENZI Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ukerewe, Mwanza Dr. Leonard Masale ametakiwa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na tatizo la umasikini linalowakabili wakazi wa wilaya hiyo.

Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo iliyosomwa na mkuu wa wilaya hiyo Bi, Mery Tesha

Akionekana kushutushwa na hali ya umasikini inayowakabili wakazi wa wilaya hiyo alisema hatakubali kuona tatizo hilo linaendelea wakati viongozi wa wilaya hiyo na mkoa wakibaki bila kubuni na kuanzisha miradi ya kulitatua matatizo
yanayowakabili wa kazi wa wilaya hiyo.

Alisema wakati wilaya nyingine za mkoa wa Mwanza wakazi wake wanakipato cha wasitani ya sh. 926,000 kwa mwaka katika wilaya ya Ukerewe pato la mwananchi ni wasitani wa sh. 340,000.

Alisema wasitani wa kipato cha mkazi wa Ukerewe unaonyesha kuwa kwa siku anapata sh. 800 kiasi ambacho ni chini ya makisio ya pato la taifa la sh. 1,500 kwa mtanzania kwa siku .

Kufuatia hali hiyo amemuagiza Dk. Masale kubuni miradi yenye tija ya kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo Ufugaji nyuki, kilimo na kuhakikisha pato la uvuvi linapatika na kuwanufaisha wakazi wa wilaya hiyo.

Akieleza zaidi Pinda alisema wakati asilimia 90 ya wilaya hiyo ni eneo la maji ya ziwa Victoria lakini pato linalotokana na rasilimali hiyo aliwanufaishi wakazi wake na kutaka juudi za makusudi zichukuliwe ili wananchi waondokane na umasikini uliokkisili.

Naye Dr. Masale alisema hatua mbali mabali za kukabiliana na tatizo hilo zinafanyika ikiwemo kuboresha ufugaji pamoja na kutoa mafunzo ya kilimo na ufugaji bora pamoja na kutoa mbegu bora za mazao ya chakula na biashara zinazoimili magonjwa.

Blogzamikoa

www.blogszamikoa.blogspot.com

Wilaya ya Ukerewe ni Masikini lakini kuna pesa za KUWAJENG EA VIGOGO WA CHAMA TAWALA MAHEKALU; YEYE Watoto Wake Wote

Wameendelea KIMASOMO Na Kikazi baadhi yao WAMEPATA UPENDELEO WA SERIKALI TAWALA...

HEKALU LIKIFUNGULIWA wanasema ni JENGO la VIONGOZI... NI PIUS MSEKWA ??

mail.google.comc.jpg

KLumbe Pinda kigeugeu? Anapojiita mtoto wa mkulima na kujifanya hajui umaskini maana yake nini? Hili ndilo tatizo la watawala wetu. Wakipata madaraka wanajisahau kuwa ni binadamu na hataki kuuona ukweli bali kujifanya kushangaa wakati huu umaskini unasababishwa nao kutokana na wizi na kukosa sera na mipango madhubuti kuendesha nchi. Shame on you Pinda.
 
Lowassa alipokuwa Waziri Mkuu; alitembelea UKEREWE na kama sikusahau aliulizwa SWALI na MTOTO W PRIMARY SCHOOL

kwanini WAO VIONGOZI Wana-Vyeo Vingi (Wajilimbikizia Vyeo) ? Sasa Lowassa aliona hayo hayo PINDA aliona na labda

maendeleo MABAYA ZAIDI; Lakini Lowassa hakusema CHOCHOTE ? Ina Maana aliridhika na UMASIKINI UKEREWE? NDIO

HUYU TUNAYEMTAKA KUWA RAIS WA NCHI?????
 
Yeye amebuni nini kuiepusha nchi na umaskini. Rukwa si ni kati ya mikoa maskini nchini?? Amefanya nini huko kwao zaidi ya mkoa kujulikana kwa uchawi!!
 
Pale uliposema Lowasa ndo TUNAYETAKA awe rais. Hiyo TU mwingine ni nani?

Oh... Ni JINSI ninvyoona anavyojipandikiza MADARAKANI... kugawa MADAWATI, KUTEMBELEA BALOZI... kugombana na

MEMBE na RIDHWAN yuko kwa MEMBE Unaona kabisa ni fight ya URAIS HIYO; Au Mlio Tanzania Mnaona MENGINE???
 
MKURUGENZI Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ukerewe, Mwanza Dr. Leonard Masale ametakiwa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na tatizo la umasikini linalowakabili wakazi wa wilaya hiyo.

Agizo hilo limetolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya wilaya hiyo iliyosomwa na mkuu wa wilaya hiyo Bi, Mery Tesha

Akionekana kushutushwa na hali ya umasikini inayowakabili wakazi wa wilaya hiyo alisema hatakubali kuona tatizo hilo linaendelea wakati viongozi wa wilaya hiyo na mkoa wakibaki bila kubuni na kuanzisha miradi ya kulitatua matatizo
yanayowakabili wa kazi wa wilaya hiyo.

Alisema wakati wilaya nyingine za mkoa wa Mwanza wakazi wake wanakipato cha wasitani ya sh. 926,000 kwa mwaka katika wilaya ya Ukerewe pato la mwananchi ni wasitani wa sh. 340,000.

Alisema wasitani wa kipato cha mkazi wa Ukerewe unaonyesha kuwa kwa siku anapata sh. 800 kiasi ambacho ni chini ya makisio ya pato la taifa la sh. 1,500 kwa mtanzania kwa siku .

Kufuatia hali hiyo amemuagiza Dk. Masale kubuni miradi yenye tija ya kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo Ufugaji nyuki, kilimo na kuhakikisha pato la uvuvi linapatika na kuwanufaisha wakazi wa wilaya hiyo.

Akieleza zaidi Pinda alisema wakati asilimia 90 ya wilaya hiyo ni eneo la maji ya ziwa Victoria lakini pato linalotokana na rasilimali hiyo aliwanufaishi wakazi wake na kutaka juudi za makusudi zichukuliwe ili wananchi waondokane na umasikini uliokkisili.

Naye Dr. Masale alisema hatua mbali mabali za kukabiliana na tatizo hilo zinafanyika ikiwemo kuboresha ufugaji pamoja na kutoa mafunzo ya kilimo na ufugaji bora pamoja na kutoa mbegu bora za mazao ya chakula na biashara zinazoimili magonjwa.

Kuna mtoa maada humu ndani alisema wanandoa wakikaa muda mrefu hufanana kwa sura na tabia. Ha pa naamini kwani hata JK alisema anashangaa kwa nini Tz ni maskini. Hivyo mie nasubiri
 
Agreed.
Na mbona tumezoea hawa, wanashtushwa, wanatoa maagizo (Dhaifu alitoa agizo la nyumba DC miaka hiyooo) then wanaondoka na kusahau kila kitu !!!
Huyu alikuwa mtoto wa mkulima zamani, boss wake Dhaifu kashamfundisha ujambazi- kamuunganishia dili na wale matapeli wa USA, wakapora mashamba, akaja USA na baadhi ya madiwani kwa kulipiwa kila kitu- rushwa- sasa hivi amerundika miradi kwao- baada ya kugawiwa mkoa mzima wenye wilaya moja (haijawahi kutokea) na anajiandaa kuishi kifisadi !! Na ule uwanja wa kimataifa anajua atasafirisha sana wanyama kutoka mbuga za Katavi na maeneo jirani !

Sasa Pinda ameshtushwa utadhani ANC ndio chama tawala Tanzania??
 
Back
Top Bottom