Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,163
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Akitangaza uamuzi huo mkoani Mara leo (Jumatano Julai 1, 2009) Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda alisema itaazishwa piakambi ya Jeshi la Kujenga Taifa na kuimarisha miundombinu ya barabara kwa madhumuni hayo hayo.
Waziri Mkuu alikuwa akihutubia sherehe za Siku ya Serikali za Mitaa kwenye uwanja wa Mkendo mjini Musoma leo na baadaye alipotembelea maeneo yaliyokumbwa na mauaji katika wilaya za Rorya na Tarime leo (Jumatano, Julai 1, 2009).
Waziri Mkuu pia alisema anatoa miezi sita kwa uongozi wa wilaya hizo na mkoa kwa jumla kuandaa mkakakati na kuuwasilisha serikalini jinsi ya kukomesha mauaji hayo ama sivyo maeneo hayo yatatawaliwa kijeshi kwa kuwa utawala wa kiraia utakuwa umeshindwa.
Madhumuni ni kuhakikisha amani na usalama wa raia katika maeneo hayo. Serikali imechoshwa na mauaji haya, alisema.
Katika matukio ya hivi karibuni, zaidi ya wiki moja iliyopita, mpaka sasa watu 32 wameuawa katika mapigno kufuatia wizi wa ngombe watano ambao kati yao ng,ombe watatu walipatikana.
Nyumba zaidi ya 400 zimechomwa na watu zaidi ya 3,000 wamekosa mahali pa kukaa.
Serikali imekwishadhibiti ulinzi na usalama katika maeneo hayo kwa kuowangeza nguvu za polisi na imeanza kutoa msaada kwa walioathirika.
Waziri Mkuu alisema ni aibu mauaji kama hayo kutokea nchini kwa hivi sasa lakini inaonekana pia kuwa viongozi wa wa kiraia wa maeneo hayo wameshindwa kazi kwani ni wajibu wao kuyazuia tangu mapema.
Alisema Serikali inachukua hatua za hadhari hivi sasa za muda mfupi, lakini za muda mrefu zitategemea mkakati wa viongozi wa wilaya hizo za Tarime na Rorya na mkoa mzima wa Mara.
Waziri Mkuu pia alitembelea kwa helikopta na kutuaalipata kwenye maeneo yaliyotokea maafa hayo katika wilaya za Rorya na Tarime na kuzungumza na wananchi. Aliambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali SaidMwema ambaye amekuwepo mkoani Mara kwa siku kadhaa akiwa na baadhi ya makamanda wake wakuu.
Katika eneo la Changuge, wilayani Rorya, wananchi waliopewa nafasi na Waziri Mkuu kutoa kero zao walimthibitishia kuwa mauaji hayo siyo ya kikabila na ya koo kati ya Wakurya wa Tarime na Wajaluo wa Rorya bali ni kati ya raia wema na majambazi wezi wa mifugo.
Waliiomba Serikali kuimarisha ulinzi kwa kuongeza askari polisi na zana.
Mbunge wa Rorya, Prof. Philemon Sarungi alimwambia Waziri Mkuu kuwa zaidi ya ngombe 2,000 wameibiwa mpaka sasa katika wizi huo.
Katika maeneo hayo yaliyokuwa na mauaji, Waziri Mkuu alifuatana pia na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Said Mwema.
Akizungumzia Siku ya Serikali za Mitaa, Waziri Mkuu alisema kuendeleza kwa pamoja sekta za kilimo, mifugo na uvuvi, ndiyo njia pekee ya kuondoa umasikini nchini.
Waziri Mkuu alisema kuwa kuanzia sasa, uongozi bora wa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya,Wenyeviti wa Halmashauti na Wakurugenzi, utapimwa kwa jinsi wanavyohimiza na kusimamia kwa vitendo kilimo, ufugaji na uvuvi.
Alisema viongozi waonyeshe uongozi wao kwa vitendo huko vijijini na siyo kukaa ofisini tu mijini.
(mwisho)
Imetolewa na:
Ofisi ya Waziri Mkuu
S.L.P. 3021
DAR ES SALAAM
Jumatano Julai 1, 2009