Pinda aogopa wimbi la umma kumng'oa ya JK, aomba mjadala wa ulinzi kitaifa kunusuru

Not_Yet_Uhuru

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,304
431
Katika hali inayoonyesha wasiwasi halisi alio nao JK na utawala wake kuhusu hali iliyoikumba Tunisia kwa umma kuchukua madaraka ya nchi kutokana na utawala mbovu, maisha magumu pamoja na rushwa, hali ambayo inaweza kutokea hapa tanzania na jeshi lao kukwama kutuliza mambo, Pinda amefikia hatua ya kujitwika zigo la JK na kuomba mjadala wa kitaifa kuhusu hali ya ulinzi nchini. Ameyasema haya ktk semina fupi 'elekezi' Dodoma na watendaji wapya wa halmashauri, ikijumuisha pia madiwani, wakurugenzi nk.
source TBC1

My take:
Hii inadhihirishwa ukweli kuwa hali ni tete na serikali haina uhakika na majeshi yake na haijui nini kitatokea kesho kama nguvu ya umma itafuata nyayo za wananchi wa Tunisia kwa kuingia mabarabarani. JK hapati usingizi sasa na hataupata.

naomba kuwasilisha.
 
Mh great thinker hop u miss interpreted the information,mbona pinda kaeleza vizur na waz kuwa maeneo anayoona yanahtaj zaid ulinz zaid nchin kutokana na ujambaz ni Ruvum,Kigoma na mkoa mpya.felows let we post topics we ar sure of.
 
Kwa yaliyompata yule fisadi wa kiarabu, sasa tumbo joto........ usingizi hakuna tena, maisha yanavozidi kuwa magumu kwa watanzania wa kawaida!!!!!!!!!
 
Tbc naona toka wamemchakachua TIDO imebadilika!

I miss TBC taaluma iliokua chini ya Mhe Tido Mhando! Nakerwa sana na TBC propaganda iliozaliwa takriban wiki 3 sasa. Kasi ya TBC kuelekea enzi za ujima na waziri wa habari kugeuka kuwa mhariri mkuu ndio huu hapa.
 
Mimi binafsi namshangaa Pinda. Alistahili kujiuzulu siku nyingi sana. Amejijengea heshima kwa miaka yake yote. Watu watamsamehe kwa awamu iliyopita. Lakini sasa hana budi kukataa kuwa associate wa JK. Waziri gani mkuu wakati mawaziri wanaropoka kivyao, ambaye hana mamlaka, ushauri hausikilizwi.
Pinda ndugu yangu jipinde achana na hii serikali, hutafanya jema lakini utaingia kwenye historia mbaya. Wewe si fisadi au wamekubatiza sasa? UUngwana wako nikujiuzulu mapema
Huu ni ushari tu au mnasemaje jamani?
 
" Dodoma: Waziri Mkuu (Mh) Mizengo Pinda ... amesema Serikali inaagalia uwezekano wa kuimarisha Ulinzi katika mikoa ya ....."

Source: Radio One

Sijui maana ya neno "kuangalia uwezekano" ni nini? Hivi si ni jukumu la Serikali Kulinda Raia na Mali zao? Kwa nini iwe ni kuangalia uwezekano?
 
Baba E unashangaa hili mbona dogo? Mwaka jana kwenye moja ya events, boss wake na huyu pm kibogoyo alisema serikali itatoa msaada wa vifaa kwa jeshi la polisi ili liweze kusimamia vizuri uchaguzi mkuu.By the way sikusimuliwa nilimwona mwenyewe kwenye luninga live bila chenga. Aliniacha hoi sana sana, nikajiuliza hivi serikali ni nini, msaada ni nini na jeshi la polisi ni nini. Yote nilikosa majibu yake. Sasa nikijumlisha na haya ya mtoto wa mkulima ndio naishiwa nguvu kabisa. Does this mean rais na pm wake hawajuwi nini wajibu wa serikali wanayoiongoza which means hawaijui hata katiba wanayoisamamia? Nasuburi siku nyingine akisema serikali itatoa msaada wa ujenzi wa barabara tena nahisi haiko mbali sana.
 
Katika hali inayoonyesha wasiwasi halisi alio nao JK na utawala wake kuhusu hali iliyoikumba Tunisia kwa umma kuchukua madaraka ya nchi kutokana na utawala mbovu, maisha magumu pamoja na rushwa, hali ambayo inaweza kutokea hapa tanzania na jeshi lao kukwama kutuliza mambo, Pinda amefikia hatua ya kujitwika zigo la JK na kuomba mjadala wa kitaifa kuhusu hali ya ulinzi nchini. Ameyasema haya ktk semina fupi 'elekezi' Dodoma na watendaji wapya wa halmashauri, ikijumuisha pia madiwani, wakurugenzi nk.
source TBC1

My take:
Hii inadhihirishwa ukweli kuwa hali ni tete na serikali haina uhakika na majeshi yake na haijui nini kitatokea kesho kama nguvu ya umma itafuata nyayo za wananchi wa Tunisia kwa kuingia mabarabarani. JK hapati usingizi sasa na hataupata.

naomba kuwasilisha.

Tatizo la huyu mtoto wa mkulima hajiamini na pia anaweza kuwa na inferiority complex kitu ambacho hapaswi kuwa nacho kwa dhamana aliyopewa kuongoza Serikali.

Inakuwaje unataka Ulinzi wakati una usalama wa Taifa, Police, JWTZ, JKT, unakusanya kodi. Huu ni upuuzi, ndio maana hata alishindwa kuwakamata wauaji wa Albino akaishia kulialia bungeni.

I hate such complex, UWT wanashindwa kufanya kazi zao kisa wamekuwa wanasiasa, Polisi pia, tumeona kwa Mwema alivyokuwa mwanasiasa, JWTZ nao hawako nje ya siasa, tulimwona Shimbo.

Sasa anataka ulinzi shirikishi kila kona, what for?
 
Katika hali inayoonyesha wasiwasi halisi alio nao JK na utawala wake kuhusu hali iliyoikumba Tunisia kwa umma kuchukua madaraka ya nchi kutokana na utawala mbovu, maisha magumu pamoja na rushwa, hali ambayo inaweza kutokea hapa tanzania na jeshi lao kukwama kutuliza mambo, Pinda amefikia hatua ya kujitwika zigo la JK na kuomba mjadala wa kitaifa kuhusu hali ya ulinzi nchini. Ameyasema haya ktk semina fupi 'elekezi' Dodoma na watendaji wapya wa halmashauri, ikijumuisha pia madiwani, wakurugenzi nk.
source TBC1

My take:
Hii inadhihirishwa ukweli kuwa hali ni tete na serikali haina uhakika na majeshi yake na haijui nini kitatokea kesho kama nguvu ya umma itafuata nyayo za wananchi wa Tunisia kwa kuingia mabarabarani. JK hapati usingizi sasa na hataupata.

naomba kuwasilisha.

Du, kweli ww ni mpotoshaji humu JF hakuna mfano wake, na uwe unasikiliza habari na kuielewa, umejitia aibu kwa kuonyesha uwezo wako mdogo wa kufikiri na kuchambua mambo. Alichosema Pinda, ni kuhusu kuimarisha ulinzi kwenye mikoa ambayo inapakana na nchi jirani km Kagera, Kigoma , Rukwa ili kuondoa / kupunguza matukio ya ujambazi na utekaji nyara na si suala la ulinzi wa madaraka ya JK. Na kwa taarifa yako , katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara Tanzania ndio nchi iliyo na jeshi imara na lenye nguvu
 
mh great thinker hop u miss interpreted the information,mbona pinda kaeleza vizur na waz kuwa maeneo anayoona yanahtaj zaid ulinz zaid nchin kutokana na ujambaz ni ruvum,kigoma na mkoa mpya.felows let we post topics we ar sure of.
kwa hiyo tukuamini wewe zaidi,kwa kuwa wewe ndiyo msema kweli!!
 
" Dodoma: Waziri Mkuu (Mh) Mizengo Pinda ... amesema Serikali inaagalia uwezekano wa kuimarisha Ulinzi katika mikoa ya ....."

Source: Radio One

Sijui maana ya neno "kuangalia uwezekano" ni nini? Hivi si ni jukumu la Serikali Kulinda Raia na Mali zao? Kwa nini iwe ni kuangalia uwezekano?

Maana yake ni kuwa makini zaidi!!
 
Back
Top Bottom