Pinda amvaa Lowassa: "Kuvunja Baraza" yataka moyo!

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Wakati akiendelea na hoja zake mambo yafuatayo yamekuwa ni ushindi kwa CHADEMA.

  1. Kuhusu mauaji yanayofanywa na jeshi la polisi - sasa wamekubaliana na hoja ya CDM ya kutaka ufanyike uchunguzi na kuanzisha mahakama maalum ya kusimamia suala hilo kwa kutumia sheria ya Inquest na kuundwa kwa Corronas court.
  2. kuanzisha utaratibu wa kila wilaya kuwa na mpango wake wa maendeleo (District Economic Master Plan).
  3. kuundwa kwa kamati ya kudumu ya bunge ya kupambana na Rushwa na isimamiwe na kambi ya Upinzani bungeni.
  4. kuangalia suala la posho na kufanya utaratibu mpya.
  5. kufanya marekebisho ya sheria na kuzifanya Halimashauri ziwe na uwezo wa kuajiri watumishi wake.
  6. kuhusu ajali za barabarani

haya ni baadhi ya mambo ila kuna haja ya kuipata hansard nzima na kuona yalivyojibiwa mambo yaliyoibuliwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe.Mbowe wakati akiwasilisha hotuba ya Kambi ya upinzani.

La kushangaza ni kuwa naona ameamua kumtolea uvivu Lowassa na kumueleza kuwa serikali inafanya maamuzi magumu na imewahi kuamua waziri mkuu na baraza la mawaziri kuondoka akiwamo yeye Lowassa na huo ni uamuzi mgumu , na akamwahidi kuwa bado watafanya maamuzi magumu zaidi.

Notices za alichoongea bungeni zimeambatanishwa chini
 

Attachments

  • NOTES ZA Hon MIZENGO Pinda.pdf
    545.4 KB · Views: 362
Mkuu tuko mbali na tv na umeme wetu wa mgao tunaomba taarifa zaidi mkuu ya kilichotokea maana hapo ni kama umetuonjesha pipi
 
Kuna hoja wakati wa kushika vifungu zimetengwa shilingi milioni mbili kwa ajili ya kujenga barabara na madaraja ........Lukuvi ameshindwa kujibu anasema ni madaraja yaliyopo nyumbanmi kwa waziri Mkuu.
 
bado wanaendelea ndio wabunge wamesimama kung'ang'ania mshahara wa waziri mkuu na haswa kutaka hoja mbalimbali ziweze kujibiwa kama hazikujibiwa kikamilifu.

L a Lowassa limestua watu sana kwani ni kama aliamua kumvaa moja kwa moja .
 
Pia madiwani wataongezewa osho kuwa kati ya laki 3 na laki5, na posho za wabunge kuongezwa kwenye mishahara midogo ya wabunge
 
Asante sana
Anajitengea pesa kw aajili ya kujenga madaraja kwake wakati sehem kibao zina shida
 
Pia madiwani wataongezewa osho kuwa kati ya laki 3 na laki5, na posho za wabunge kuongezwa kwenye mishahara midogo ya wabunge

Mkuu fafanua madiwani kulipwa laki tatu mpaka tano ni posho au mshahara
na zile sitting allowance zao wanazojipangia kwa kila kikao
 
Kuna hoja wakati wa kushika vifungu zimetengwa shilingi milioni mbili kwa ajili ya kujenga barabara na madaraja ........Lukuvi ameshindwa kujibu anasema ni madaraja yaliyopo nyumbanmi kwa waziri Mkuu.

Mkuu umekosea wewe au ndicho kilichotajwa?! MILIONI MBILI KUJENGA DARAJA NA BARABARA?! MILIONI? Nnachofahamu mimi km 1 ya barabara ni zaidi ya 1.2 billions!
 
sasa wamebanwa kuwa wanapaswa kuleta sera kuhusiana na posho na matumizi ya serikali ndani ya mwaka mmoja , ila wamesisitiza kuwa wataileta ndani ya miaka mitano ijayo katika kupunguza posho na aina ya magari yatakayokuwa yanatumiwa na viongozi wa serikali .

Hili nalo ni jambo jema ambalo wamelikubali muda huu baada ya Lukuvi kujibu.
 
Milioni mbili , na jibu likawa kuwa ni kujenga madaraja yaliyopo nyumbani kwa waziri mkuu na aliyejibu ni Lukuvi kila mmoja anashangaa nyumbani kwa Pinda kuna madaraja gani?
 
nimeisikia lakini ana base sana kwenye takwimu kama kwenye suala la TAKUKURU, kiukweli hawa jamaa wako dhaifu sana na naona anawatetea
 
Suala hilo lipo kwenye kitabu cha serikali cha matumizi volume II. VOTE 25 ofisi ya waziri mkuu ,chini ya kifungu kinachoitwa programme 10 adminstration and General kifungu kidogo cha 230100 ambacho kimeandikwa "routine maintanance and repair of roads and bridges" na zimetengwa shilingi milioni mbili za kitanzania .
 
HOJA YA SERIKALI KUFANYA MAAMUZI MAGUMU


· Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wametupatia Changamoto kuhusu Hoja ya kutaka Serikali kufanya maamuzi na hasa maamuzi waliyoyaita magumu.

Mheshimiwa Spika,
· Awali niseme kuwa Serikali ya Awamu ya Nne imekuwa ikifanya maamuzi thabiti na magumu lakini kwa busara na tahadhari ili kutenda haki na kwa kuzingatia uwezo wa Serikali ili kulinda maslahi ya Wananchi kudumisha Amani. Katika kufanya maamuzi hayo, Serikali imekuwa makini kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu.

· Tunatambua kuwa moja ya sifa za Kiongozi ni kuweza kufanya maamuzi. Tunayo historia ya Viongozi ambao tunawakumbuka kwa maamuzi yao kwa Taifa hili.

· Mfano mzuri, ni Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Wakati wa Uongozi wake, moja ya Maamuzi magumu ambayo aliyafanya na tunayakumbuka ni kuruhusu Nchi yetu kuingia katika harakati za kusaidia Nchi za Bara la Afrika ambazo zilikuwa hazijapata Uhuru. Tunayo mifano ya Nchi za Angola, Afrika Kusini, Msumbiji, Namibia, Zimbabwe, kwa kutaja chache tu, ambazo kwa maneno yake alisema: "Hatuwezi kuwa huru kama baadhi ya Nchi za Waafrika Wenzetu bado zinatawaliwa na bado haziko huru.

· Vilevile, tunakumbuka uamuzi mgumu uliofanywa na Baba wa Taifa kuwasaidia Ndugu zetu wa Uganda kujikomboa kutoka kwenye Utawala wa Dikteta Iddi Amin. Lakini pia tunakumbuka uamuzi mzito uliofanywa na Baba wa Taifa kuhusu vita dhidi ya Walanguzi, uamuzi ambao ulisababisha baadhi ya Wafanyabiashara kutupa bidhaa Barabarani. Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pia alifanya maamuzi mengi mazito ambayo yalituletea maendeleo katika Nchi yetu.

· Yapo pia maeneo mengi ya maamuzi mazito ambayo yamefanywa na Uongozi wa Awamu ya Pili na Awamu ya Tatu. Yote hayo siwezi kuyaorodhesha hapa kutokana na muda. Lakini wote ni Mashahidi kwamba barabara nyingi ambazo zimekamilika sasa zimeanza kujengwa tangu enzi za Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Pili na Awamu ya Tatu.

Mheshimiwa Spika,
· Napenda kulifahamisha Bunge lako Tukufu kwamba Serikali ya Awamu ya Nne chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ndiyo pekee imefanya Maamuzi Magumu na Mazito kuliko zote zilizopita.

· Maamuzi Magumu yaliyotolewa na Serikali ya Awamu ya Nne ni mengi. Naomba uniruhusu nitaje mifano ya baadhi ya Maamuzi hayo.

· Ili kuimarisha Utawala Bora tumefanya Uamuzi Mgumu wa kuwafikisha Mahakamani waliokuwa Mawaziri wa Serikali zilizopita kutokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili za kutumia Madara isivyo halali.

· Serikali ya Awamu ya Nne ndiyo iliamua kujenga Shule za Sekondari za Kata ambazo zimewezesha Wanafunzi wengi kupata Elimu ya Sekondari. Leo tumeshuhudia kuwa kati ya Wanafunzi 20 tuliowapongeza kwa kufanya vizuri kwenye Mitihani ya Kidato cha Sita 2011, Saba (7) wanatoka Shule za Kata, sawa na Asilimia 35.

· Tumeweka historia ya kuamua kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma ambacho ni kikubwa mno Nchini. Faida yake tunaiona. Watoto wetu takriban 20,000, wanasoma. Ninaamini kila mmoja kati yetu humu ndani anaye Mtoto, awe Mjukuu, Mjomba, Shangazi, Baba Mdogo, Ndugu, Jamaa na hata Rafiki tu ambaye anasoma katika Chuo hiki. Ndiyo sababu kubwa inayotufanya wote tuone uchungu wa baadhi ya Watu wanaowasumbua hivyo kusababisha Watoto wetu washindwe kukamilisha masomo yao kwa wakati kutokana na Migomo inayojitokeza mara kwa mara.

· Aidha, tunajenga Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo ambacho kimefikia hatua nzuri.

· Serikali ya Awamu ya Nne imekamilisha Miradi yote 27 ya Barabara Kuu zilizoanzishwa na Serikali ya Awamu ya Tatu. Sasa hivi unaweza kutoka Mtwara-Dar es Salaam-Dodoma

hadi Mwanza kwa kupitia kwenye barabara ya lami. Vilevile, tumeamua fedha zote za MCC tuzipeleke kujenga Barabara za Mikoa iliyoko pembezoni. Tumeshuhudia ndani ya Bunge hili Waheshimiwa Wabunge, bila ya kujali itikadi za Vyama wakisifu maendeleo yaliyopatikana kule Kigoma. Tumesikia maendeleo yaliyopatikana kule Kilimanjaro. Tumesikia maendeleo yaliyopatikana kule Rukwa, na tumesikia maendeleo yaliyopatikana kule Mtwara. Tumesikia maendeleo yaliyopatikana maeneo mbalimbali Nchini ambapo Barabara za Lami zinakaribia kukamilika. Tutasimamia hili na Barabara hizo zitakamilika.

· Ujenzi na ukamilishaji wa Miradi ya Maji Nchini.

· Tumefanya maamuzi mazito katika kuwalinda Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi na tumefanikiwa.


  • Aidha, ili kuondoa mpasuko wa Kisiasa Zanzibar, tumefanya maamuzi magumu ya kukubali kuanzisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Tumefanikiwa na Ulimwengu ulitusifia kwa hilo.

· Tumefanya maamuzi ya kupanua na kushamiri kwa Demokrasia Nchini kwa kiwango kikubwa. Nadhani, hii ndilo linasababisha baadhi yetu sasa tunajisahau na kuanza kutumia maamuzi hayo visivyo. Tunahamasisha maandamano huku tukijisifu kwamba huo ndio uzalendo.

· Zaidi ya hayo,tumefanya maamuzi ya kuruhusu Uhuru mkubwa wa Vyombo vya Habari. Mtu anaandika anachotaka, na uhuru wa kusema lolote.

· Hivi karibuni tumefanya uamuzi wa kuruhusu kuanzisha mchakato wa Kupata Katiba Mpya. Hili nalo siyo jambo dogo hata kidogo.

· Lakini pia katika Awamu hii ndipo tumefanya maamuzi mazito sana ya kuvunja Baraza la Mawaziri kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Edward Lowassa, (Mb.). Hili nalo halikuwa jambo jepesi hata kidogo. Inataka Moyo!

Mheshimiwa Spika,
· Orodha ni ndefu kama tunaihitaji kwa maana ya kuorodhesha. Nimeona niyaseme yote haya ili kuthibitisha ukweli kwamba maamuzi yanafanyika tena kwa wakati na kwa manufaa ya Wananchi wetu.

· Aidha, maamuzi haya ni sehemu ya maisha ya Serikali katika kutekeleza majukumu yake kwa dhana ya Uwajibikaji wa pamoja Collective Responsibility kupitia Baraza la Mawaziri. Tunachohitaji ni kuvumiliana. Kuvuta subira, kwani Mambo Mema Hayataki Haraka! Tutaamua na Tutafanya!


Pinda naona kamtolea uvivu...
 
bado wanaendelea ndio wabunge wamesimama kung'ang'ania mshahara wa waziri mkuu na haswa kutaka hoja mbalimbali ziweze kujibiwa kama hazikujibiwa kikamilifu.
.

Hapo kwenye red: wabunge wengi wa ccm walitumia muda wao wakati wa kujadili bajeti ya office ya waziri mkuu kwa kuishambulia CHADEMA na mipasho! Wakati wa hitimisho ndio wanashtuka na kuanza kutoa hoja za wananchi! huku ni kupoteza muda.
 
Nimemsikia Pinda sasa hivi, kumbe hata wabunge wakienda Ulaya wanapewa posho ya mavazi? Nilifikiri posho hii inawahusu vijana wanaokuwa wametoka shule moja kwa moja.
 
Teh teh teh teh

Sasa wabunge si tayari wanazo suti za kutosha wanzovaa mjengoni. Hiyo posho ya mavazi gani Au wakineda ulaya wanatakiwa kuvaa kimasai

Wabubge bana wamecopy haki zote walizonazo wafanyakazi wenye TGS lakini wao hawataki kuwapa wafanyakazi wenye TGS haki kama zao,
 
Back
Top Bottom