Pinda amethibitisha ndani ya bongo wote hatuko sawa mbele ya sheria.

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Kulingana na katiba yetu mamlaka ya juu kabisa ya kuamua iwapo mtuhumiwa wa kosa lajinai afikishwe mahakamani hao la, ni Mkurugenzi wa mashitaka; lakini hivi majuzi wakati Pinda anahitimisha mjadala wa makisio ya ofisi yake alisema JK alifanya maamuzi magumu kwa kuridhia baadhi ya mawaziri wa awamu ya tatu kufikishwa mahakamani. Usemi huo ulinikumbusha sakata la fedha za EPA ambapo JK alisema kama watuhumiwa hao watarejesha fedha walizokwapua katika muda aliowapa hawatashitakiwa. Wakati huo wengi wetu tulijihuliza hayo madaraka JK ameyapata wapi! Kwani kwa mujibu wa katiba rais anayo madaraka ya kumsamehe mtu ambaye tayari amewekwa hatiani lakini siyo kabla. Katika mambo mengi yanayokwenda hovyo nchini mwetu ni pamoja na hii tabia ya watawala ya kujichukulia sheria mikononi mwao. Ifike mahali watanzania wote bila kujali vyama au itikadi zetu, tuseme kwa nguvu na kauli moja ya kuwa IMETOSHA.
 
Back
Top Bottom