Pinda ameshindwa kuizuia rushwa nchini

Kisendi

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
699
178
Tatizo la Rushwa nchini linazidi kuongezeka kila kukicha baada ya Waziri Mkuu kuwasihi mashehe na Maaskofu wahubiri rushwa misikitini na makanisani hii ni kutokana na RUSHWA kukithiri NCHINI mara dufu.

Je Yeye Kama W/Mkuu sheria zipo anafanya nini kuwatimua kazi watu wanaoiba wazi wazi na wanafahamiki
Je yeye ni mtu safi au na yeye anatumiwa
Je yeye yupo tayari kwa kuwasaliti wenzake
Je Hii inamaanisha nini kwa Nchi yetu
Je nani yupo tayari kwa maslahi ya watz masikini
je na hizo kamati za bunge na posho zao za mikutano kila kukicha na hatuoni maendeleo hizo si rushwa tu
Je Wabunge wangapi wapo kimaslahi ya TAIFA kwenye hizo KAMATI
 
Pinda ameishawasaliti wakulima wa nchi hii kwa kujiita mtoto wa mkulima huku anatumikia mafisadi. Nahisi yeye ni mmoja wa wala rushwa wakubwa ndo maana kakimbilia kwa viongozi wa dini ambao hawana jela wala magereza. Mpotezee huyo jamaa miaka yake ipite tu hana anachokifanya.
 
Mpotezee huyo jamaa miaka yake ipite tu hana anachokifanya.[/QUOTE]

Achana na Pinda,yaani alivyopinda ni bora hata angekua mtoto wa mfanyabiashara/mafisadi
 
Moja ya kazi kuu ya kiongozi mahiri ni kusimamia utekelezaji wa sheria za nchi, na kutatua matatizo mbalimbali yanayowakumba wananchi.Kwa bahati mbaya mzee wetu Pinda naye badala ya kuwa mtatuzi na msimamizi wa utekelezaji, yeye naye amekuwa AKILALAMIKA hadharani just like other ordinary citizens.So hii inakuwa ngumu kutushawishi endapo kweli hiyo nafasi ya uwaziri mkuu anaiweza.Arejee utendaji kama wa akina Edward Sokoine, Cleopa Msuya, Rashid Kawawa, ili ajifunze what it takes to be a prime minister.Uadilifu wake tu hautoshi, bali yeye needs to be tough, strong and uncompromising in dealing with corrupt and economic saboteurs who are ruining prosperity of this country.Asipoweza kuyasimamia hayo kwa dhati na bila woga ajue kwamba historia ya nchi hii haitampa legacy nzuri kama ambazo wenzake akina Sokoine, Kawawa wameziacha hapa Tanzania na Africa kwa ujumla.LEADERSHIP IS TO SACRIFICE FOR THE PEOPLE.
 
viongozi wetu wanapenda kusingizia watu wengine mambo.....sasa hata maana ya mtu kuwa kiongozi inapotea....hata JK alisema yeye hawezi kuzuia malipo ya DOWANS.......hamwoni mwenzake Ghadafi anavyofanya huko?......huwezi hutaki?
 
Pinda hapaswi kuwatupia mzigo viongozi wa dini kuhusu ufisadi.kazi ya viongozi wa dini ni kuwajenga raia kimaadili, na ukweli si wote wako radhi kufuata kuwa waadilifu.endapo uadilifu haupo hapo ndio dola huingilia kati kwa kuwashughulikia kwa mujibu sheria zilizopo.sasa endapo serikali haiwezi kuwashughulikia (incompetence or neglegence) mafisadi walio serikalini, sasa anatarajia viongozi wafanye nini? Mheshiwa pinda asikwepe majukumu kwa kuwarushia watu wengine ugonjwa ambao serikali imekuwa ikiukumbatia.tunamtaka yeye kama premier achukue hatua dhidi ya wahusika.ajifunze china ambako corrupt officials are executed bila mjadala.nini kinachoifanya serikali yake kutumia bunge ili kutunga sheria kali zaidi (death penalty) dhidi ya wezi wa nchi hii? Mheshimiwa anapaswa kuelewa kwamba people will judge him by his deeds and not by just giving mere words and inexcusable excuses.
 
Back
Top Bottom