Pinda akataa shangingi Toyota VX 8 ya Tsh 280 milioni!

Pinda ni mnafiki mkubwa. Amekataa ilo VX,afu kakubali Mercedes S-Class 600! Huo si unafiki mkubw!
Bhebhe nyanda, hebu niambie mkuu; Pinda anatumia gari gani vile? Hiyo S-Class 600 mbona bei ni zaidi ya 250M!!!!, tena hiyo nigari ya matanuzi HAWEZI HATA KWENDA NAYO KIJIJINI KWA BI MKUBWA! Ama kweli atawahadaa wengi!!!!
 
Mpuuzi tu huyu, inasaidia nini kukataa gari halafu anasema apewe mwingine? Huyo atakayepewa atakuwa anatumia hela ya nani kama si ya serikali? Kama kweli ana nia ya dhati ya kupunguza matumizi mabaya ya pesa za serikali basi angeagiza kwamba iuzwe na pesa zitumike kwa shughuli nyingine. Na zaidi ya yote, hiyo gari aliyoikataa ni ile iliyonunuliwa kwa ajili ya waziri mkuu, je anasemaje kuhusu gari zilizonunuliwa kwa ajili ya wizara nyingine? Amewaambia mawaziri wengine kwamba na wenyewe wazikatae? Huyu Pinda kwa kweli hakustahili kuwa waziri mkuu. Hana bado sifa za kuwa waziri mkuu. Anashindwaje kutoa tamko na agizo kwa taasisi zote za serikali ili zisiendelee kutumia fedha kiholela? Hana lolote huyu.

nakubaliana na wewe, liuzwe hela ifanyiwe mambo mengine.
 
Siasa!!

Yeye (Pinda) ndiyo mtoa kibali.

Hakujua kama kama na yeye kuna mzigo(VX) wake kwenye hicho kibali alichotoa?

hatudanganyiki.

kama ana ubavu, aamuru badala ya shangingi watumie RAV4.

kazi kukopi sera za watu (chadema) tu.
 
..................Pinda ambaye ndiye anayetoa kibali cha ununuzi wa magari ya serikali alisema hatakubali kuidhinisha viongozi wa serikali kutaka kununua magari ya kifahari wakati wanaweza kutumia magari ya kawaida..............................


I am lost somewhere, does it mean alijotolea kibali gari linanunuliwa ili baadae alikatae? Plse some more elucidations.
 

- Mkuu wangu hii hoja yako ninaikataa kwa nguvu zangu zote, kwa sababu Mbunge wa Mahenge, au Ulanga hawezi kufika jimboni kwake bila gari lenye thamani ya angalau Shilingi Millioni 300, halafu wengu hapa mnaonekana kutojua matumizi ya magari ya wabunge, people hua yanatumika sana na wananchi jimboni licha ya mbunge mwenyewe, wananchi wa jimbo huyachukulia haya magari kama ni yao, ninasema niliyoyaona kwa macho yangu,

- I mean msiba wowote unapotokea kwenye jimbo ni gari la Mbunge ndilo linategemewa kutumika kusaidia kusaifirisha mwili, hizi ndio realities za siasa za bongo people, inaonekana wengi hapa tunajua kushambulia tu bila kujua kinachoendelea ground zero, mimi nilikuwa vijijini this June, kuna sehemu bila gari la Mbunge kila kitu kinasimama jamani! Pole pole na hizi hoja!


William.

...William, i doubt kama unayajua yanayotokea majimboni na realities za ukaribu wa wabunge kwa wananchi.

...Unataka kusema gari ya Ndugu Masha ilikuwa ikitumika kubeba miili kule Nyamagana?

...Ukiwa unatetea jambo uwe na data zitakazo support hoja yako. Unadiriki kusema kwamba gari la mbunge inabidi liwe na thamani ya M300? ina maana lenye thamani ya M50 halitaweza kutembea au barabara zetu zinapitisha magari kutokana na thamani pamoja na hadhi ya mmliki?

...Sasa, wewe ndio haujui matumizi ya gari la mbunge! Gari la mbunge si la kubebea wagonjwa na maiti hospitali....yapo au yanahitajika magari kwa kazi hiyo.

...Kwa akili za kawaida tu, hiyo M300 ingetoa magari mangapi yenye thamani ya M50 yakahudumia hao ambayo kama hamna gari ya mbunge jimboni mwao shughuli zinasimama?

...Tafakari, utapata jibu!
 
- Mkuu hamna jipya hapa, unasema wanakopeshwa! halafu hela za kuyalipia zinalipwa nani? Hebu piga hesabu ya hela za mbunge in five years akiwa bungeni hivi kweli anaweza kuyalipia haya magari akamaliza in five years?

- Pole sana mkuu!
William.

MKuu heshima kwako, lakini umepindisha ukweli. Alichokisema Mwanalugali ndo ukweli. Wabunge WANAKOPESHWA magari na wao wana uhuru siku hizi ya kuchagua aina ya gari wanayotaka kununua kwa mkopo huu. Mkopo huu ni nafuu kuliko ule wa benki lakini HAWAPEWI bali wanakatwa kutoka mishahara yao. Mikopo hii ya magari ni makubaliano maalum ambayo serikali iliingia awali na DT Dobie na baadae makampuni mengine. Kwa utaratibu wa sasa hivi hata second-hand yaani gari la mitumba wanaruhusiwa kununua waheshimiwa. Kwa wale ambao hawategemei sana mishahara yao ya ubunge wana uwezo hata wakulipa kwa mkupuo moja ingawa kwa taarifa nilizokuwa nazo wengi hupendelea kuendleea kukatwa kila mwezi. Kwa hiyo tuiweke hii sawa na tusipotoshe umma.
Kwa upande wa Waziri mkuu na magari yale yanayobadilishwa kila baada ya miaka miwili ni magari ya SERIKALI. Na si kuwa magari yote ya wabunge, bali magari yote ya mawaziri ndo hubadilishwa kila baada ya miaka 2 au 3. Na hata waziri wa wizara husika ana uwezo wa kuzuia kuwa katika bajeti ya wizara yake wasiweke ununuzi wa gari jipya. Kwa hiyo kusema eti Pinda alikuwa powerless si kweli kwani ana uwezo wa kupitia bajeti na kutoa vipengele anavyoona havistahili. Zaidi ya hayo Pinda hawezi kusingizia kuwa aliyemtangulia ndiye aliyeacha matumizi haya kwani alikuwa Waziri mkuu mwaka jana pia.
This simply doesn't fly!
 
PM amejikosha tu, kwanza utendaji wake umekaa kiwoga woga, siyo mkali, akiwa kama kilanja mkuu haya angeyafanya mapema angekuwa mkali toka mwanzo hawa watendaji wasingenunua hilo VX..:bump:
 
- Nimesema mara nyingi sana kwamba Great Thinkers tunatakiwa kujadili taifa kwa kutumia katiba, miongozo na facts, Waziri Mkuu hawezi kutoa amri ya kuzuia kununuliwa kwa magari yanayonunuliwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri, ambayo ilipitishwa na bunge la pamoja kati ya CCM na Wapinzani, na kuwekewa bajeti yake tayari!

- Mengine ni common sense japo kidogo sana na wala sio politics as usual!

William.

Mr Malecela kwa hili nadhani wewe ndo umeenda nje ya mstari.
Hebu tuambie kipengere cha Katiba kinachozungumzia ununuzi wa magari ili tupate kuelimika kidogo. Kwa ufahamu wangu hizi ni taratibu na kanuni tu za serikali hazihitaji mabadiliko ya katiba (kununua/kutokununua) na kwa msingi huio Wizara ya Ujenzi/Miundombinu ndo inahusika na magari yote ya serikali. Mizengo Pinda hawezi kujivua lawama kwa kukataa gari, angeenda mbali zaidi ama kuamuru liuzwe hata kama ingekuwa at a -20% price au kuwajibisha watendaji.
Ugomvi wetu na haya magari ni gharama za uendeshaji wake. Pinda ndiye msimamizi mkuu wa serikali sasa kama alitamka yasinunuliwe na gari linanunuliwa hizo ndio hatua muafaka za kuchukua kama PM au hajui madarake yake??
Viongozi wetu wanafiki angalia mawaziri waliopigwa chini kama utakuta wanaendesha hayo ma V8 kama wapo ni wale waliovuna mapema (likes of karamagi etc), wengine wengi wanakamua ndani magari ya kawaida saaaaaaana.

Tukilitazama kisiasa hapa mtoto wa mkulima ameonyesha hapendi makuu INGAWA hilo pekee halitoshi.
 
Huyu jamaa nimeshamsoma, yukokwenye daraja tofauti kabisa, haamini na hakubali kuwa waziri anaweza kutumia hardtop ya 60M! na wala haoni umuhimu na mamlaka ya waziri mkuu katika kuangalia vipaumbele vya matumizi ya fedha ya wavuja jasho, huyujamaa simtofautishi na Pinda, Makamba au Rizwani! By the way...si ndy walewale......! MTACHOMOKA TU, MMOJA MMOJA!:redfaces:
 
Naomba tupitie habari hii taratibu

Gharama yake Sh280milioni, asema nchi yetu ni masikini
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameonyesha kwa vitendo kuwa yeye ni mtoto wa mkulima baada ya kukataa gari jipya ka kifahari alilonunuliwa na wasaidizi wake kwa akisema kwamba alilonalo linamtosha.


Hapa tumeona mil 280 kwa ajili ya gari tu!


"Ni kweli nimelikataa kulitumia gari hilo kwani niliona hata gari hili ambalo nimeanza nalo kulitumia kama mawaziri mkuu bado halikuwa na matatizo, sasa kwa nini nipewe jingine jipya, hii itakuwa ni matumizi mabaya fedha za serikali," alisema.

Hapa tunaona nia ya kukataa matumizi makubwa! Je vitendo lini?



Pinda ambaye ndiye anayetoa kibali cha ununuzi wa magari ya serikali alisema hatakubali kuidhinisha viongozi wa serikali kutaka kununua magari ya kifahari wakati wanaweza kutumia magari ya kawaida.

Hapa inaonyesha anatoa vibali bila kujua ni vya nini? Au hili hakulipa kibali?

Hata hivyo,alisema kuwa hawezi kupiga marufuku moja moja ununuzi wa magari ya kifahari kwa vile ni jambo ambalo linahitaji kuchukuliwa kwa hatua, lakini taratibu watedaji wa serikali watahamia katika kutumia magari ya kawaida.

Kwanini usipige marufuku wakati nchi ni maskini? Mbona Rwanda yalipigwa stop na kuuzwa kwa yale yaliyokuwa yanatumika! Hii inaonyesha hakuna nia ya DHATI.


Ripoti ya Mpango wa Serikali kuhusu Orodha ya Magari yake na Kudhibiti Matumizi ambayo ilipendekeza pamoja na mambo mengine magari ya kifahari ya mawaziri maarufu kama mashangingi yanunuliwe kila baada ya miaka saba badala ya miwili ya wakati huo.

Hapa nawapa pongezi, kwasababu hata baada ya miaka 7 magari haya yanakuwa bado ni mazuri. Angalia watanzania tunaonunua Used Cars nyingi zinakuwa na miaka 10!

Utaratibu uliozoeleka ni kwamba, gari la waziri huweza kununuliwa kila baada ya miaka miwili tangu linunuliwe na kuanza kutumika, kisha hutumiwa na watendaji wa ngazi ya chini, au kuuzwa au waziri 'kujiuzia'.


Huu ulikuwa ufujaji wa hela za umma. Ndio maana sisi ni masikini!


Pendekezo la serikali ni kwamba katika ngazi ya Serikali za Mitaa, linataka Mkuu wa Mkoa pekee ndiye atumie Vx ili kuwezesha Rais anapofika aweze kulitumia huku Wakuu wa Wilaya na watendaji wengine wakitakiwa kupatiwa gari za kawaida kama Toyota Landcruiser si Vx.

Hata mkuu wa mkoa hapaswi kutumia gari la thamani ya mil 280. Hii ni hela ya walalahoi wasio na vituo vya afya!


MWISHO
Mimi naamin hapa Tanzania hakuna kiongozi anastahili kutumia gari la kifahari ambalo linanunuliwa na Serikali. Serikali maskini lazima iendeshwa kimaskini. Kwani viongozi wakinunuliwa Say VITARA/COROLLA/RAV 4 kuna tatizo gani?. Nashauri serikali iachane na magari ya kifahari na matumizi mengine yote ya kifahari mara moja. Watanzania tuamke katika hili, nchi ni maskini kwasababu tunafumbia macho matumizi ya kifahari kwa viongozi wetu. Nilisikia ripoti ya CAG kuhusu nyumba za gavana na wasaidizi wake za zaid bil 1.2 kila moja eti kuna VALUE FOR MONEY! Great thinkers jiulize, je Gavana kwanini ajengewe nyumba ya Bilion? Hivi yeye hawezi kuishi kwenye nyumba ya kawaida? hapa ndipo chimbuko la umaskini wetu kama taifa. TAFAKARI

 
Siasa!!

Yeye (Pinda) ndiyo mtoa kibali.

Hakujua kama kama na yeye kuna mzigo(VX) wake kwenye hicho kibali alichotoa?

hatudanganyiki.

kama ana ubavu, aamuru badala ya shangingi watumie RAV4.

kazi kukopi sera za watu (chadema) tu.
CCM baada ya uchaguzi pamoja na kuchakachua kura.Wameanza kuzisoma na kuzipitia sera za CHADEMA ambapo awali walikua wanadai hazitekelezeki.Kama Mtoto wa mkulima ni mkweli basi magari hayo ya fahari yapigwe bei na pesa zake ziende kusaidia sekta nyingine kama elimu na afya n.k.Vinginevyo ilo NI CHANGA LA MACHO MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
[Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana jioni kwa njia ya simu, Pinda alisema kuwa uamuzi huo aliuchukua mwaka huu kabla ya uchaguzi mkuu kuanza baada ya kukataa kulitumia gari jipya aina ya Landcruiser VX 8 lenye thmamani ya sh milioni 280.]

Hivi jamani mbona tunapotosha mada NI MBUNGE GANI ANANUNULIWA GARI KABLA YA UCHAGUZI KUFANYIKA..?
 
MKuu heshima kwako, lakini umepindisha ukweli. Alichokisema Mwanalugali ndo ukweli. Wabunge WANAKOPESHWA magari na wao wana uhuru siku hizi ya kuchagua aina ya gari wanayotaka kununua kwa mkopo huu. Mkopo huu ni nafuu kuliko ule wa benki lakini HAWAPEWI bali wanakatwa kutoka mishahara yao. Mikopo hii ya magari ni makubaliano maalum ambayo serikali iliingia awali na DT Dobie na baadae makampuni mengine. Kwa utaratibu wa sasa hivi hata second-hand yaani gari la mitumba wanaruhusiwa kununua waheshimiwa. Kwa wale ambao hawategemei sana mishahara yao ya ubunge wana uwezo hata wakulipa kwa mkupuo moja ingawa kwa taarifa nilizokuwa nazo wengi hupendelea kuendleea kukatwa kila mwezi. Kwa hiyo tuiweke hii sawa na tusipotoshe umma.
Kwa upande wa Waziri mkuu na magari yale yanayobadilishwa kila baada ya miaka miwili ni magari ya SERIKALI. Na si kuwa magari yote ya wabunge, bali magari yote ya mawaziri ndo hubadilishwa kila baada ya miaka 2 au 3. Na hata waziri wa wizara husika ana uwezo wa kuzuia kuwa katika bajeti ya wizara yake wasiweke ununuzi wa gari jipya. Kwa hiyo kusema eti Pinda alikuwa powerless si kweli kwani ana uwezo wa kupitia bajeti na kutoa vipengele anavyoona havistahili. Zaidi ya hayo Pinda hawezi kusingizia kuwa aliyemtangulia ndiye aliyeacha matumizi haya kwani alikuwa Waziri mkuu mwaka jana pia.
This simply doesn't fly!

...Susuviri, point si kwamba Ndugu Pinda ni powerless au la. Kwa kuangalia siasa za Tanganyika zilivyo na hasa katika utawala wa JMK, Pinda hapendi kujiiingiza kwenye ugomvi na watu. Kwanini? Inavyoonekana, wapo wengi wanaopenda kutanua katika hayo magari. Pia, wapo wanaofaidika na uagizaji wa magari hayo. Na, wapo wasiojali matumizi ya fedha zinazotokana na kodi wanayotozwa waTanganyika yanapewa vipaumbele gani na kwa kiasi gani.

...Utashangaa, kuna wananchi, tena choka mbaya, wanaosema kwamba viongozi wetu wanastahili magari hayo ya kifahari. Hawa ni wale wanaopeleka wagonjwa wao waliozidiwa kwa baiskeli au miguu hospitali ambazo ziko kilometa kadhaa toka wanapoishi.
 
Jamani tusimlaumu Pinda. Pengine yeye kawekwa kama kimvuli tu kuwa waziri mkuu, maamuzi yote yanaamuliwa na waliomuweka madarakani. Nahisi hakujua kuwa magari yameagizwa yeye kashtukia tu hilo hapo ndo maana kakataa. Namuhurumia sana Pinda kajiingiza kwenye umafia kutoka hawezi.
 
Mi naona hakuna alichokifanya kuokoa hizo fedha for tanzanian, kama alimaanisha watatnzania ni maskini, he could odrered to sell the car and use the money for developments sasa kupewa mtu mwingine wakati mawaziri wote washanunuliwa magari may be ni uzushi. na hoji pia mie tu nisie mwanasiasa najua kila term mpya mawaziri, wabunge wanaletewa magari mapya, if he were seroius angezuia mapema hilo gari lisinunuliwe, na hizo fedha angeziagiza ziende sehemu nyingine. mi nafikiri asituletee unafiki, na kwa cheo alichonacho angeweza kuzuia pia hata hao mawaziri wengine wasinunuliwe hayo magari, ziko vx8 za bei chini ya 100 mazuri kabisa. nasisitiza aache unafiki befor people, hizo fedha hazijatusaidia zaidi ya kutumiwa na mtu mwingine ambaye tayari ameshapata gari.
 

- Gari alilolikataa ni gari la ubunge ambalo kila Mbunge anatakiwa kupewa anapoanza ubunge, hizo hela za hayo magari zimo kwenye bajeti tayari kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri, sasa Mbunge anaweza kukataa gari lakini hawezi kusimamisha katiba eti kwa sababu yeye ni Waziri Mkuu na kuzuia wabunge wengine wasipewe magari.

- Understand kwamba Waziri Mkuu amepewa hili gari kama Mbunge na sio Waziri Mkuu, yaani hata haya madogo sana nayo yanahitaji malumbano, vipi wakuu katiba yetu inatupita pembeni nini? Huu uamuzi wa Wabunge kupeana magari mapya kila baada ya miaka mitano ulianza zilipoanza siasa za vyama vingi, wakuu tulikuwa wapi?

- Hii inasikitisha sana, kwamba hatuelewi vitu vidogo sana vya katiba ya Jamhuri yetu no wonder tunabambikwa mambo ya Dowans, ni kwa sababu simply kwamba hatujui kinachoendelea na taifa letu, kelele tu za madebe matupu!



William
Hapo ndo unadhiirisha Umbumbumbu wako na hiyo Katiba unayoiongelea hapo labda kama ni ya Familia yako,Ongea vitu unavyovielewa na unauhakika navyo sio kupotosha watu.
Kwanza hilo la kwamba Gari anapewa kama Mbunge we umelitoa wapi?
Nani aliyekuambia Mbunge anapewa gari?Ninavyoelewa mie Mbunge anakopeshwa Ela kwaajili yakununua gari na anakuwa anakatwa kwenye Mshahara wake.
Waziri kama Mtendaji wa Serikali ndo ananunuliwa Gari kutokana na Kodi zetu.Jipange Mzee usituletee Bla bla hapa jamvini.Huyu PM na Presidaa ni kwamba vipofu wanaongozana na lazima tu Watutumbukize shimoni kwa haya Madudu wanayoyafanya M1 hajui kwanin Tz ni Maskini mwingine na usaníi wakukataa gari wakati kaidhinisha linunuliwe Et Mtoto wa Mkulima!!Iv Milembe imejaa?
 
Putting everything aside, Lets give Credit where credits due... For this action nampongeza huyu Jamaa tena asiishie hapo awaambie na mshahara wampunguzie pia.... He is leading by example.... maybe atawashinikiza na wengine wamfate
 
Katika hili Pinda anachezea akili ya watanzania; kwa wadhifa wake anashiriki kwenye vikao vyote vya juu vya maamuzi hapa nchini, kwa mantiki hiyo yeye siyo mtu wa kunungunika, kwani anayo fursa ya kuleta suala lolote linalogusa hisia zake katika vikao husika, na akishafanya hivyo na akalijengea hoja na kutokana na uamuzi wa wengi likakataliwa anabakia na njia mbili zakufanya; njia ya kwanza ni kufuta msimamo wake wa hapo awali na kuunga suala hilo mkono; vinginevyo anawajibika kuachia ngazi, ikiwa dhamira yake haimruhusu kuunga mkono huo uamuzi wa walio wengi. Kufanya vinginevyo kwa maoni yangu kunaashiria utovu wa nidhamu na kunamuweka katika hali ambapo mkuu wake wa kazi anaweza kumchukulia hatua za kinidhamu.
 

- Mkuu wangu hii hoja yako ninaikataa kwa nguvu zangu zote, kwa sababu Mbunge wa Mahenge, au Ulanga hawezi kufika jimboni kwake bila gari lenye thamani ya angalau Shilingi Millioni 300, halafu wengu hapa mnaonekana kutojua matumizi ya magari ya wabunge, people hua yanatumika sana na wananchi jimboni licha ya mbunge mwenyewe, wananchi wa jimbo huyachukulia haya magari kama ni yao, ninasema niliyoyaona kwa macho yangu,

- I mean msiba wowote unapotokea kwenye jimbo ni gari la Mbunge ndilo linategemewa kutumika kusaidia kusaifirisha mwili, hizi ndio realities za siasa za bongo people, inaonekana wengi hapa tunajua kushambulia tu bila kujua kinachoendelea ground zero, mimi nilikuwa vijijini this June, kuna sehemu bila gari la Mbunge kila kitu kinasimama jamani! Pole pole na hizi hoja!


William.

Kwa kweli mtoto wa nyoka ni nyoka. Yaani William unatuambia mbunge wa mahenge hawazi kufika kwake bila ya gari la milioni 300? Hivi mbona nyie watu mliokulia kwenye neema mna matatizo sana? Ni mahali gani hapa tanzania ambako Toyota Hardtop (mkonga) haifiki? Tena mkonga inaweza kuwa ya uhakika zaidi kuliko hata hilo shangingi! kwa uwezo wetu mdogo wa serikali, hakuna sababu yoyote ya msingi ya mtu kutumia gari la milioni 300 wakati kuna VX za milioni 120 ambazo na zenyewe zinaweza kufanya kazi sawasawa na hiyo Vx 8. Jamani, hebu wakati mwingine tuwahurumie na wale watu wa vijijini wanaoishi kwa mlo mmoja.
 
Hapo hakuna alichookoa! Kama gari limeshanunuliwa, na fedha ya walipa kodi imeshatumika! Huko ni kujisafisha tu! Halafu inakuaji fedha nyingi kiasi hicho inatumika bila yeye kushirikishwa? Shilingi 280 ni fedha inayotosha kufadhili nusu ya mpango wa maendeleo ya kilimo ya Wilaya moja (DADPS) kwa mwaka moja wa fedha!!! Hivi..... Huyo ni mtoto wa mkulima kweli?!!!!.... Hicho ni kichefuchefu kingine!!!!... Hamna kitu hapo!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom