Pinda akataa shangingi Toyota VX 8 ya Tsh 280 milioni!

O.k. tueleweshane taratibu mkuu. So ngoja nione kama nime kusoma. Umesema hilo gari kanunuliwa kama mbunge na si waziri mkuu sawa? Na ana haki ya kulikataa au kuli kubali right? Sasa kama mbunge ina julikana ana weza kataa gari au laa kwa nini linunuliwe kabla mbunge hajaulizwa kama ana taka gari au la? Na yeye si mara ya kwanza kuwa mbunge kwa hiyo anajua huo utaratibu kwa hiyo kwa nini hakukataa tokea mwanzo na wakati anajua kama mbunge lazima ange nunuliwa gari jipya na angelikataa? Does it make sense?Hatumsemi waziri mkuu tu tunaongelea utaratibu mzima elewa hilo. Na hata kama kitu kipo kwenye katiba kama kina dosari tusiseme? Mbunge ana apishwa within a few days ya kushinda uchaguzi. Waziri mkuu ana pitishwa na kuapishwa within a few days after elections. Hayo magari yana nunuliwa pending na kupewa mtu yoyote atakae shinda au wana subiria mtu ashinde ubunge ndiyo wamuagizie? Kama yana nunuliwa pending basi hapo kuna dosari kwa sababu mbunge ana haki ya kulikataa. Sasa wata nunuaje gari kabla ya kujua mbunge ata likubali au la?Siyo kwamba ina sikitisha. The problem is kuna watu wana fikiria katiba ipo perfect na watu hawawezi kuhoji vipengele. Hata kama katiba ina ruhusu kitu kama haileti mantiki tuna hoji hiyo haimaanishi hatujui katiba. Hapa hamna anaesema Pinda kavunja katiba, at least I am not saying that.

- Mkuu to me hii habari kwangu ni sawa sawa ile habari ya Udini, haina substance yoyote kwa taifa Waziri Mkuu ana magari mengi sana at his disposal kwamba hahitaji gari lingine zaidi, otherwise on this ishu ninaamini kwamba katiba is perfect kwa sababu bila haya magari kuna wabunge wengine hawataweza kufika kwenye majimbo yao, na mfano mzuri sana ni majimbo kama ya Mahenge, na Ulanga.

William.
 
Hacha kupotosha --- hakuna sehemu ambayo habari hii inasema gari alilokataa PM ni sehemu ya gari wanazopewa wabunge, Gari hili lilinunuliwa na WASAIDIZI WAKE kwa MATUMIZI YAKE KAMA PM. Zaidi ya hilo, hebu tafakali hizi sentensi hapa chini:

Baada ya kutafakali hizi "Quotes" jiulize:

1. nani aliidhinisha kununuliwa kwa hilo gari?

2. alikuwa wapi wakati bunge inapitisha bajeti kununua hayo magari licha ya uwepo wa ripoti ya $erikali?!

Hacha uZitto!

- Waziri Mkuu amekataa Shangingi la ubunge, hawezi hata siku moja akakataa magari ya Waziri Mkuu as Waziri Mkuu, sihitaji kusoma popote kujua haya, Waziri Mkuu hanunuliwi magari ya Waziri Mkuu na wasaidizi, maana hawahusiki kabisa na hilo zoezi la kununua magari ya Waziri Mkuu,

- Lakini for sure wasaidizi wanahusika na kumchagulia gari la ubunge wake, pole sana mkuuu!

William.
 
- Mkuu to me hii habari kwangu ni sawa sawa ile habari ya Udini, haina substance yoyote kwa taifa Waziri Mkuu ana magari mengi sana at his disposal kwamba hahitaji gari lingine zaidi, otherwise on this ishu ninaamini kwamba katiba is perfect kwa sababu bila haya magari kuna wabunge wengine hawataweza kufika kwenye majimbo yao, na mfano mzuri sana ni majimbo kama ya Mahenge, na Ulanga.

William.

Una kosea unapo jaribu kucompare swala hili na udini. Anyway umesema kapewa gari kama mbunge now una sema ni waziri mkuu hali hitaji hilo gari kwa nini kanunuliwa? Hauja jibu basic question ya kama hilo gari lime nunuliwa kabla au baada ya yeye kuwa mbunge.
Kuhusu wabunge kuwa na magari wapi nimesema wabunge wasiwe na magari? Nilicho hoji mimi ni kwamba kama mbunge ana haki ya kukubali au kukataa gari siyo common sense kusubiri huyo mbunge akubali kupewa gari ndiyo anunuliwe?
 
- Mkuu vipi mbona unaonekana hujielewi, huwezi kununuliwa gari bila ya uchaguzi kuisha kwanza na ikathibitika kikatiba kwamba ni mbunge, halafu limenunuliwa lini na wapi sio ishu hapa, the ishu nini political impact ya kitendo cha Waziri Mkuu kukataa gari la ubunge,

- Ninasema hakuna imapct yoyote wala substance na it is simply a none political ishu kwa sababu a sitting Waziri Mkuu ana magari ya kutosha kwamba hahitaji another gari ndio maana sishangai kuona hapa Waziri Mkuu amekataa gari la ubunge!

William.
 
...sihitaji kusoma popote kujua haya, Waziri Mkuu hanunuliwi magari ya Waziri Mkuu na wasaidizi, maana hawahusiki kabisa na hilo zoezi la kununua magari ya Waziri Mkuu
Ustaadh said:
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameonyesha kwa vitendo kuwa yeye ni mtoto wa mkulima baada ya kukataa gari jipya ka kifahari alilonunuliwa na wasaidizi wake kwa akisema kwamba alilonalo linamtosha.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana jioni kwa njia ya simu, Pinda alisema kuwa uamuzi huo aliuchukua mwaka huu kabla ya uchaguzi mkuu kuanza baada ya kukataa kulitumia gari jipya aina ya Landcruiser VX 8 lenye thmamani ya sh milioni 280.
Nitaendelea kusisitiza kuwa unataka KUPOTOSHA. Hili gari limenunuliwa kabla ya uchaguzi ikiwa ni miaka miwili baada ya yeye kuanza kutumia gari alilopewa 2008 (baada ya kuwa PM).

Ni wazi kwamba ofisi yake ilihusika kupitisha maamuzi ya ununuzi wa GARI hilo; suala la kusema hawahusiki kabisa ni kutaka kupotosha ukweli ukidhani kila mtu ataamini spinning yako -- possibly based on your name with relation to fomer PM (pale unaposema "sihitaji kusoma popote kujua haya").
 
- Gari alilolikataa ni gari la ubunge ambalo kila Mbunge anatakiwa kupewa anapoanza ubunge, hizo hela za hayo magari zimo kwenye bajeti tayari kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri, sasa Mbunge anaweza kukataa gari lakini hawezi kusimamisha katiba eti kwa sababu yeye ni Waziri Mkuu na kuzuia wabunge wengine wasipewe magari.

- Understand kwamba Waziri Mkuu amepewa hili gari kama Mbunge na sio Waziri Mkuu, yaani hata haya madogo sana nayo yanahitaji malumbano, vipi wakuu katiba yetu inatupita pembeni nini? Huu uamuzi wa Wabunge kupeana magari mapya kila baada ya miaka mitano ulianza zilipoanza siasa za vyama vingi, wakuu tulikuwa wapi?

- Hii inasikitisha sana, kwamba hatuelewi vitu vidogo sana vya katiba ya Jamhuri yetu no wonder tunabambikwa mambo ya Dowans, ni kwa sababu simply kwamba hatujui kinachoendelea na taifa letu, kelele tu za madebe matupu!

William

Wabunge wanapewa magari?? give me a break.
Hakuna mpango wowote mahala popote ktk kanuni , mwongozo au katiba kama unavyosema panaposema kuwa wabunge wanapewa magari! Utaratibu ulioko ni kwamba wabunge wanakopeshwa magari tena ni wenyewe wanaochagua wanayoyataka. Hivi sasa mchakato unaendelea kwa makampuni yanayouza magari ( CMC, Diamond,Toyota) kupeleka magari Dododma kwenye maonyesho wakati wakikao cha january ili Wabunge wajichagulie magari.
Inasikitisha kwa Bw. malecele kujenga hoja kwa misingi ya uongo na kupotosha ukweli. Ni vyema kukubali kuwa kuna mushkeli ktk ununuzi na kukataa kwa gari hilo vinginevyo Pinda awawajibishe wote waliolinunua. Kama anataka kumuiga Kibaki, basi awafukuze kazi waliolinunua halafu liuzwe na pesa zipelekwe kwenye mapungufu!
 
Waziri mkuu kaanza kuonesha udhaifu mkubwa sana.Kukataa gari moja kati ya magari maelfu sio kitu.Angeanzisha operations mathubuti kwa vitengo vyote hadi kwa wabunge.Aache woga,pia Watanzania wanataka katiba mpya na tume huru ya uchaguzi,hilo pia asimamie kwa dhati ktk kipindi chake
 
Aliyemkabidhi Pinda ofisi,pamoja na mabaya yote aliyonayo lakini alikuwa na uwezo mkubwa wa kusimamia jambo analoamini likatekelezeka.Pinda ni dhaifu.Hatendi kama waziri mkuu,anaongozwa ama na uoga au unafiki.Kama waziri wa elimu anaweza kubadilisha sera ya elimu(rejea maghembe hivi karibuni),kwa nini MP anashndwa kuwa msiamiaji wa kitu tangu mwanzo mpaka mwisho?Ni udhaifu na nahakika amewekwa pale kwa sababu hiyo,wamburuze.
 
Wabunge wanapewa magari?? give me a break.
Hakuna mpango wowote mahala popote ktk kanuni , mwongozo au katiba kama unavyosema panaposema kuwa wabunge wanapewa magari! Utaratibu ulioko ni kwamba wabunge wanakopeshwa magari tena ni wenyewe wanaochagua wanayoyataka. Hivi sasa mchakato unaendelea kwa makampuni yanayouza magari ( CMC, Diamond,Toyota) kupeleka magari Dododma kwenye maonyesho wakati wakikao cha january ili Wabunge wajichagulie magari.
Inasikitisha kwa Bw. malecele kujenga hoja kwa misingi ya uongo na kupotosha ukweli. Ni vyema kukubali kuwa kuna mushkeli ktk ununuzi na kukataa kwa gari hilo vinginevyo Pinda awawajibishe wote waliolinunua. Kama anataka kumuiga Kibaki, basi awafukuze kazi waliolinunua halafu liuzwe na pesa zipelekwe kwenye mapungufu!

- Mkuu hamna jipya hapa, unasema wanakopeshwa! halafu hela za kuyalipia zinalipwa nani? Hebu piga hesabu ya hela za mbunge in five years akiwa bungeni hivi kweli anaweza kuyalipia haya magari akamaliza in five years?

- Pole sana mkuu!

William.
 
Nitaendelea kusisitiza kuwa unataka KUPOTOSHA. Hili gari limenunuliwa kabla ya uchaguzi ikiwa ni miaka miwili baada ya yeye kuanza kutumia gari alilopewa 2008 (baada ya kuwa PM).

Ni wazi kwamba ofisi yake ilihusika kupitisha maamuzi ya ununuzi wa GARI hilo; suala la kusema hawahusiki kabisa ni kutaka kupotosha ukweli ukidhani kila mtu ataamini spinning yako -- possibly based on your name with relation to fomer PM (pale unaposema "sihitaji kusoma popote kujua haya").

- Habari hii imeandikwa na mwandishi aliyekwua anajaribu sana kuipamba hii habari ionekane ina mvuto, ukweli ni kwamba Waziri Mkuu hanunuliwi gari la u-Waziri Mkuu na wasaidizi na wala hana choice ya gari as Waziri Mkuu, isipokuwa ana choice ya gari la ubunge tu, sina sababu ya malumbano na non ishu kama hii, naomba ksuema tena ni kwamba Wasaidizi wa Waziri Mkuu hawamchagulii gari Waziri Mkuuas waziri Mkuu, never!, ukielewa hilo na kulikubali then utaelewa kwamba hiii habari imechakachuliwa ili i-fit a political profile flani hivi, otheriwse ni non-ishu!

William.
 
- Nimesema mara nyingi sana kwamba Great Thinkers tunatakiwa kujadili taifa kwa kutumia katiba, miongozo na facts, Waziri Mkuu hawezi kutoa amri ya kuzuia kununuliwa kwa magari yanayonunuliwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri, ambayo ilipitishwa na bunge la pamoja kati ya CCM na Wapinzani, na kuwekewa bajeti yake tayari!

- Mengine ni common sense japo kidogo sana na wala sio politics as usual!

William.
Kwahiyo mkuu kwa kukataa gari alilonunuliwa kwa mujibu wa Katiba, amekiuka katiba??? Nahisi hujui unachokisema
 
Huyu Pinda alitoa tamko kabla ya hata gari hili kununuliwa. Alichotakiwa kufanya ni kuchukua hatua. Hivi akipewa mtendaji mwingine inamaana ndio ameepusha gharama? Kuna haja ya kuwachukulia hatua watumishi wa hivyo hii ya kutafuta umaarufu magazetini haitoshi.

Ukweli ni kwamba Pinda hana uthubutu wa kusimamia maamuzi magumu na ndio maana hata hayo magari Landcruser V8 yaliingizwa nchini; yeye aliisha toa amri kuwa magari ya kifahari yasiagizwe na serikali lakini wajanja wakaendelea kutoa order TOYOTA na mgao wao wakapata inspite of the PM,s directive. Pinda aache kulialia na kutaka umaarufu kupitia magazetini anatakiwa kuchukua hatua!!
 
William mbona great thinkers wamekimbia humu siku nyingi? Pita angali threads zinavyojibiwa utachefuka! Tumevamiwa tena shukuru sasa hivi wameenda kula sikukuu wakirudi utajuta Mangi!
 
Aliyemkabidhi Pinda ofisi,pamoja na mabaya yote aliyonayo lakini alikuwa na uwezo mkubwa wa kusimamia jambo analoamini likatekelezeka.Pinda ni dhaifu.Hatendi kama waziri mkuu,anaongozwa ama na uoga au unafiki.Kama waziri wa elimu anaweza kubadilisha sera ya elimu(rejea maghembe hivi karibuni),kwa nini MP anashndwa kuwa msiamiaji wa kitu tangu mwanzo mpaka mwisho?Ni udhaifu na nahakika amewekwa pale kwa sababu hiyo,wamburuze.
 
Pinda ni mnafiki mkubwa. Amekataa ilo VX,afu kakubali Mercedes S-Class 600! Huo si unafiki mkubw!
 
Mpuuzi tu huyu, inasaidia nini kukataa gari halafu anasema apewe mwingine? Huyo atakayepewa atakuwa anatumia hela ya nani kama si ya serikali? Kama kweli ana nia ya dhati ya kupunguza matumizi mabaya ya pesa za serikali basi angeagiza kwamba iuzwe na pesa zitumike kwa shughuli nyingine. Na zaidi ya yote, hiyo gari aliyoikataa ni ile iliyonunuliwa kwa ajili ya waziri mkuu, je anasemaje kuhusu gari zilizonunuliwa kwa ajili ya wizara nyingine? Amewaambia mawaziri wengine kwamba na wenyewe wazikatae? Huyu Pinda kwa kweli hakustahili kuwa waziri mkuu. Hana bado sifa za kuwa waziri mkuu. Anashindwaje kutoa tamko na agizo kwa taasisi zote za serikali ili zisiendelee kutumia fedha kiholela? Hana lolote huyu.

...Si mpuuzi. Yeye ana imani na dhamira ya kutofuja fedha za serikali, lakini, amezungukwa na watu wenye imani na dhamira tofauti. Kama bosi wake anabadilisha kila mara, yeye atafanya lipi zaidi ya kukataa kama mtu binafsi?

...Kimsingi, Pinda anatuonyesha kuwa yeye yu tofauti lakini hana nguvu ya kufanya mabadiliko, zaidi ya kuwa mfano kwa wengine.
 
tamko ameshatoa hebu soma vizuri na kwaumakini maeleze hapojuu pinda ameshatoa maagizo yakubana matumizi nakupunguza kwakiasi kikubwa matumizi yakifahari ya pesa zawalalahoi,hongera mkuu pinda kwakuonesha mfano,ila unatakiwa uwemkali kidogo ili agizolako la kubana matumizi lifanyiwe kazi kwavitendo,hakika ukilisimamia hilo kwa umakini nina iman utafanikiwa na utakumbukwa daima nawalalahoi wa nchi hii,na utaandikwa ktk vitabu vya kumbukumbu za histroria ya taifa hili,aluta continua mjomba pinda mimi nakukubalisana,hakika wewe ni muadilifu na usiependa makuu.

Wewe ungekuwa waziri mkuu, ukatoa tamko la kubana matumizi kwa kutonunuamagari ya kifahari, later msaidizi wako anakuja kukukabidhi fungua ya gari la kifahari na kukujulisha kuwa yamenunuliwa hayo kwa mawaziri wote UTACHUKUA HATUA GANI? Huyu mzee aache kuwapumbaza wananchi, achukue hatua, magari yauzwe zinunuliwe prado tu! Mbona enzi za mwalimu walikuwa wanaendesha defender na pajero na walikuwa hawakoromi! Pinda; prove that you are not a weak PM.
 
- Mkuu understand kwamba haya magari wanapewa wabunge wote wa CCM na Wapinzani, lini tumesikia mbunge wa kawaida asiye Waziri mkuu akikataa haya magari?

William.

...William, wanapewa au wanakopeshwa. Hivi, siku hizi hawachagui wao wenyewe, wanachaguliwa na kupewa?
 
Back
Top Bottom