Pinda aingia mitini, ashindwa kukutana na wahadhiri

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Pinda aingia mitini, ashindwa kukutana na wahadhiri
• Wanafunzi Kitivo cha Elimu wamteka DC

na Danson Kaijage, Dodoma


amka2.gif
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, ameshindwa kumaliza kiu ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa madai kuwa hakuwa vizuri kiafya.
Taarifa iliyotolewa kwa wahadhiri hao na Waziri wa Elimu, Dk. Shukuru Kawambwa, alisema kuwa Pinda alishindwa kukutana na wahadhiri hao kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria.
Dk. Kawambwa alisema pamoja na wahadhiri hao kuwa na kiu ya kutaka kukutana na Pinda ili kutatuliwa matatizo yao, lakini alishindwa kuonana nao kutokana na kuumwa.
Aidha, katika ratiba yake, Pinda alitakiwa kutembelea maeneo mbalimbali ya chuoni hapo, ambayo yamekuwa yakionekana kuwa ni kero kubwa, ikiwa ni pamoja na kuangalia miundombinu ya maji, hali ya mabweni na wanafunzi kushindwa kupatiwa fedha za mikopo kwa wakati.
Katika msafara huo, wanafunzi wa Kitivo cha Elimu chuoni hapo waliteka msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, John Tupa, kwa saa tatu, ikiwa ni hatua ya kutaka kumshinikiza Waziri Pinda kuweza kuongea na wanafunzi hao.
Kutokana na hatua hiyo, wanafunzi hao walitoa upepo gari la mkuu wa wilaya, jambo lililosababisha kushindwa kuambatana na msafara wa Pinda kwa wakati.
Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa wataalamu wahadhiri katika chuo hicho, Paulo Louisulie, alisema wamekubaliana na maombi ya Pinda kwa kumtuma Waziri wa Elimu kuhusu kushindwa kwake kuonana na wahadhiri hao.
Mwenyekiti huyo pia alidai kuwa pamoja na kutoweza kuongea nao lakini wanamsubiri kwa kesho (leo) na wanachotegemea zaidi ni kuona jinsi gani wataweza kufikia muafaka juu ya madai yao .
Wahadhiri hao walidai kuwa hata wakikutana na Pinda hawataweza kuingia madarasani hadi walipwe fedha zao.
“Kwa sasa tunashughulikia haki yetu na si maneno yasiyo na msingi, ambayo yatatushawishi kuingia madarasani,” alisema.
 
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, ameshindwa kumaliza kiu ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa madai kuwa hakuwa vizuri kiafya.
Taarifa iliyotolewa kwa wahadhiri hao na Waziri wa Elimu, Dk. Shukuru Kawambwa, alisema kuwa Pinda alishindwa kukutana na wahadhiri hao kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria.

Hivi hawa viongozi mbona hivi...............................hata AG alikwepa kongamano la katiba mpya akidai anaumwa....................
 
sio kucheleshewa pesa za mikopo tu bali bodi ya mkopo imetuzulumu pesa za field mwaka jana kwa kigezo cha kutodaiwa baadae kitu ambacho ni ufisadi ,piatatizo la maji ni kbwa zaidi mpaka infika wiki maji hayatoki na kuna vyoo vya kuflash wanafunzi wanatumia muda mrefu kutafuta maji badadla ya kuingia madarasani na kusoma,hudma mbovu za afya inafika kipindi mpaka wanachuo wanalazimika kukodi magari kupeleka mgojwa hospitalini,tena cha kuhuzunisha zaidi hakuna vipimo dhabiti katika hospital za chuo ingawa wanafunzi wanatozwa Tshs LAKI MOJA YA MATIBABU.pia wanachuo cha dodoma pamojana wahadhiri hawamtaki prof mlacha kwa kile kinachodaiwa kuwa ni chanzo cha migogoro yote katika chuo cha dodoma maana anatafuna pesa za wanachuo kwa kuwalazimisha walipe pesa nying kuliko kawaida yake na kukataa kuzirudisha pindi wanachuo wanapozidai pesa zao
 
Sasa kama alikuwa anaumwa ameenda Dodoma kufanya nini? Hii ni kuchezea pesa zetu tu.
 
Back
Top Bottom