Pinda acha kutudhihaki

Hata bosi wake sialishangaza umati kwenye pre-conference ughaibuni eti anashangaa kwanini watz ni masikini....useless wote kiama yao inakaribia:A S 13:
 

Attachments

  • NALO NENO.JPG
    NALO NENO.JPG
    37.8 KB · Views: 30
Ashangae hapo kwa jirani zake tena karibu kabisa na kijijini kwao....natamani hata dawa za mchungaji loliondo zisiwaponeshe hao mafisadi wanaofanya ufisadi ndo ujasiriliamali wao
 
Mh.Pinda huku ni kutudhihaki Watanzania.Eti unashangaa watu kujenga nyumba za nyasi Ngara! Umetembea nchi nzima na kuona? Hujaona nyumba za tembe zilivyo zagaa Shinyanga,Tabora,Singida na Dodoma? Maisha yetu magumu sana wakati ninyi mnajinufaisha! Pesa tu ya mlo wa kilasiku kwetu ni mbinde,simenti na bati tutaviweza? Tujengeeni nyumba kisha mtupe bure,kwani pesa kiasi gani zinapotea? Nasi twataka kuifaidi nchi yetu wala sio wachache.Wengine mnaishi peponi bwana wakati sisi tupo kwenye mateso.Usishangae kwani Mh.wewe hujui?
hebu tupite mkoa wa rukwa tuone viroja

huyu jamaa sasa utani wake umezidi
 
Mnamshangaa Pinda kushangaa kwanini watu wanaishi nyumba za nyasi? mbona bosi wake aliulizwa kwa nini Tanzania ni masikini kupindukia naye akashangaa na kusema hajui kwa nini TZ ni masikini. Hao ndio Nahodha na Msaidizi wake katika meli yetu iliyo safarini ikipigwa na mawimbi. Lakini wao hawajui wapi north wapi east, bora liende tuu.
 
Hana lolote huyo kashindwa kusimamia matumizi ya serikali yake wananunua magari ya zaidi ya mil 260 yenye kutumia mafuta karibu mara tatu ya magari ya kawaida halafu leo anashangaa walala hoi kushi kwenye nyumba za nyasi kwanza kwanini hamkuondoka kwenye mkutano wake au mng'emzomea.

vipi watoto huwa wanakwenda kwenye mikutano yake maana hiyo sura duu.......
 
Alishangaa mtumizi ya ma V 8 (Mashangingi) Serikalini, akashindwa kudhibiti. Sasa anashangaa nyumba za tembe.

Madini Mrahaba asilimia 3
Songo songo sijui gesi ya nani
Na mengine mengi ndio yanayotufanya tuwe tofauti na Libya.
Mafuta ni ya walibya.
Madini ya huko kanda ya ziwa ni ya nani?

Mtoto wa Mkulima usisahau ulikotoka.:A S 13:
 
Mnamshangaa Pinda kushangaa kwanini watu wanaishi nyumba za nyasi? mbona bosi wake aliulizwa kwa nini Tanzania ni masikini kupindukia naye akashangaa na kusema hajui kwa nini TZ ni masikini. Hao ndio Nahodha na Msaidizi wake katika meli yetu iliyo safarini ikipigwa na mawimbi. Lakini wao hawajui wapi north wapi east, bora liende tuu.
Na kulia lia eti wachungaji wakemee mafisadi maana ni waumini wao kweli waziri mkuu unaweza kumtegemea mchungaji/sheikh awakemei mafisadi wakati serikali inawajua na haitaki kuwachukulia hatua...juzi aliomba majina ya wasambazaji wa sukari huko Bukoba sijui anataka kuwafanya nini au ni unafiki tu kama ni kuwachukulia hatua siaanze na mapapa walio tuibia mabilioni....Mkwere nae analialia tu uoh chadema wataleta machafuko ujinga mtupu....
Fanyeni kazi zenu ipasavyo na siyo kulialia kipuu
 
Back
Top Bottom