Pinda abebeshwa zigo

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Licha ya mpangilio wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) kujengwa kwa mpango ambao ungekwaza juhudi za chuo kugoma kwa mkupuo kutokana na kila kitivo kuwa mbali na kingine, mgomo wa kwanza na mkubwa umetikisha chuo hicho kipya ambacho ni fahari ya Serikali ya Awamu ya Nne.
Katika juhudi za kukinusuru chuo na mgomo huo mkubwa ambao chimbuko lake ni madai ya maslahi kadhaa ya msingi ya wahadhiri wake, serikali imeunda Tume tatu tofauti kushughulikia hali hiyo, huku Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiripotiwa kutua chuoni hapo kutatua hali hiyo leo.
Tofauti na vyuo vikuu vingine nchini, Udom kimejengwa kwenye miinuko ya vilima mbalimbali, kikiwa kimetanda umbali wa km tano.
Hali hiyo ilielezwa na wataalam wa saikolojia na menejimenti ya taasisi za elimu kuwa ni mbinu ya kuvunja mjumuiko wa pamoja kwa sababu kila kitivo kinajitegemea kwa miundombinu yake.
Pinda leo anatarajia kukutana na serikali ya wanafunzi pamoja na kuzungumza na wahadhiri wa Udom, huku tume hizo zikiagizwa kuanza kazi mara moja.
Tume hizo tatu zinaundwa na Katibu Mkuu Kiongozi kwa maelekezo ya Rais Jakaya Kikwete.
Tume hizo ni inayoundwa na Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG); Tume ya Makatibu Wakuu wa Wizara na ya tatu ni ya Kamisheni ya Vyuo Vikuu Nchini. Kila moja imepewa jukumu lake.
Tume ya CAG) itaanza kazi yake kwa kukagua mishahara ya wahadhiri hao.
Tume hiyo ilitarajiwa kuanza kazi mara moja kwenye ofisi za Hazina kwa ajili ya kukagua orodha ya wanaolipwa mishahara (Pay roll) Udom ambayo ndiyo madai yao makubwa.
Tume ya makatibu wakuu itadadisi masuala mbalimbali ya Udom na kujua matatizo yaliyopo na nini chanzo chake.
Tume ya Kamisheni ya Vyuo Vikuu vya Tanzania itaangalia masuala mbalimbali ikiwemo taaluma.
Habari za kuundwa kwa Tume hizo zilithibitishwa na Makamu Mkuu wa Udom, Profesa Idris Kikula, ambaye alisema zitafuatilia madai ya mishahara ya wahadhiri hao kama kweli ama la.
Profesa Kilula aliliambia NIPASHE jana jioni kuwa wajumbe wa tume hizo watakwenda Hazina na baadaye Jumatatu watakwenda Udom kufuatilia.
Hatua ya kuundwa kwa tume hizo ilichukuliwa baada ya wahadhiri hao kuendelea na mgomo na hivyo kushindwa kuingia madarasani kwa masharti kwamba kero zao zishughulikiwe kwanza.
Sababu kubwa iliyosababisha wahadhiri hao kugoma kwa siku kadhaa sasa ni kutolipwa mishahara mipya ambayo ilianza kutolewa na Hazina tangu Novemba 2010.
Hatua ya Rais Kikwete imekuja siku chache baada ya wahadhiri wa chuo hicho kudai kuwa hawataingia madarasani hadi hapo watakapoonana naye kwa ajili ya kutoa malalamiko yao.
Wakati Tume hizo zikijielekeza kwenye majukumu hayo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanataaluma wa Udom (Udomasa), Paul Loisulie, alisema kuwa Pinda atakwenda chuoni hapo kwa ajili ya kushughulikia matatizo mbalimbali ambayo yanaendelea chuoni hapo.
Hata hivyo, Loisulie alisema kwa upande wao bado wanaendelea na mkutano wao endelevu ikiwa ni pamoja na mchakato wa kuupeleka uongozi wa Udom mahakamani wiki ijayo.
Akizungumzia ujio wa Waziri Pinda, Loisulie alisema hata akienda kwa ajili ya kuwataka waingie madarasani hawatafanya hivyo hadi walipwe chao.
Loisulie alisema wao kwa sasa wanachoshughulikia ni haki yao na si maneno yasiyokuwa na msingi ambayo yatawashawishi kuingia madarasani.
“Sisi hapa tupo kwa ajili ya kupigania haki zetu, hata Pinda akija na maneno matupu hatutamsikiliza. Sisi tunachohitaji ni pesa tu na wala si kingine,” alisema Loisulie.
Miaka ya nyuma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ndicho kilikuwa chimbuko la migomo mikubwa ya vyuo vya elimu ya juu nchini, mgomo kumbwa zaidi ambao uliitingisha serikali ni ule wa mwaka 1990 ambao aliyekuwa Mkuu wa Chuo hicho wakati huo, Rais Ali Hassan Mwinyi, alikifunga kwa miezi minane, huko serikali yake ikilaumu jumuiya ya chuo kuwa kitovu cha wanamageuzi wakati wa vuguvugu la vyama vingi nchini.
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na maoni kwamba serikali kwa makusudi imekuwa ikikipendelea Udom ambacho kinakusudia kupanuka hadi kuchukua wanafunzi 40,000 kitakapokamilika.
Mahafali ya kwanza ya Udom yalifanyika mwaka jana, ambako pamoja na mambo mengine Rais Kikwete alipewa shahada ya daktari wa falsafa ya heshima (PhD). Mkuu wa chuo hicho ni Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.


CHANZO: NIPASHE
 
Kuundwa tume kuna mambo 2 huwa yanajitokeza...watabaini tatizo na kujua kila kitu ila utekelezaji wa mapendekezo ya tume hayatatokea ukizingatia pale kuna kesi kabisa iko wazi wameiba mishahaara wa wahadhiri kweupe ila tume itafukiaa kabisaa hilo suala wakati liko wazi....itawalipa arreas zote lengo kuwabakiza shemeji wa mkuu waendelee kupeta pesa za walipa kodi zimeteketea na tume haijafanya lolote lengo kuwapooza walimu na kuwa sevisha walaji...period
 
Tatizo mara nyingi tume za serikali zinaundwa kuangalia namna ya kuficha baadhi ya mambo hasa yanayowahusu wakubwa na zile zinazoamua kufanya kazi kwa uhakika mapendekezo yao hubaki kwenye mashelf!! Wahadhiri komaen hadi kieleweka!!
 
Tume za kuwajibika kwa rais siku zote hazina mashiko kama ingeundwa kamati ya bunge ingekua bora zaidi lakn sio tume ya rais. Hata waziri mkuu pinda ataenda kutoa majibu ya kisiasa tu. Wahadhiri hatua mliyofikia hampaswi kurudi nyuma. Wakati wa mapambano ndio huu. Hakuna kulala hadi kieleweke.
 
Kuundwa tume kuna mambo 2 huwa yanajitokeza...watabaini tatizo na kujua kila kitu ila utekelezaji wa mapendekezo ya tume hayatatokea ukizingatia pale kuna kesi kabisa iko wazi wameiba mishahaara wa wahadhiri kweupe ila tume itafukiaa kabisaa hilo suala wakati liko wazi....itawalipa arreas zote lengo kuwabakiza shemeji wa mkuu waendelee kupeta pesa za walipa kodi zimeteketea na tume haijafanya lolote lengo kuwapooza walimu na kuwa sevisha walaji...period
jIBU LA TUME LIKIWA MINUZ TOFAUTI NA MADAI YA WAHADHIRI MAANA YAKE MGOMO UTAENDELEA?JINGINE IKIONEKANA UONGOZI UNA MAKOSA KWAMBA KWELI WAMEIBA HIZO FEDHA ZA AREAS NA MISHAHARA HAWA WAKUBWA WATAWAJIBISHWA BINAFSI NAONA HILI SUALA LA TUME TAYARI HAPO SERIKALI IMESHAWAOGOPA HAWA WAKUBWA ESPECIALLY PROFFESSOR MLACHA KAMA WAHADHIRI WANAVYODAI MAY BE ANA MAHUSIANO NA MKULU WA NCHI NA PINDA NINA WASIWASI NAE SABABU MAMBO MENGI YUPO KIMYA SANA HILO SUALA HATA YEYE ANGEWEZA KULITOLEA MAAMUZI HAKUKUA NA ULAZIMA WA TUME SABABU HAZINA WANASEMA WALITOA FEDHA NA MAKARATASI YANAONYESHA HIVYO PIA HAPO KUNA SALARY SLEEP ZA AINA MBILI SASA TUME YA NINI WAKATI TATIZO LINAONEKANA WAZI KABISA!
 
Eti Chuo kujengwa scatted ili kupunguza mobilazation? Huko ni kujidanganya na mawazo mgando, hii ni dunia ya DOTCOM, dunia ya WWW, dunia ya Utandawazi. Mfano mzuri ni wanaJF tumetawanyika sehemu mbali*2 ya dunia ila tunahabarishana kama tuko nyumba moja na libeneke tunaliendeleza kama kawa.
 
Tume?Tume?Tume!Tumeeeeeeee!Basi iunde wizara ya tume kabisaaa tujue moja!Kila kukicha tume hata jambo linalo jieleza tume!Wanategenezeana posho tu na kufcha wizi wao....
 
waziri mkuu aja udom wakati huo management yamficha mgomo wa wanafunzi uliokuwa ukiendelea kitivo cha elimu na bado wameahidi kuliendeleza juma tatu wanafunzi hao wanawiki moja hawasomi,management yamficha pinda uovu, waziri mkuu akitaka aheshimike na kujua ukweli aongee na wanafunzi wote atagundua kuwa kiini cha tatizo ni nini,asipofanya hivyo itakwa sawa na bure kwani wenye matatizo ni wanafunzi na si management,bodi ya mkopo imekwa ikiiba pesa za wanafunzi tangu cho hicho kilipoanzishwa,vyombo vya habari vyaficha mgomo wa wanafunzi udom na kuutangaza ule wa malecturer tu basi itafahamika wanaafunzi watakapo rudishwa nyumbani
 
Back
Top Bottom