Pinda abanwa na wananchi; akwepa maswali yao!

Mara wamethubutu na wameweza. Mimi na wewe tukithubutu pia tutawashinda Mafisadi Tushikaman tulikomboe TAIFA LETU.
 
Chadema wamefanikiwa kwa sababu ya kuwafanya wananchi "wajisikie nyumbani". Siku watakapopoteza hii kitu watakalia kuti hilihili la CCM. CCM inabidi mjipange upya, mbadili na kuwafanya wananchi priority....else you are doomed! This country belongs to ALL sons and daughters of Tanzania no some group or people.
Wake up!
 
Sioni faida ya ziara ya waziri mkuu hata kidogo.
Hayo matamko/maagizo angeweza kuyafanya akiwa Dar, kutumia gharama kubwa ya fedha ya walalahoi kuja kuwakejeli kwa misemo ni kuongeza ukali wa maisha na machungu.
 
Wangeuonyesha mwamko huu wakati wa Mwalimu ningewasifu. Mwalimu aliiacha Mara hoi bin taaban si kwa miundombinu, elimu, uchumi,.... Watu wa Mara wakawa wanaishia darasa la nne na la saba tu kisha wanakimbilia jeshini.
Kuna kipindi cha mabadiliko kwa kila jamii. Mwalimu alikuwa "smart" kusoma ishara za nyakati na kustep down mapema. Viazi kama kina kingwendu wa magamba wanashindana na mabadiliko. Utakuwa mwehu ukifikiri zamadamu ni sasa. Au kuleta mambo ya "zamadamu" karne hii.
 
Wangeuonyesha mwamko huu wakati wa Mwalimu ningewasifu. Mwalimu aliiacha Mara hoi bin taaban si kwa miundombinu, elimu, uchumi,.... Watu wa Mara wakawa wanaishia darasa la nne na la saba tu kisha wanakimbilia jeshini.
<br>Kuna kipindi cha mabadiliko kwa kila jamii. Mwalimu alikuwa "smart" kusoma ishara za nyakati na kustep down mapema. Viazi kama kina kingwendu wa magamba wanashindana na mabadiliko. Utakuwa mwehu ukifikiri zamadamu ni sasa. Au kuleta mambo ya "zamadamu" karne hii.
 
Wangeuonyesha mwamko huu wakati wa Mwalimu ningewasifu. Mwalimu aliiacha Mara hoi bin taaban si kwa miundombinu, elimu, uchumi,.... Watu wa Mara wakawa wanaishia darasa la nne na la saba tu kisha wanakimbilia jeshini.
&lt;br&gt;Kuna kipindi cha mabadiliko kwa kila jamii. Mwalimu alikuwa "smart" kusoma ishara za nyakati na kustep down mapema. Viazi kama kina kingwendu wa magamba wanashindana na mabadiliko. Utakuwa mwehu ukifikiri zamadamu ni sasa. Au kuleta mambo ya "zamadamu" karne hii.
 
Kweli waziri mkuu wetu kilaza, yaani anadiriki kusema "Mzee wewe siyo wa kupata Njaa" na kwamba watamsaidia!!!!!!!!!!!.....Njaa ya huyo mzee inawakilisha njaa ya wananchi wa Pinda kwa ujumla, kitendo cha kumsaidia mzee mmoja ni kuendekeza na kuendeleza falsafa za kujuana! AKILI MBOVU KWELI!
 
Ccm mipangoyao nikuwapikia watu wali ,kuandikisha shahada za kura na rushwa ya pesa na mavazi na kuiba kura. Akiulizwa swali atajibu nini baba wa watu
 
Asanteni sana wananchi wa mara tupo pamoja. Tumechoka kudanganywa na hao viongozi uchwara wa magamba. Kumwona daktari, vipimo na kulala wodini ni bure kwa wazee, wajawazito na watoto chini ya miaka mitano. Dawa hakuna Kama unataka kufa jaribu kwenda hospitali bila hela utakufa.
 
Mjamzito anafanyiwa upasuaji ananunua kila kitu yaani ukiona karatasi la vifaa alivyoandikiwa akanunue inasikitisha sana, hadi nyuzi, dawa ya usingizi, gloves, iodine, drip, kiwembe cha kupasulia dawa za kutumia baada ya upasuaji kama huna hela utaumia hadi kizazi kichanike. Huyo pinda hebu awe serious na maisha ya watu.
 
&lt;font size=&quot;4&quot;&gt;Sioni faida ya ziara ya waziri mkuu hata kidogo.&lt;br /&gt;<br />
Hayo matamko/maagizo angeweza kuyafanya akiwa Dar, kutumia gharama kubwa ya fedha ya walalahoi kuja kuwakejeli kwa misemo ni kuongeza ukali wa maisha na machungu.&lt;br /&gt;<br />
&lt;/font&gt;
&lt;br /&gt;<br />
&lt;br /&gt;<br />
lile agizo alilotoa kwamba mabango ya matangazo ya waganga wa kienyeji yaondolewe (yang,olewe) limetekelezwa jijini dar-es-salaam?
 
Makamanda mlioko Igunga chukueni taarifa hii muwapashe wanaigunga wajue kinachoendelea sehemu zingine za nchi yetu. Wandanganywa kuwa Chadema ni chama kidogo kumbe sasahivi ndo babalao hata CCM hawaoni ndani
 
“Nimefurahi kukutana na Mzee aliyemfundisha Mwalimu, nimeongea naye ameniambia ana tatizo la njaa, nikamwambia Mzee wewe sio wa kupata njaa….sasa tutakaa tutaangalia namna ya kumsaidia”. - Pindia

Hehehe mwalimu wa Mwalimu Nyerere baada ya miaka 50 ya uhuru analia njaa! na umri wake ndio huo 121. Hadi wakakae na kuangalia halafu wakubaliane hiyo jinsi ya kumsaidia, huenda mzee atakuwa tayari hayupo! Mtaniambia.
 
Duh Chama changu kina pigwa! Kila kona kikienda kinabondwa tu, ndani ya chama vurugu, nje vurugu, Igunga maji ya shingo, sijui tukimbilie wapi?

Rais naye ndio kaziba masikio pamba, yeye ni kiguu na njia kila asubui.
 
pinda avuna aibu musoma


  • ni baada ya kuahidi afya bure, wananchi wamzodoa waziwaz
  • akiri kuwa chadema ni chama kikubwa, asisitiza amani na utulivu
  • nyerere amfunika, avuruga u-ccm kwenye ziara ya kiserikali

na edward kinabo, musoma


ziara ya waziri mkuu, mizengo pinda, iliyoanza jana mjini musoma mkoani mara, ilipata msukosuko wa aina yake, kutokana na wananchi waliojitokeza kumsikiliza kuikatisha hotuba yake zaidi ya mara tatu, wakimpinga waziwazi baada ya kuahidi kuwa serikali inajipanga kutoa huduma za afya bure.

Pinda alikumbana na msukosuko huo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa mukendo, mkutano uliohudhuriwa pia na mbunge wa jimbo hilo, vicent nyerere (chadema), meya wa mji huu, alex kisurura (chadema), na viongozi wa waandamizi wa kiserikali wa musoma na mkoa wa mara.

Wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo walianza kupaza sauti za kumpinga waziwazi kiongozi huyo huku baadhi yao wakizomea, pale alipoanza kuzungumzia uzinduzi wa zahanati ya kanisa la africa inland church alioufanya jana mchana katika kata ya bwire.

Akiisifu zahanati hiyo, pinda alisema serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na wadau wote wa afya nchini na kwamba inataka kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za afya bure.

Kauli hiyo ilizusha zogo kutoka kwa wananchi ambao walisikika wakiguna na kutoa kauli za kumkebehi.

“aaah aaaah aaah, uongo uongo, hamuwezi, people ndio wanaweza, people ndio wanaweza” , ulisikika umati huo ukisema.

People ndilo neno linalotumiwa na wananchi wengi wa musoma kumaanisha “chadema”.

Baada ya kupingwa na sauti hizo, pinda alisema, “pole pole jamani….looh, pole pole jamani, mbona mnatupelekesha hivyo? Jamani eeeh, naomba niwaambie kuwa hata hivi sasa watoto na wazee wanatibiwa bure, na watanzania wote wanaopelekwa nje kutibiwa magonjwa yasiyotibika hapa nchini, kama wanaokwenda china na india, wanagharamiwa na serikali…kwa hiyo…”.

Hata hivyo, kabla hajaendelea zaidi na alichokuwa anasema, wananchi hao walimkatisha tena wakisema “hamna, hamna, wanaotibiwa nje ni mawaziri….oooh oooh, hamuwezi”.

Baada ya hali hiyo, pinda alijikuta akiendelea kubishana na wananchi akisisitiza kuwa ni kweli wapo watanzania wengi wa kawaida wanaotibiwa nje ya nchi bure kwa kugharamiwa na serikali.

“wagonjwa wote wanaokwenda kutibiwa nje ya nchi wanalipiwa na serikali . Sehemu kubwa ya mzigo ule unabebwa na serikali. Hiyo ndiyo pointi yangu …”, alisema pinda na wananchi wakaikatisha tena hotuba yake na kupaza sauti za kumpinga.

“naona kuna wanasiasa wengi sana hapa…”, alisema pinda na kubadilisha mada ya afya aliyokuwa akiizungumzia na kuhamia kwenye hoja ya kupanda kwa bei ya sukari ambapo alisema kuwa tayari ameshatoa maagizo kwa viongozi wa kiserikali kuhakikisha wanadhibiti tatizo hilo.

Wakati akizungumzia hilo, baadhi ya wananchi walimkatisha tena wakimtaka ataje bei ya sukari itakuwa ni shilingi ngapi, wakisema "tunataka bei...tunataka bei...tunataka bei".


Licha ya kutakiwa kutaja bei, bado hakuitaja na badala yake alisisitiza kuwa amewaagiza viongozi wa serikali mkoa wa mara kutazama kiasi cha sukari iliyopo kwenye maghala na kuhakikisha kuwa inauzwa kwa bei nafuu kwa wafanyabiashara wadogo kwani ana taarifa kuwa bei ya sukari mkoani mara imekuwa ikipanda kwa kasi kubwa kutokana na sukari nyingi kuuzwa nchi jirani.

Wananchi hao waliingilia tena hotuba ya waziri mkuu, wakimtaka awape nafasi ya kumuuliza maswali, lakini aliwaomba wamuache kwanza aendelee na ajenda yake akisema kuwa atawapa fursa hiyo mwishoni.

“jamani naomba basi mniache kidogo nimalizie ajenda yangu halafu hayo mambo mengine nitawapa nafasi baadaye”, alisema pinda.

Hata hivyo katika hali iliyoonekana kuwashangaza wananchi wengi, pinda alihitimisha hotuba hiyo bila kuwapa wananchi muda wa kuuliza maswali na badala yake alisema “ jamani tutafuta muda mwingine tuje tuzungumze kwa kirefu, ahsanteni sana”, kisha aliingia kwenye gari na msafara ukaanza kuondoka.

Mkuu wa wilaya ya musoma mjini, godfrey ngatumi naye alikumbana na msukosuko wa wananchi wa musoma pale alipotoa fursa kwa viongozi wa kiserikali kusalimia wananchi katika mkutano huo wa hadhara, ikiwa ni pamoja na kumpa nafasi mbunge wa tarime, nyambari nyangwine (ccm) na waziri wa kazi, gaudensia kabaka, lakini bila kumpa nyerere nafasi ya kusalimia wananchi wake.

Kutokana na hali hiyo, wananchi walipaza sauti wakitaka mbunge wao apewe nafasi ya kusalimia, hali iliyomlazimu pinda kuingilia kati akiuliza "kuna nini", ndipo mkuu huyo wa wilaya akalazimika kumpa nafasi hiyo.

Nyerere aliwasalimia wananchi hao kwa salamu ya chadema ya peoples power, ambayo iliitikiwa kwa nguvu na umati wote wa wananchi huku wakimshangilia kwa nguvu.

Na baada ya kumalizika kwa mkutano huo, umati wa wananchi uliimba “peoples power… peoples power" na kulizonga gari la nyerere, wakimshangilia kwa nguvu na kumsindikiza, huku magari ya kiserikali yakiondoka kwa kasi uwanjani hapo.
Ziara hiyo ilianza rasmi jana asubuhi kwa pinda kutembelea shule ya msingi mwisenge aliyosoma baba wa taifa, hayati mwalimu julius nyerere, ambapo aliahidi serikali itafanya jitihada za kuhamasisha wadau wote kuiboresha shule hiyo ili kumuenzi baba wa taifa hasa katika kipindi hiki ambapo taifa linakwenda kuadhimisha miaka 50 ya uhuru.

Akiwa shuleni hapo pinda alipata nafasi ya kumsalimia mzee james irenge, mwenye umri wa miaka 121 ambaye aliwahi kumfundisha hayati mwalimu nyerere katika shule hiyo ya mwisenge kuanzia 1934 hadi mwaka 1936.

“nimefurahi kukutana na mzee aliyemfundisha mwalimu, nimeongea naye ameniambia ana tatizo la njaa, nikamwambia mzee wewe sio wa kupata njaa….sasa tutakaa tutaangalia namna ya kumsaidia”.

Kabla ya kuwasili pinda shuleni hapo, nyerere alipinga katibu wa ccm mkoa wa mara kupangwa kuketi meza kuu jirani na waziri mkuu, akisema ziara hiyo si ziara ya kichama bali ni ziara ya kiserikali na kuagiza kuwa nafasi hiyo aketi meya.

Kutokana hali hiyo, maafisa usalama walimuhamisha katibu huyo wa ccm kutoka kwenye nafasi hiyo, na baadaye meya aliketi hapo.

Ziara ya pinda ambayo itachukua siku saba katika mkoa wa mara itaendelea tena leo wilayani butiama.


hali hii intamkuta mzee wa suti(aka jk) akijaribu kuhutubia watu wa "a" town tunasubiri sana
 
pinda anamaanisha kuwa mzee akifa watafanya mazishi makubwa lakini siyo kumsaidia kwa chakula
 
ni faraja kuona watu wa musoma wameamka na wanajua kudai haki zao za msingi!sijui watanzania wote lini 2taamka kama wao
 
Back
Top Bottom