Pinda aapa bila Msaafu wala Biblia

Hatata mimi napatwa na wasiwasi kwamba inakuaje Pinda aapishwe bila BIble,Katika hotuba za BABA WA TAIFA MWL JK.NYERERE,Alisema na kusisitiza kwamba Kiongozi wa serikari lazima ataapishwa Eidha kwa MSAHAFU AU KUROHANI akasema kama sio muumini watatafuta namna ya Kumuapisha,(kwa pinda naungana na wajumbe wengine kuwa ameapa bila Msahafu kwa kumuogopa mungu dhamila inamsuta wakati yeye ni mcha mungu.
Ndio vitu gani hivyo mkuu!?
 
Vituko haviishi kila siku tunaona jipya? Natamani bunge letu liwe na demokrsia kama ya Kenya na India
 
Wanaelewa kuwa watajiongezea hukumu kwa kuahidi yalowashinda kuyafanya. Bora aape hivyo hivyo tu!
 
Nilishawahi kuuliza tusioamini mungu tukichaguliwa tutaapaje? Naona jibu ndilo hilo.

Pole pole watu wanaona misahafu ina busara, lakini ina uzushi mwingi tu, na wanaweza kuapa bila misahafu.
 
..hata mimi napata shida kidogo watu wanapoapa na kushika vitabu vya dini.

..sina uhakika kama kitendo hicho kinaendana na mafundisho ya dini husika.

..pia mambo wanayoapa kwenda kuyashughulikia hayahusiana na mafundisho ya dini.

..unaapa kuilinda katiba, huku umeshika msahafu au biblia. sasa hapo ni kipi kilicho juu ya mwenzake?
 
Unatakiwa kuthibitisha kuwa alicho shika si biblia.

Heshima yako mkuu wangu. Hapa janvini kila mtu anajivuna kuwa great thinker. Sina hakika kama wote tunajua maana na sayansi ya thinking. Umaskini wetu unatokana unatokana kwa kiwango kikubwa na ulemavu huu.
 
Kwanza kwa ushauri wabunge wa ccm wangetakiwa kuapa na kitabu chenye kanuni za nec kwani ndio waliowaweka madarakani, unapoapa kuitumikia nchi na wananchi ambao hawajakutuma inakuwa ina contradict. Wel done baba Pinda kwa kutoa ushahidi wa kwanza kabisa kwamba kura zilichakachuliwa. Na hii ni kilele cha mtu kufundishika mafundisho matakatifu yanayozuia wizi
 
DSC_1947as.JPG

Pinda ameshika Biblia hapa.
 
acheni uongo. Hebu angalieni michuzi blog. pinda ameshika bible. mkono wa kulia:A S angry::A S angry:
 
Kwani Hakuapa kuitii katiba na Rais? Pamoja na yote lakini Kaapa!!!!!! Nyerere alisema akiwa mpagani tutatafuta njia ya kuapisha sasa imetokea.
 
Mtu asiyeamini Mungu mnamtarajia ale kiapo vipi cha bunge au urais iwapo mwisho analazimika kusema " Ewe Mungu nisaidie"?

Kulazimishwa kusema hivyo, jee hakupingani na haki yake ya msingi kikatiba?

Akikataa kuimba wimbo wa taifa jee?
 
Heshima yako mkuu wangu. Hapa janvini kila mtu anajivuna kuwa great thinker. Sina hakika kama wote tunajua maana na sayansi ya thinking. Umaskini wetu unatokana unatokana kwa kiwango kikubwa na ulemavu huu.
Mkuu mimi ni mwanagenzi tu katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia, kutokana na forum hizi najifunza mengi na kukutana na wengi... Wakati wote tunapaswa kuweka ithibati ya yale tunayo yaandika ili yapate kujilinda yenyewe bila kuingiza ili na lile.

Ni matumaini yangu kuwa umenielewa ndugu yangu!
 
Hivi kumbe wanaapa kulinda na kuitetea katiba iliyo mbofu mbofu? Hata wa chadema wameapa hivyo?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom