Pinda aapa bila Msaafu wala Biblia

Yeye Katoka Rukwa Kingunge Ngombale Mwiru pia alikuwa haapi na Msaafu au Biblia; Inaonyesha kuwa watu wengi wa Rukwa hawana hizi dini za kupachikwa wanafuata fursa za kienyeji au tunaita upagani; Nyerere alikuwa anamsifia sana kingunge kila mara anatoa mfano wake kwenye masuala mengi tuu
 
Mbona nimeona kwenye Michuzi blog wamepost picha kashika kitabu cheusi, hicho kilikuwa kitabu gani. Jamani wanaJF tafadhali tuwe tunachunguza habari kabla ya kuitupa humu jamvini maana kuna maelfu ya watu tunaotegemea jamvi hili kama reliable source of information.
 
Kama kweli Pinda amefanya hivyo, naamini atakuwa ni mcha Mungu wa kweli!!!!! Ni dalili kuwa hataki unafiki na anajua fika Mungu hataki unafiki. Ahsante Mizengo.
 
Hatata mimi napatwa na wasiwasi kwamba inakuaje Pinda aapishwe bila BIble,Katika hotuba za BABA WA TAIFA MWL JK.NYERERE,Alisema na kusisitiza kwamba Kiongozi wa serikari lazima ataapishwa Eidha kwa MSAHAFU AU KUROHANI akasema kama sio muumini watatafuta namna ya Kumuapisha,(kwa pinda naungana na wajumbe wengine kuwa ameapa bila Msahafu kwa kumuogopa mungu dhamila inamsuta wakati yeye ni mcha mungu.
 
Anajua alichowafanyia wananchi wa jimbo la Sumbawanga Mjini, kisa kutishiwa na JK kuwa asipochakachua ataukosa u-PM

kwa kweli kwa kitendo alichofanya sumbawanga, angeshika Biblia tungemshangaa. Bora amejiweka wazi kuwa ni mwovu anayeitumikia serikali ovu inayoongozwa na mwovu.
 
Nimeipenda hii kwani huwa wanaapa na vitabu vitakatibu kisha wanakuja kufanya kinyume chake

UONGO MWINGINE , ALISHOSHIKA NI NINI
DSC_1947as.JPG
 
kwa kweli kwa kitendo alichofanya sumbawanga, angeshika Biblia tungemshangaa. Bora amejiweka wazi kuwa ni mwovu anayeitumikia serikali ovu inayoongozwa na mwovu.
Shangaa sasa....angalia picha hizo...mbona kashika biblia!!
 
Acha kuchakachua habari wewe. Hiyo aliyeshika kwa mkono wa kulia si biblia hiyo? au ni hirizi
 
tafadhali muwe na uhakika na mnachoongea. hivi mna uhakika alichoshika ni biblia?

Kwa sababu yeye ni mkristo na hata wakati wa kiapo cha ubunge alifanya hivyo

do we need a rocket science kujua alichoshika ni biblia au quran wakati tunajua ni mkristo
kweli JF ni zaidi ya thinkers
 
Hi
Maneno yenu sio kweli, nimeona picha kwenye michuzi wakati Pinda akiapa ameshika kitabu kidogo cheusi kwa mkono wa kulia
na karatasi nyeupe mkono wa kushoto. Mbona tunadanganyana kama watoto wadogo!!!!
 
Hata ingekuwa hajaapa kwa biblia kwani kutoamini Mungu ajabu?

Ni bora hata asitumie Bible maana wanayotenda ni kinyume na kilichomo kwenye bible. Wanafiki wakubwa. Hivi kwa nini wakiapa wasishike Ilani ya CCM maana hiyo ndio wanayoapia kuitekeleza na mara nyingi hawaitekelezi na matokeo yake kuja na data za uongo uongo?
:A S angry:
 
Nimeipenda hii kwani huwa wanaapa na vitabu vitakatibu kisha wanakuja kufanya kinyume chake


Kwaherini JF, kwa mtindo huu wa kudanganyana ni bora nijipe "ban" manake sasa JF inaanza kuwa kama kijiwe cha kahawa, kila mtu anajiandikia tu lolote lile analojisikia au alilosikia bila hata kuthibitisha. JF ilishajijengea jina kama one of the reliable information base, lakini kwa mwendo huu wa kudanganyana hata kwenye vitu vidogo kama hivi mmmh! sijui kama tutafika.
 
Kwa sababu yeye ni mkristo na hata wakati wa kiapo cha ubunge alifanya hivyo

do we need a rocket science kujua alichoshika ni biblia au quran wakati tunajua ni mkristo
kweli JF ni zaidi ya thinkers

acha rongo rongo bana, thibitisha kwamba alichoshika kilikuwa biblia. na swali la msingi ni kwamba, unajua unachosema?
 
Back
Top Bottom