pin code kwenye simu....

inapotokea wewe huna time na yake lakini yeye ndio kazi yake kupekua yako inakuwaje?.....mana nakerekaga sana, ukitoka kidogo tu unakuta cmu imepekuliwa mpaka bac.

Mi nikimfuma anapekua pekua na kujaribu jaribu password atakiona cha mtema kuni.
Cmu yangu binafsi hauiguswi hata chembe.
 
Abira chukua tahadhali safari imeanza hivyo funga mkanda,so aliyewekewa pin code ajue mwenzi wake kuna kitu kipya ameanza!
 
Sugar lakini kama wameoana will u let a little thing as this to break your marriage? you know there other ways to catch a cheating man... lakini hii ya password itakutolea raha bore.. mie wala sishiki simu yake... and if I have any doubts that he is cheating I will not tell him till I am 100% sure he is cheating...
 
ghafla tu mwenzako unaeishi nae ndani anaweka pin code kwenye simu ni inakua nini maamuzi,uoga au ni kutaka privacy maana nashindwa kuelewa na hiyo pincode hampi mwenzie hivi inawezekana kweli kwa uhusiano ulio wazi.....

mtu anaibiwa hapo... au usukununu umezidi
 
Pin code ni muhimu na ndio maana hio huduma ipo katika baadhi ya simu, is for security purpose only... sasa ukitoa pin code kwa m2 wa pili mbali na wewe.. hio haina umaana wowote... !!! Naomba ieleweke hivi ni for " Security " Hata kama ni kwa kulinda ndoa, ndio maana yake pia...!!
 
Tena kama wewe ndo nakuhitaji utoke chawote na vipin code vyako napasua simu tetetetee am kidding

Hahahaha hapo shingo inaweza ikachubuliwa.
Juzi kati hapa nilikuwa na toto la geti kufika kwa meza anaomba cmu yangu nilishangaa nikamuuliza unataka upige au unataka ufanyeje akasema anataka aangalie nikamwambia kama umejia hicho kuchunguza cmu yangu basi tuishie hapa hapa.
 
Dah...simu tena wajameni..safari hii PIN code!

haya za nini? mi nadhani watu wa hivyo bado hawajakomaa kimapenzi... eeh? ndo kutokujiamini huko!

Hivi hata kama ndo mechi za mchangani si yanaishia huko huko kwa nini mfatane hadi kwenye simu? (Fidel inahusu hapo)
 
Hahahaha hapo shingo inaweza ikachubuliwa.
Juzi kati hapa nilikuwa na toto la geti kufika kwa meza anaomba cmu yangu nilishangaa nikamuuliza unataka upige au unataka ufanyeje akasema anataka aangalie nikamwambia kama umejia hicho kuchunguza cmu yangu basi tuishie hapa hapa.
huyo nae ...
 
Hivi hata kama ndo mechi za mchangani si yanaishia huko huko kwa nini mfatane hadi kwenye simu? (Fidel inahusu hapo)

Hahahahaha mpwa kwema lakini? Wenzio twalowa huku vitanda vinaelea, Game za mchangani zipo busy na waheshimiwa kuwaliwaza yaani kama tupo maeneo ya USALULE kuleeeeeeeee.
Cmu yangu hagusi n'tu mpwa kuna kazi ya geti ikataka itizame cmu yangu nilimwambia haiwezekani kama amejia kupekua pekua hapo NO.
 
hahaha mpwa kwema kabisa......duh....hii SEACOM fever naona imeathiri wapwa wengi hapa hawaonekani

hahaha...usalule iko juu mpwa......sasa wa mchangani anataka kupekua simu tena ama ndo kapewa kidoela anataka mkono mzima?
 
ghafla tu mwenzako unaeishi nae ndani anaweka pin code kwenye simu ni inakua nini maamuzi,uoga au ni kutaka privacy maana nashindwa kuelewa na hiyo pincode hampi mwenzie hivi inawezekana kweli kwa uhusiano ulio wazi.....

unauliza majibu wewe pin code ya mwenzio tena ya simu yanini au unataka kufumania mimi nimeweka pini kodi kila mahali eti siku moja amekukuta ya laptop yangu yangu akaanza kulia nikamuuliza nini anasema eti umeweka pini kodi kwenye laptop kwanza laptop yenyewe ya kazi na kazi zangu ni za siri hata mke wangu mwenyewe hajui kazi hapasi kujua nafanya nini ingawa naajua ofisi ninayofanyia na anajua kazi yangu moja hiyo nyingine nuilisaini makataba kuwa itakuwa ni siri yangu na ofisi yangu kutokana na na unyeji wa kazi yenyewe sasa wewe unataka pasi wedi jamani kila kitu kina mipaka sio kwavile nimekuoa basi ndio niwe mtumwa
 
wewe mtumishi wa mungu nawewe pincode ya nini hizi ni kwa wanandoa tu wewe si mseja?
 
Hapo ni wazi kwamba something is going on underground, mojawapo ya mambo ya msingi kwa watu wapendanao tena wanaoishi pamoja ni kuwa wawazi. Ifikie hatua hata kupokeleana simu au kujibiana messages au hata kama umepinda unahamisha salio.

mojawapo ya mambo ya msingi kwa watu wapendanao tena wanaoishi pamoja ni kuwa wawazi. Ifikie hatua hata umweleze mwenzako kuwa una kimada nje ya ndoa?
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom