Pima hoja za Mnyika na Nape juu ya shutuma za mauwaji ya wana-CHADEMA

Hivi nani alisoma na Nape o level alipata div gani na A level alipata nini? Manaake msije mkawa mnaelezea mambo magumu!

Mkuu,kuwa mvumilivu.
Sikusoma naye ila ninaifahamu historia ya elimu yake.
Siku nikiamka vibaya nitapata muda wa kuichambua elimu ya jamaa kwa hizo ngazi unazotaka kujua.
Ninajua wengi mna hamu ya kuijua.Ila kwa sasa jua tu kuwa alikuwa na matokeo mabaya.
Nadhani hata yeye mwenyewe huwa yanamnyima amani!
 
Hoja zote mbili yaani ya Nape na ya Myika zina mashiko....... Ya Nape, si vema kuwaaminisha watu hata mwana CDM akiiba na kuuwawa na rai wema basi ameuwawa na CCM kwakuwa ni mwana CDM Ya Mnyika, ni kweli CCM imeshindwa wajibu wake kama mtawala
Wala hoja za Nape hazina mashiko, huwezi ukaacha kuhusianisha kukatwa mapanga kwa akina Kiwia na siasa za CCM maana ni ugomvi tu wa udiwani wa kata ya Kirumba na Masamaki walidhani pesa ndiyo kura kumbe siku hizi...uadilifu na mabadiliko ndiyo kura!!! Wanahusika kote Igunga, Mwanza, Arusha, etc Ila kama polisi ni wema tutaona uchunguzi wao...kwa kuwa hatuwaamini tuombe CDM wapeleke kesi mahakama kuu ili turuhusiwe kuomba na kulipia 'indipendent investigator' na CDM pitisheni mchango sisi tutatoa kuujua ukweli, maana binafsi sina imani na vijana wa Mwema kama wanaweza kutenda haki katika sakata hili maana linawahusu ndo waliona na kukaa wakati watu wanakatwa mapanga...!!
 
Mtu kama Nape Moses Nnauye siwezi hata kubishana nae huyu sana sana naweza kumuweka na mtoto wa darasa la tatu kwa mdahalo huyu mtoto ndio atakuwa saizi yake ni kweli kabisa Kamanda ModdyMtoi kasema ukinywa uchafu utatoa uchafu kama sijakosea kunukuu maneno yake.Huyu jamaa hivi kwa nini asijipange vyema kabla ya kwenda kwenye vyombo vya habari.
 
Wamekanusha ili ICC wasije kuwachunguza wanajua kabisa mambo yakiwa wazi kuna watu watawajibishwa na mahakama ya kimataifa ndio maana wamekurupuka kukanusha.
Lakini ukweli utabaki palepale kwamba uchu wao wa kung'ang'ania madaraka hata kama wanarudisha nyuma ustawi wa nchi na wananchi ndio unaowafanya waue watu wenye misimamo tofauti na wao ambao wanatishia maslahi yao.
Lakini wajue wanaipeleka nchi kwenye machafuko kama hawatakubali sauti ya wanyonge inayosema yatosha sasa basi wapisheni wengine waoneshe uwezo wao lengo ni kuiona Tanzania inapiga hatua kuliko hivi sasa ambapo kila kitu kipo-stagnant.
 
kibogo najua unapenda kusikia tu mtu akiipamba CDM au akiiponda CCM basi........kuna wengine hatuangalii mambo haya kwa jicho la upofu wa mahaba ya vyama., inawezekana hayo mauji yapo kweli lakini si sahihi pia kusema kila mauji yaliotajwa ya mwana CDM ni mbinu ya CCM kuwatisha eti wananchi wasiingie upinzani........
Ndg. Paulss sipo katika ushabiki wowote wa Chama hapa naoanisha matukio ya vifo hivyo, kwa mtu yeyote mwenye fikra pevu hawezi kuwa na mtazamo tofauti wa ninavyosema mimi na hii ni kutokana na hali ya sasa kisiasa ilivyo katika nchi yetu.
 
Wakuu.
Great thinkers lazima tujifunze kuwa independent thinkers! Najua wote kwa umoja na wingi wetu tu mashabiki, wapenzi, wafuasi au wanachama wa vyama fulani. Tujifunze kuwa katika ushabiki wetu hakuna alie mtanzania kuliko mtanzania mwingine.

Swala la vifo au kuuwawa kwa ndugu au jamaa zetu kutoka katika chama chochote cha siasa halipaswi kuangaliwa kwa ushabiki kwa namna yoyote ile maana ni kinyume na mafundisho ya mungu lakini pia ni kinyume na hitaji la kikatiba lenye kutambua haki ya kuishi kwa kila raia.

Tujadili kauli za Nape kwa tahadhari ya kupima usalama na uwajibikaji wa serikali yetu maana vifo au mauwajaji vikiwa vya utata hudondokea kwenye uchunguzi wa vyombo vya dola.
 
Kweli, hapo ndio niliona tofauti za vijana hawa wawili. Niliona taarifa ya Nape kwenye wanabidii ambayo ukiisoma huwezi kuamini kama ni tamko rasmi la CCM namna lilivyo na mipasho. Halafu Mnyika akajibu kwa email ambayo inaonyesha kutumwa toka simu ya mkononi ya Nokia, kwa hiyo inaonyesha ni majibu ya haraka lakini yenye hoja.
 
Habari ya nape-ni propaganda,inakanusha...... sawa na za yule jamaa yao aliyeondoka baada ya Makamba

Habari ya Mnyika -mantiki, inaongelea matukio na mifano na inatoa mwelekeo wa tufanye/serikali ifanya nini
 
mbowe naye mtata,nassari akisema watu wajitenge anasema ana akili ya kitoto,yeye anatuhumu bila stroeg evidence,tutamvua uchairman
 
Ukiwa ccm hata kama ulikuwa na akili nzuri upeo wako unakuwa duni.kama wanatuchagulia hadi darasa la 7 kuwa madc hapo inakuwaje
 
Hivi karibuni chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kilielezea kile ilichoeleza kuwa ni kutishwa na wimbi la mauaji yanayotishiaamani ya nchi kikidai kuwa jumla ya wanachama wake 15 wameuawa katika wilaya ya Igunga peke yake.

Madai hayo ya CHADEMA, pamoja na wanachama wengine na mashabiki wao, yalitolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, ambaye alidai kuwa mauaji hayo yana mkono wa serikali ya CCM, ambayo kwa madai yao imeona wazi kuwa upepo wa kisiasa umekiendea vibaya na sasa kinataka kujiimarisha katika utawala kwa kuua watu wanaoipinga.

Akifungua kikao cha Baraza Kuu la chama hicho jijini Dar es Salaam Aprili 29 mwaku huu mwenyekiti huyo alifafanua kuwa mbali na kuuawa kwa watu wanne kwa pamoja na juzi kifo cha mwenyekiti wao wa tawi huko Arumeru mkoani Arusha, jumla ya wanachama wake 15 wameuawa katika wilaya ya Igunga peke yake tangu kumalizika kwa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo mwaka jana. Mbowe katika maelezo yake alijaribu katika maeneo kadhaa kuihusisha CCM na au serikali yake katika matukio kadhaa yaliyowakabili baadhi ya wanachama na viongozi wa Chadema katika maeneo mbalimbali nchini likiwemo lile la Mbunge Highness Kiwia ambaye Suala lake bado Lipo mikononi mwa vyombo Vya dola likishughulikiwa.

Katika sehemu kubwa ya maelezo ya Ndg. Mbowe amejitahidi kuonesha kuwa mauaji yote yaliyoikabili na yatakayokuwa yakiikabili Chadema kupitia wafuasi wake yanafanyika kisiasa, Jambo ambalo ni la uzushi, kwani Halina ushahidi wa kisheria hata kimazingira, wa Moja kwa Moja unaoondosha ujinai au makosa hayo, na kuwa ni makosa yanayolenga muktadha wa kisiasa.

Huku akitaka kuuaminisha umma kuwa huo ndio ukweli, Ndg. Mbowe amesisitiza kuwa hilo lime kuwa likitekelezwa na CCM kwa lengo la kuwatisha wananchi kujiunga na chama hicho hoja ambayo haina msingi wowote wa kiutafiti.

Hivyo CCM kwa kutambua kuwa Suala la mauaji linabeba Kosa la jinai, na kwa kuwa Ndg. Mbowe ameshutumu Moja kwa Moja CCM na serikali yake kuihusisha na mauaji hayo, ni vema sasa nasi tukatoa msimamo wetu dhidi ya tuhuma, hiyo.

Kwanza, si busara hata kidogo kuihusisha CCM katika matukio hayo, kwani uchunguzi unaofanywa na vyombo vya dola umeshindwa mpaka sasa kuhusisha matukio hayo na siasa, badala ya kuyahusisha na makosa ya jinai ambayo hufanywa na watu kwa malengo tofauti na yale ambayo Ndg. Mbowe anataka kuwaaminisha watu.

Pili, CCM haijawai, haiwezi, na haitakuja fanya jambo lolote lenye lengo la kuvuruga Amani na Usalama wenye utulivu ndani ya taifa letu, hivyo uzushi na usingiziaji uliofanywa na Mtu Kama Ndg. Mbowe, si vema kuuacha kimya, badala yake nimetumia wasaa Huu muhimu Kujibu, na kutoa ufafanuzi ili Kuupa umma wa watanzania habari sahihi.

Ni aibu kwa Chama kama Chadema kujitahidi kwa nguvu zote kujaribu kuficha ukweli wa mauaji yanayotoa roho za watanzania wenzetu kwa kuyapa sura ya kisiasa. Hizi ni juhudi za makusudi za kutaka kuficha ukweli wa kinachotokea.

Ni aibu kwa chama kama Chadema kujaribu kutumia mauaji mabaya kama haya kutafuta mtaji wa kisiasa. Huku ni kuonyesha jinsi gani wamefilisika kisiasa mpaka wanafikia mahali pa kuamini kuwa wanaweza kutumia chochote kama mtaji wa kisiasa, vikiwemo vifo vya watanzania wenzetu. Huku si kufilisika tu ila kwakweli ni unyama unaotakiwa kulaaniwa na kila muungwana.

Mwisho.

Imetolewa na:
Nape Moses Nnauye
Chama Cha Mapinduzi
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Taarifa hii ya CCM inadhihirisha masuala kadhaa ya msingi;

mosi, kwamba chama legelege huzaa serikali legelege. Ulegelege wa serikali katika kushughulikia masuala ya mauji ya raia ni matokeo ya CCM kushindwa kuonyesha kwa vitendo inavyothamini utu na uhai wa binadamu. CCM isingekuwa legelege ingeiwezesha serikali inayoongozwa na wanachama wake kufanya uchunguzi wa vifo vyenye utata (inquest) kupitia mahakama maalum (coronary court).

Pili, kwamba CCM imekosa uhalali wa kimaadili wa kukumea vitendo hivyo na kuchukua hatua zinazostahili kwa kuwa wanazungumza maneno matupu ya amani na utulivu huku viongozi na wanachama wake wanafanya matendo ya vurugu na umwahaji damu. Nape anasema hakuna ushahidi wa kimazingira, wakati anajua kwamba mpaka sasa kuna majalada yamefunguliwa dhidi ya viongozi wa CCM Kiteto, Busanda, Biharamulo kwa vitendo vya umwagaji damu kwenye kampeni za chaguzi ndogo. CCM inajua pia kifo cha kiongozi wa CHADEMA Arumeru mpaka sasa kuna viongozi wake wamekamatwa na kuhojiwa na polisi. CCM inajua kuwa makada wake wametajwa kwa majina kwenye tukio la kukatwa mapanga kwa wabunge wa CHADEMA Mwanza tukio ambalo mashahidi wameeleza kuwa hata Askari polisi wameshuhudia na kuachia litokee.

Na CCM inajua kilichomo mpaka sasa kwenye jalada la uchunguzi la mauji ya Mbwana Masudi kule Igunga. Orodha ni ndefu ya watu na matukio, hivyo taarifa ya CCM ya kutoa kanusho la ujumla ni ishara ya kufisha ukweli na kugeuza mjadala suala ambalo halitafanikiwa, tamko hili la Nape ni kama Al Sahaf kule Iraq, CCM ikae vikao vyake vya kikatiba itoe maamuzi ya chama hicho kuhusu suala hili la umwagaji damu na mauaji ambayo yanatuhumiwa kufanywa na viongozi wa chama hicho pamoja na vyombo vya dola sio kwa wanaCHADEMA tu bali hata kwa wananchi wa kawaida. Inapaswa kuwa kutoka kauli ya amiri jeshi mkuu na kiongozi wa serikali Rais Jakaya Kikwete. Tunachohitaji kusikia ni hatua kuchukuliwa kwa wahusika kama kweli hawajatumwa na CCM na serikali na sio propaganda.

Tatu, imekuwa ni kawaida ya CCM kuanza kwa kuukana ukweli unapotolewa lakini hatimaye hukiri sehemu ya ukweli huo kama zilivyokuwa kauli za CCM mara baada ya kutolewa hadharani kwa Orodha ya Mafisadi. Walianza kwa kanusho lakini hatimaye wakakubali kuna ufisadi ila wakadai mafisadi ni baadhi ya wanachama na sio chama, lakini mpaka leo wameshindwa kujivua gamba kama walivyodai. Hata hili, wameanza kwa kukukana baadaye wanatesema ni la wanachama wachache waliotenda jinai bila kutumwa na chama, lakini ukweli utabaki kwamba haiwezekani matendo yote haya yakajirudiarudia bila vyombo vya ulinzi na usalama kufahamu. Na tunazo taarifa juu ya mikakati ya CCM ya vurugu na vikundi wanavyotumia kufanya uharamia, na yapo majalada ambayo yamefunguliwa polisi. CCM inahitaji ushahidi gani zaidi toka kwa CHADEMA na umma?

John Mnyika
Kwa nini Rais hayuko tayari kukubali kuunda tume huru ya kijaji kuchunguza hivi vifo vyenye utata?

Kuna nini anachoogopa kitafichuka kwa kuchunguza mauaji haya kwa kutumia tume huru ya kijaji?
 
hapa sasa ndo tunapata uhakika kwanini watu wa ubungo walimchagua mnyika na kumwacha huyu nape, soma maandishi yao then utaona nani kichwa hapo!

CDM wekeni KUMBUKUMBU zote za manyanyaso,mauaji,vipigo mnavyopata kutoka kwa magamba na polisi wake.tena "IN DETAIL".
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom