Pillars of The State

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,273
17,096
Naomba wataalam wa constitutional affairs watuongoze juu hizi pillars of state.....

Executive (JK);

Parliament(6);

Judiciary (Ramadhan);

Media (not in tanzania)

..zinafanyaje kazi?..mbona JK anamuapoint CJ, ni sawa hili? Nchi nyingine wanafanyaje (hasa India na Pakistan) ..na je kwa nini rais ana maguvu mengi na inashindikana kumweka sawa... ana mamalaka mengi zaidi ya uwezo?
 
president amepewa power na katiba kumuapoint cj, hii ni katika kuhakikisha principle ya check and balance inatumika jua hakuna absolute separation of power, pia media ra madhan zipo chini ya Parliament.bunge linapitisha sheria ya haya mambo..lkn tatizo ni kwamba pres amekuwa vested na alot of power and protection na ndio maana wanaharakati wanalilia constitutional amendmend kupunguza power kama hizi...

soma katiba fresh
 
Kwa Tanzania we have the executive headed by the president,the judiciary headed by the chief justice and the parliament consisting of the national assembly headed by the speaker of parliament one on side and the president o other side.

kwenye such system,the doctrine of separation of powers is adhered to with due respect to the doctrine of checks and balances.this answers your question as to why JK has to appoint the CJ.
If this three organs do not interact it may bring the whole system down.

Suala la JK kumu-appoint CJ may interfere with the independence of judiciary but one aspect in the constitution has limited the President's powers that is the President is bound by the advice regarding the attitude or behaviour of a justice of the court.

Rais wetu ni kweli kuwa ana madaraka mengi.kila nchi ina mfumo wa utawala wake.mfano tanzania ina mfumo wa presidential and executive supremacy.nchi kama UK ina parliamentary supremacy coz bunge lake ndio liko juu coz hamna chombo chochote kile chenye madaraka ya ku-declare against ama over-rule any laws passed by the parliament.

Marekani ina mfumo tofauti kidogo kwa sababu the Judiciary has the power to declare the powers and acts of the executive as ultra-vires the constitution na kuzi-overrule
 
Ukiangalia nchi nyingi, lazima katika hizi pillars kuwe na link flani. Kwa mfano, kwa sasa Uingereza, Executive na Parliament zimeungana kikaribu. Na pia ukiangalia ofisi ya AG, yeye yupo kote kutatu. Kwa Tanzania, in theory, bunge ndo the most powerful institution. Maana lina hata uwezo wa kumu-impeach Rais, na kumweka kando - s46A Katiba ya Jamuhuri ya Tanzania. Lakini pia kumbuka bunge = Rais na Wabunge....s62(1) ya Katiba.

Lakini tatizo nionalo mimi kwa sasa bunge na chama ni kama kitu kimoja. Na chama na serikali ni kitu kimoja. Which means bunge na serikali ni kitu kimoja. Je siku Rais akatoka chama A na bunge likawa na majority ya chama B, serikali itaundwa na nani?

Kumbuka:

36.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika Katiba hii na ya sheria nyingine yoyote, Rais atakuwa na
mamlaka ya kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namna mbalimbali katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Rais atakuwa na madaraka ya kuteua watu wa kushika nafasi za madaraka ya viongozi wanaowajibika kuweka sera za
idara na taasisi za Serikali, na watendaji wakuu wanaowajibika kusimamia utekelezaji wa sera za idara na taasisi hizo katika
utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano, nafasi ambazo zimetajwa katika Katiba hii au katika sheria mbalimbali
zilizotungwa na Bunge kwamba zitajazwa kwa uteuzi unaofanywa na Rais.
Hapa ndipo mchezo unanoga.

Napenda sana Public Law. Ngojea nimalize shule tuje kubanana huko huko Bongo.

Kwa hiyo mh, hizi pillars ni muhimu katika ku-keep separation of power. Lakini sidhani kama kuna shida kama Rais ana uwezo wa kumchagua CJ. Cha muhimu ni nguvu ziwe kwa wananchi. Na hapa kwetu wananchi = Bunge kutokana na direct accountability yao. Hivyo in theory, Bunge ndo lenye nguvu.

But in practice, CCM ndo yenye nguvu na sio Rais... hahahaha!
 
Je siku Rais akatoka chama A na bunge likawa na majority ya chama B, serikali itaundwa na nani?

Ieleweke kwamba kwa Tanzania, iwapo rais ametoka chama A na bunge majority limetoka chama B, ni bunge ndio linalomchagua waziri mkuu hivyo basi tutakuwa na rais wa chama A na waziri mkuu kutoka chama B then ni waziri mkuu akishirikiana na rais ndio wanatengeneza cabinet.

Rais hawezi kum-suggest waziri mkuu kutoka A party minority. Its obvious, clear and with no doubt hatapitishwa!
 
Ningependa kusahihisha statement yako. Katiba inasema hivi:
51.-(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
atakayeteuliwa na Rais
kwa kufuata masharti ya ibara hii na
ambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais
kwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa
na Bunge.
(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku
kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua
Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi
anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi
Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge
wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge walio
wengi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika
madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa
na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge
walio wengi.

Hivyo basi, it's clear kwamba Rais ndo anayemchagua waziri mkuu na Bunge ndo linalomthibitisha. Na sio Bunge kumchagua.
Anyway, ndo hapo sasa tunataka kuleta mchezo wa Kenya na Zimbabwe. Sasa inaponoga zaidi ni hapa:

53.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, Waziri Mkuu
atawajibika kwa Rais kuhusu utekelezaji wa madaraka yake.
(2) Serikali ya Jamhuri ya Muungano, chini ya mamlaka ya
Rais, ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya
Serikali kwa jumla, na Mawaziri, chini ya uongozi wa Waziri Mkuu,
watawajibika kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuli
za Serikali ya Jamhuri ya Muungano
.

Kwa hiyo basi, serikali inaongozwa na Rais, full stop. Sasa kweli itawezekana kuwa na serikali iliyoundwa na vyama viwili?

Mtoto,

Nimekuelewa vizuri na asante kwa kisomo.I probably meant the same thing nadhani Kiswahili ndio kimeniingiza chaka.Thanks.

Well nakubaliana na wewe kwamba Rais ndiye anayeongoza serikali coz Rais is not bound by decisions of the cabinet sasa ndio hapo vile vile issue ya accountability ya Mawaziri na Waziri Mkuu linapoleta utata.
Inakuwaje wanakuwa accountable na decisions ambazo Rais amezifanya either without their approval and consultation???

Uwezekano wa Serikali mbili upo lakini sasa ndio yale yale ya mambo ya Kenya na Zimbabwe na Rais ku-over exercise his veto powers!!!!!!!!
 
Hamna kware mh. Mawaziri wanakuwa accountable kutokana na principle ya collective accountability. kitu kinachoamuliwa in Cabinet, hata kama wewe hukubaliani nacho, lazima ufuate. Kama hutaki, basi ni sharti u-resign. Rais yeye ana-chair Cabinet, lakini anakuwa adviced by Ministers. Kwa hiyo wanafanya kazi as a body. Ndo maana (nadhani) ilimbidi JK avunje Cabinet pale ilipobainika Richmond ilipitia kule na kumfanya PM ku-resign. Sasa cha kuchangaza na yeye hakujiwajibisha. Lakini anaweza ku-argue kuwa yeye alikuwa adviced by hao ministers, na alipo-make the decision, alikuwa anafuata advice yao. Hivyo he was making a decision w/out having all the information. Hili ndilo Dk Slaa anaimba nalo kila siku.
Pia kumbuka:

54.-(1) Kutakuwa na Baraza la Mawaziri ambalo wajumbe
wake watakuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa
Zanzibar na Mawaziri wote.
(2) Rais atahudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri na ndiye
atkayeongoza mikutano hiyo. Na endapo Rais hayupo basi
mikutano itaongozwa na Makamu wa Rais na kama wote wawili
Rais na Makamu wa Rais hawapo Waziri Mkuu ndiye ataongoza
Mikutano hiyo.
(3) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara ya 37(1) ya
Katiba hii, Baraza la Mawaziri litakuwa ndicho chombo kikuu cha
kumshauri Rais juu ya mambo yote yanayohusika na utekelezaji
wa madaraka yake kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii, na
litamsaidia na kumshauri Rais juu ya jambo lolote
litakalowasilishwa kwenye Baraza hilo kwa mujibu wa maagizo
maalum au maagizo ya jumla yatakayotolewa na Rais.

(4) Mwanasheria Mkuu wa Serikali atahudhuria mikutano yote
ya Baraza la Mawaziri na atakuwa na haki zote za mjumbe wa
mikutano hiyo isipokuwa hatakuwa na haki ya kupiga kura katika
mikutano hiyo.
(5) Suala kama ushauri wowote, na ni ushauri gani, ulitolewa
na Baraza la Mawaziri kwa Rais, halitachunguzwa katika
mahakama yoyote.

Soma vizuri kifungu cha tano. Kama ni hivyo, basi ishu za Richmond kama zilipitia Cabinet, haziwezi kujadiliwa mahakamani. Au sio?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom