Pigo jingine CUF: sekretarieti ya vijana Bara yajiuzulu.

tatizo la chama cha upinzani kikiamua kujiunga na chama tawala basi ujue ndio mwanzo wa kufa kwa chama. Mfano angalia kule uk, liberal democrats walifanya kosa la kujiunga na conservatives sasa hivi hicho chama ndio kimeshakufa na uchaguzi mkuu wa uk hawatapata hata kiti kimoja cha ubunge.
 
Nini tatizo lililosababisha wajiuzulu!? Au ni mwendelezo wa kuvua gamba umeikumba hadi ccm B?

Gamba litawatesa sana kwani wamekunywa mvinyo uleule wa CCM na ndio unaanza kuvuruga hali ya hewa tusubirie kuona mengi kutoka CUF na hiyo ndoa yao itavunjika,
 
Gamba litawatesa sana kwani wamekunywa mvinyo uleule wa CCM na ndio unaanza kuvuruga hali ya hewa tusubirie kuona mengi kutoka CUF na hiyo ndoa yao itavunjika,

Kwa style hii hakika gamba linawatesa.......huwezi ku'team up na Magamba then ukapona, haiwezekani. 'Ni Kama kula nyama ya MTU......' hutoacha (baba WA TAIFA alinena haya)
 
Katika ule muendelezo WA kuangamia kwa chama cha wananchi CUF almaarufu Ngangari, Uongozi WA Sekretarieti ya Vijana Taifa ya chama hicho Bara imejiuzulu rasmi hapo tar.08-06-2012.
Waliojiuzulu ni pamoja na Mwenyekiti wao MHE. Mohamed Babu, Naibu Katibu Mkuu WA Sekretarieti Bara MHE. Abubakar Kitogo, Mkurugenzi WA Fedha MHE. Maulid Said, Mkurugenzi WA Mafunzo na Mausiano Vijana MHE. Dalia Majid, Mkurugenzi WA Mipango na Uchaguzi MHE. Grace Mgumba.
Wengine ni Wajumbe WA Sekretarieti hiyo ambao ni Mussa Mbarouk (Diwani CUF - Tanga), Daalin Mlenga na Asumini Maringo Shayo.
Hili ni pigo jingine kubwa kwa Oganaizesheni hiyo HASA ukizingatia MIEZI michache aliyekuwa Mkurugenzi WA Sanaa na Utamaduni MHE. Omar Costantine kujiuzulu na kuhamia chama kipya cha ADC.
Tukio hili limetokea sambamba na Naibu Katibu Mkuu Bara MHE. Julius Mtatiro akiwa safarini kikazi mkoani Arusha kupoteza Laptop na nyaraka nyingine muhimu za chama.
Ndani ya Laptop hiyo kulikuwepo na MPANGO MKAKATI WA CHAMA TAIFA 2013/2015 kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao WA 2015.

Same source.

Kumekua na upotosha wa chama Tawala CCM ya kua CHADEMA ni Chama cha udini hiki CUF tukiitejea?Au kwa kua hakuwanyimi usingizi na ni Mke mdogo.
 
Back
Top Bottom