Pigo jingine CUF: sekretarieti ya vijana Bara yajiuzulu.

hasan124

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
716
128
Katika ule muendelezo WA kuangamia kwa chama cha wananchi CUF almaarufu Ngangari, Uongozi WA Sekretarieti ya Vijana Taifa ya chama hicho Bara imejiuzulu rasmi hapo tar.08-06-2012.
Waliojiuzulu ni pamoja na Mwenyekiti wao MHE. Mohamed Babu, Naibu Katibu Mkuu WA Sekretarieti Bara MHE. Abubakar Kitogo, Mkurugenzi WA Fedha MHE. Maulid Said, Mkurugenzi WA Mafunzo na Mausiano Vijana MHE. Dalia Majid, Mkurugenzi WA Mipango na Uchaguzi MHE. Grace Mgumba.
Wengine ni Wajumbe WA Sekretarieti hiyo ambao ni Mussa Mbarouk (Diwani CUF - Tanga), Daalin Mlenga na Asumini Maringo Shayo.
Hili ni pigo jingine kubwa kwa Oganaizesheni hiyo HASA ukizingatia MIEZI michache aliyekuwa Mkurugenzi WA Sanaa na Utamaduni MHE. Omar Costantine kujiuzulu na kuhamia chama kipya cha ADC.
Tukio hili limetokea sambamba na Naibu Katibu Mkuu Bara MHE. Julius Mtatiro akiwa safarini kikazi mkoani Arusha kupoteza Laptop na nyaraka nyingine muhimu za chama.
Ndani ya Laptop hiyo kulikuwepo na MPANGO MKAKATI WA CHAMA TAIFA 2013/2015 kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao WA 2015.

Same source.
 
Nini tatizo lililosababisha wajiuzulu!? Au ni mwendelezo wa kuvua gamba umeikumba hadi ccm B?
 
Tukio hili limetokea sambamba na Naibu Katibu Mkuu Bara MHE. Julius Mtatiro akiwa safarini kikazi mkoani Arusha kupoteza Laptop na nyaraka nyingine muhimu za chama.
Ndani ya Laptop hiyo kulikuwepo na MPANGO MKAKATI WA CHAMA TAIFA 2013/2015 kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao WA 2015.
Yote 9, lakini la 10 huu utakuwa ama ni uzembe au hujuma. Itakuwaje nyaraka muhimu kama hizo zisiwekwe kwenye flash disk "just in case"? Kama sio kupotea kwa laptop, ingeweza kukumbwa na matatizo mengine na nyaraka hizo kupotea. Mwaka wa kufa nyani, miti yote huteleza.
 
Huku ni mwanzo wa kufa kwa chama cha wananchi CUF? Au kuna usanii unaendelea hapo? jamani Bazazi! haelewi iwapo kuna mpangokazi wa kuihuisha CUF kwa viongozi waliopo sasa kwa kukosa mvuto wajiuzulu kuwapisha wengine au ndio njia moja ya makaburini (Kama ni makaburini kiwasalimie PONA, CCJ, nk).

Bazazi ni Bazazi
 
Pole kwa CUF! naamini hizo nyaraka muhimu hakuwanazo pekee yake kwahiyo anaweza kuzi-access kwa mwenyekiti taifa (kwa mfano).
 
Hawa viongozi wa kuamka hawa acha wamalizike .KAFU ina dhambi kubwa mno kama Mrema .Waliwapa watanzania matumaini lakini wameishia kuamsha sasa.Laana tuulah
 
Yawezekana wamehamia UAMSHO na Greace M4C maana yupo peke yake na Ukitaka kuijua Cuf angalia safu ya viongozi wake
 
Back
Top Bottom