Pierluigi collina

Achraf Hakimi

JF-Expert Member
Mar 3, 2010
875
1,779
Collina alikuwa ni mwamuzi wa kiitaliano anayechukuliwa na wadau wa soka duniani kama muamuzi bora aliyewahi kutokea. Nguli huyu alikuwa ni mwamuzi mwenye haiba na mwenye kuogopwa na wachezaji anapokuwa uwanjani. Lakini pia alikua ni mwamuzi ambaye timu nyingi zilifurahia kupangiwa achezeshe michezo yao kwani uamuzi wake mara nyingi haukuwa na makosa. Collina alizaliwa tarehe 13 Februari 1960 mjini Bologna na kupata elimu yake ya chuo kikuu katika mji huo huo akipata shahada ya uchumi mnamo mwaka 1984, Kabla ya kupata shahada yake alihudhuria mafunzo madogo ya uamuzi mwaka 1977 na hapo ndipo alipoanza kugundua uwezo wake katika fani hiyo. Baada ya miaka mitatu Collina alijikuta akichezesha mechi kubwa zaidi katika jimbo lake huku wakati huo huo akimalizia mafunzo ya lazima ya jeshi, mwaka 1988 alichaguliwa kuwa mwamuzi katika ligi daraja la tatu nchini Italia yani serie C1 na serie C2, baada ya misimu mitatu alipanda daraja na kuwa mwamuzi wa ligi daraja la pili yani serie B na baadaye kidogo akapandishwa kuchezesha serie A. Kuna kipindi aliugua ugonjwa fulani uitwao alopecia uliosababisha apoteze nywele zake zote na hivyo watu wake wa karibu kumpa jina la utani la “kojak”. Mnamo mwaka 1995 baada ya kuwa mwamuzi katika mechi 43 za ligi kuu ya Italia aliwekwa katika orodha ya waamuzi wa FIFA. Alichaguliwa kuwa muamuzi katika mechi tano za mashindano ya Olimpiki ya mwaka 1996 ikiwemo mechi ya fainali kati ya Nigeria na Argentina. Alikuwa mwamuzi katika mechi ya Fainali ya kombe la mabingwa barani ulaya mwaka 1999 kati ya Bayern Munich na Manchester United. Collina anachukulia mechi hii kama mechi anayoikumbuka zaidi katika historia yake sababu ya sauti za washabiki mara baada ya mechi kwisha zilikuwa kama muungurumo wa simba. Mwaka 2002 ulikuwa ni mwaka wa kukumbukwa katika maisha yake ya uamuzi kwani alichaguliwa kuwa muamuzi wa mchezo wa fainali ya kombe la dunia kati ya Brazil na Ujerumani. Kabla ya mchezo nahodha wa timu ya Ujerumani alisikika akiwaambia wandishi wa habari wa Ireland.com kuwa “Collina ni muamuzi wa kimataifa lakini huwa analeta bahati?”. alisema hivi sababu katika mechi mbili ambazo Kahn alikuwepo huku Collina akiwa muamuzi yani mechi ya fainali kombe la mabingwa ulaya 1999 na mechi kati ya Ujerumani na Uingereza mwaka 2001 ambapo ujerumani ilifungwa 5-1.hata hivyo bahati ya Kahn haikubadilika katika fainali hiyo. Mwaka 2003 Collina alichapisha kitabu cha historia yake kilichoitwa kwa Kiingereza “The rules of the game”. Mchezo wake wa mwisho kimataifa ulikuwa ni wa fainali ya kombe la UEFA mwaka 2004 kati ya Valencia na Olympique Marseille kwani alifikisha umri wa miaka 45 na hivyo alitakiwa kustaafu kwa sheria za waamuzi wa FIFA. Hata hivyo Chama cha soka nchini italia kiliongeza umri wa kustaafu kwa waamuzi hadi miaka 46 ili kumuongeze a Collina mwaka mmoja zaidi, ila kulitokea msuguano kati ya Collina na chama cha soka nchini Italia baada ya Collina kusaini mkataba wa kibishara na kampuni ya Opel mkataba huu ulionekana kama ugesababisha upendeleo kwa timu ya AC Milan ambao walikuwa wakidhaminiwa na kampuni hiyo hiyo ya Opel na hivyo Collina alilazimika kujiuzulu na hivyo kuacha rasmi uamuzi wa soka. Baada ya maisha yake ya Uamuzi Collina amekuwa akijishughulisha na masuala ya kibiashara kwani sura yake imetumika katika matangazo kadhaa kama matangazo ya adidas na Mastercard katika kombe la Dunia 2006 pamoja na michezo ya video ya Pro Evolution Soccer 3 na Pro Evolution Soccer 4. Ingawa Collina anatambulika sana katika ulimwengu wa soka, timu ya michezo aipendayo ni timu ya mpira wa kikapu ya Fortitudo Bologna ambayo amekuwa mshabiki wake wa muda mrefu. Collina anaishi katika mji wa Viarregio na mke wa kiitaliano aitwae Gianna na watoto wawili na mbwa wao aitwae Wallace. Kwa sasa Collina na Kampuni yake ya kutoa ushauri wa kibiashara.
 
alipata kunena haya ''SIJAWAHI KTK MAISHA YANGU KUJIHUSISHA NA UTATA WOWOTE JUU YA MAGOLI ANAYOYAFUNGA PIPO INZAGHI...MARA ZOTE NIMEKUWA NIKIWAACHIA MAAMUZI HAYO LINE MEN AMBAO NDIO MAADUI WAKUBWA WA PIPO ''
 
swali:
Je Colina ktk mechi moja unaweza kutoa maamuzi ya penati ngapi?

jibu:
Hata penati 50 naweza kuzitoa kama zitakuwa za halali.
 
Nakumbuka nilimuona akichezesha mechi ya fainali ya Olimpiki 1996 Nigeria vs Argentina, aliwapa pelnati isiyo ya halali Argentina baada ya mchezaji wao kujiangusha kwenye box, halafu baadaye akakubali Goli la Kanu ambaye alikuwa amezidi (kwa offside rule za muda ule).

Baada ya hapo sikuwahi kuona significant controversial decision kutoka kwake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom