Pichani, Daraja Kigamboni hiloo... Kigamboni yakufikirika yawa kweli

Kuna michakato ya kila aina si ya kujenga daraja tu, ipo kwenye makaratasi na ndoto za mchana, kabla wewe na mimi hatujakuwepo, Jee, tuipongeze kwa kuwa ipo kwenye ndoto zao au tumpongeze aliyeifanya ikawa kweli na si ndoto tu? Fikiri.

Kikwete anafanya kweli.
Kiuwekezaji haihitaji pongezi maana mashirika yanayotafuta kukamua wananchi ni mengi ila kama angefanya kweli kwakutumia rasilimali zetu wenyewe (gas, gold, uranium nk) hakika tungempongeza.
 
Kiuwekezaji haihitaji pongezi maana mashirika yanayotafuta kukamua wananchi ni mengi ila kama angefanya kweli kwakutumia rasilimali zetu wenyewe (gas, gold, uranium nk) hakika tungempongeza.

Hizo Gas, Gold na Uranium bila jitihada yake ungezisikia jina tu. Kikwete anafanya kweli.
 
Idea ya kujenga hili daraja aliitowa babu yake babu yangu mwaka 1919 na ramani alichora. Mchoro wa kwanza ulikuwa ni wake lakini alichora itumike mianzi na udongo wa mfinyazi uliochanganywa na mayai ya kuku wa kienyeji kuufanya ukamatane vizuri na kuwa "salt water proof". Bahati mbaya ikaonekana kuku wanaoweza kutoa aina ya mayai yanayofaa kwa kazi hiyo wanapatikana Iguguno tu huko Singida na itachukuwa miaka 35 kupata kuku na mayai ya kutosha. Kwa hayo plan yake ikarudishwa kwa maboresho na re-design. Zikabaki ndoto na mawazo ya kila aina na kila watu mpaka hapa tulipofikia.

Michoro ya daraja la sasa na upembuzi yakinifu imeanza mwaka 2007 na kumalizika 2010. Na Jakaya Mrisho Kikwete kwa kushauriana na Dokta Ramadhan Dau wameweza kutimiza ndoto za muda mrefu na kazi imeanza kwa kasi zaidi kama picha zinavyoshuhudisha.

Vizuri mdau kwa taarifa kuhusu upembuzi yakinifu kitu ninachoaamini kila kitu kinawezekana kama utaamua na kuweka plan na design ya kitu in advance kabla ya kutafuta hela hata kama utekelezaji utafanyika baada ya miaka 30 kwani plan na design ndio inakuwa base ya nini kifanyike ili daraja lijengwe na ndio maana nilikuwa napinga sana hii issue ya power tiller nikiwa nina maana tumeji-under rate kwa kuweka minimum standard ambazo sio kumbe kama tungejipanga tungeweza kuweka at least kila wilaya trekta kadhaa na baada ya miaka kadhaa tuwe na trekta kadhaa. Otherwise nipo poa na nimefurahi hii kitu kuendelea kujengwa maana ilikuwa ni hadithi ya muda mrefu na ilionekana kama haiwezekani.
 
Naomba niwajulishe , hicho kidaraja mnachokiona, kimejengwa temporary tu, kwa kuwawezesha hao jamaa kwenda na kurudi kwa muda, daraja lenyewe mtaliona au mmeshaona picha zake, acheni kukashif, mtu akifanya mambo mazuri msifieni, hata kama ni pesa yenu / yetu ya NSSF kuna pesa ngapi zilikuwa enzi za tawala zilizopita na mbona hatukuwahi kuona majambo kama ya sasa? hongera Dr Dau, hongera kikwete, ari na kasi yako tumiona, ila tafadhali usituhamishe kigamboni mpaka umetuwekea mazingira mazuri ya kutulipa haki zetu
 
Mimi ni mmojawapo ambaye sikupenda kupata kiwanja cha kujenga Kigamboni sababu ya tatizo la kusubiria ferry. Leo ninapoona hili daraja naanza kubadili mtazamo wa kuona Kigamboni si kisiwani tena. Mwenye kiwanja cha Ekari moja mpaka mbili nipm, niko tayari kwa gharama yo yote kwani sasa naona Kigamboni yawa kama :A S 465:Long Island beach ya NY.:A S 465:

Hata nikipata pale Vijibweni sawa tu, maana huko karibu na beach kabisa nako mawimbi ya bahari yakitikisika kwa kishindo cha tetemeko balaa kufunikwa na maji ya chumvi.

Wewe nawe! mbona viwanja vya serikali vipo vingi sana unahangaika na viwanja ambavo havijapimwa? kiwanja cha eka moja au mbili ni wazi kitakuwa hakijapimwa, na huu mradi uwe muangalifu wa kununua ardhi hovyo kigamboni au sivyo itakula kwako! nenda gezaulole kuna viwanja bwelele !
 
Hizo Gas, Gold na Uranium bila jitihada yake ungezisikia jina tu. Kikwete anafanya kweli.
Hata hivyo vyote vilivyotajwa tunavisikia majina tu, labda wewe ni mmoja wa wale wenye ile kampuni ilinayotuhumiwa pale Mwanza, kama ni hivyo wewe husikii tu kama sisi utakuwa navyo kwako!.
 
Ntaendelea kutumia kivuko! huko kurasini ni kuongezeana kilometres tu watu tulishazoea dk 2 tuko magogoni
 
Hata hivyo vyote vilivyotajwa tunavisikia majina tu, labda wewe ni mmoja wa wale wenye ile kampuni ilinayotuhumiwa pale Mwanza, kama ni hivyo wewe husikii tu kama sisi utakuwa navyo kwako!.
kaka kuna watu wa ajabu sana tz.namkumbuka sana meya wa jiji la dar.
 
Naomba niwajulishe , hicho kidaraja mnachokiona, kimejengwa temporary tu, kwa kuwawezesha hao jamaa kwenda na kurudi kwa muda, daraja lenyewe mtaliona au mmeshaona picha zake, acheni kukashif, mtu akifanya mambo mazuri msifieni, hata kama ni pesa yenu / yetu ya NSSF kuna pesa ngapi zilikuwa enzi za tawala zilizopita na mbona hatukuwahi kuona majambo kama ya sasa? hongera Dr Dau, hongera kikwete, ari na kasi yako tumiona, ila tafadhali usituhamishe kigamboni mpaka umetuwekea mazingira mazuri ya kutulipa haki zetu
unasifia huku unaomba msamaha miradi kama hii mara nyingi huwa na matokeo mabaya kwa raia je kama ni kweli linajengwa halafu litahitaji kumlipa mwekezaji kwa kipindi kirefu tija itakuwa wapi?halafu kutumia hela za nssf bila matakwa ya wenye hela yao si sahihi sifa lazima ziwe stahiki.
 
Hivi baada ya daraja kukamilika wamesema litatoa nafasi ngapi za ajira vile! nimesahau nikumbusheni jamani.
 
Vizuri mdau kwa taarifa kuhusu upembuzi yakinifu kitu ninachoaamini kila kitu kinawezekana kama utaamua na kuweka plan na design ya kitu in advance kabla ya kutafuta hela hata kama utekelezaji utafanyika baada ya miaka 30 kwani plan na design ndio inakuwa base ya nini kifanyike ili daraja lijengwe na ndio maana nilikuwa napinga sana hii issue ya power tiller nikiwa nina maana tumeji-under rate kwa kuweka minimum standard ambazo sio kumbe kama tungejipanga tungeweza kuweka at least kila wilaya trekta kadhaa na baada ya miaka kadhaa tuwe na trekta kadhaa. Otherwise nipo poa na nimefurahi hii kitu kuendelea kujengwa maana ilikuwa ni hadithi ya muda mrefu na ilionekana kama haiwezekani.

Power tiller zina sehemu yake na Tractor zina sehemu yake SUMA JKT wanakupa mafunzo, ukiwapa data kamili za unapotaka kutumia na wanakushauri ni aina ipi ya zana uitumie hapo. Si kila kilimo unaweza kutumia power tiller na si kila kilimo ni lazima utumie tractor kubwa.

Daraja la mianzi na udongo wa mfinyanzi kwa mayai ya kuku wa kienyeji lilishindikana kwa kuwa tu, kuku na mayai stahiki yalikuwa hayapatikani, Teknolojia ya miaka 30 au mia nyuma siyo ya leo na wala haitakuwa ya miaka 30 au 100 ijayo.

Leo mnahangaika na vidaraja, miaka 100 ijayo, unapanda gari lako, ukikuta bahari unaingia nalo linakuwa boat, au unavaa jet pack yako mgongoni, daraja litabaki kuwa makumbusho. Taaluma zinaendelea na hazina mwisho, mimi na wewe tuna mwisho.

Idea zinawezza kuwa nzuri kwenye maneno na zikawa tatizo kwenye kuetekeleza kama vile idea ya Nyerere ya Ujamaa na Kujitegemea, tuliokuwepo siku hizo sote tuliona hiki ni kitu kizuri sana na ndicho kitakachotufaa, lakini hakikuweza kutekelezeka na ikawa big failure ingawa tukishindana mimi na wewe sasa hivi naweza kukuaminisha kuwa hakuna mfumo bora kama huo, lakini ni kwa doctrine nilizojazwa enzi hizo kabla ya kuona mifumo mingine.

Mimi nna idea ya kuruka bila mashine, wengine wanaitekeleza, nasikia wanaruka kwa ungo, Jee, ni idea nzuri hiyo au mbaya?
 
unasifia huku unaomba msamaha miradi kama hii mara nyingi huwa na matokeo mabaya kwa raia je kama ni kweli linajengwa halafu litahitaji kumlipa mwekezaji kwa kipindi kirefu tija itakuwa wapi?halafu kutumia hela za nssf bila matakwa ya wenye hela yao si sahihi sifa lazima ziwe stahiki.

Ulienda kudai hela yako NSSF ukanyimwa?

Unafikiri fedha inayokaa NSSF ikikaa tu bila kufanyiwa kazi itazaa na kukupa faida?
 
Hata hivyo vyote vilivyotajwa tunavisikia majina tu, labda wewe ni mmoja wa wale wenye ile kampuni ilinayotuhumiwa pale Mwanza, kama ni hivyo wewe husikii tu kama sisi utakuwa navyo kwako!.

Hapana mimi sina hisa kwenye mgodi wowote wa dhahabu. Mimi nanuwa dhahabu za kuwavalisha wake zangu, sina kazi nazo zaidi ya hapo.

Kama unataka dhahabu si uende ukachimbe, unashindwa nini? kuna mtu aliyekuzuwia? au hujui kuna watanzania wengi wanachimba kila aina ya vito, tazama wenzako, hawaandikii mate, wanafanya kweli:

Wachimbaji%2Bwadogo%2Bkijiji%2Bcha%2BNgasamo.jpg
Wachimbaji wadogo wakikusanya vifusi vya mawe yaliyo na dhahabu...

Wachimbaji%2Bwadogo%2Bkijiji%2Bcha%2BNgasamo%2B12.jpg

Huku akiwa ameshikilia kipande cha dhahabu mdau mwananchi wa kawaida anaronga.... "Mimi ndiyo 'taita' wa mgodi huu"

Source: WACHIMBAJI WADOGO NGASAMO WILAYANI

Back
Top Bottom