Pichani, Daraja Kigamboni hiloo... Kigamboni yakufikirika yawa kweli

Swali langu ni vipi meli zenye urefu mkubwa zitapita?

Zamani tuliwahi ambiwa kuwa daraja litakuwa la kufunga na kufungua mara hadithi ikawa litakuwa kimo kirefu(Height) sana kutoka usawa wa bahari kuliko urefu wa meli yoyote duniani!

Bahati mbaya sana kwenye hivyo vielelezo vya picha sioni dalili za kimo kirefu(Height) au mwelekeo wa kufunga na kufunguka.

8E9U4243.JPG


Concrete
Tazama vizuri picha hii sehemu ambayo Kikwete alienda kuweka jiwe la msingi ujenzi wa daraja hilo.

Kama waifahamu vizuri Dar es Salaam, basi huenda wajua pia Makao ya Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania. Ukuta unaouona ni sehemu ya uzio wa TEC, off Mandela Road karibu na warehouse za Malawi Bandarini.

Sehemu hiyo kunakoishia bandari kuu ya Dar es Salaam kuna sehemu ya wavushaji kwa mitumwi kwenda ng'ambo ya pili maeneo yanayojulikana kama Vijibweni.

Hivyo
Concrete daraja hilo halijengwi pale magogoni MV Kigamboni inakovusha watu ambako ni mlango wa Meli kuingia bandarini, la hasha, bali ni huku juu kabisa.

Kukurahizishia, toka uwanja wa Taifa fuata barabara ya Mandela, kabla hujavuka kwenda shimo la Udongo, utaona kulia kwako kuna Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania, ni hapo kabla ya block ya TEC ndipo inapoanza barabara iendayo kunakojengwa daraja jipya. Nadhani kwa maelezo haya unaweza kupata picha wapi daraja limejenga katika makutano ya mkondo wa bahari na Mto Kizinga.

Daraja la kufunguka na kujifunga kwa ajili ya kupisha meli kwetu ni bado, kufanya hivyo tunaweza kuhatarisha usalama wa wasafiri wa magari, miguu, na hatari kwa meli ziingiazo na zitokazo, mbona hili zinazopita free kuingia na kutoka misiba haiishi kila mwaka?
 
haya mavitu yanayojengwa mujue kabisa kama wewe ni masikini wenzio ndo wanasonga hivyo, kwa hiyo

kuwa masikini katika nchi yenye magorofa na mabridge makukuukuu na mabarabara ya RBT na flayover usishangae ndo mnapoitwa kuvaa tisheti zxa kijani mjue kabisa
 
Back
Top Bottom