Picha. . . .

Ndoa ikivunjika wakati wahusika wana watoto ni vema picha zote ziwekwe salama kwa ajili ya kumbukumbu kwa watoto. Mfano mimi na ndugu zangu hakuna picha tunazoibiana kama picha za wazazi wetu.

Ila kama ni urafiki wa kawaida; hizo picha ni za kuchoma moto, zinaweza leta ugomvi katika new relationship.
 
Hii kitu picha imesababisha hofu kubwa sana kwa mke wa jamaa yangu. Mke wa jamaa yangu aliikuta picha ya mpenzi wa mumewe aliyepiga naye kabla hajamuowa, lakini kibaya zaidi huyo mpenzi wake mke wake anamfahamu na alifariki kwa ukimwi na mke wa jamaa yangu anajua hivyo, lakini sio kwamba alikuwa na ukimwi wakati wakiwa wapenzi na jamaa yangu. Sasa mke hakuamini kama wako salama, pamoja na kwamba wameishi miaka 20 ndani ya ndoa na wana watoto 2, ilibidi awajulishe wanandugu wote na ikaamuliwa wakapime afya, ndiyo mke wake aliporidhika baada ya kukuta wapo safi. Cha ajabu ni picha ya miaka 20 iliyopita.

Well angalau wamepata uhakika kwamba wako salama.

Di'levis . . . Yeahh ugumu upo kwenye kumbukumbu zilizopo akilini.Ukishindwa kuondoa hizo hata ukichoma mpaka taulo aliloogea haitosaidia sana.
 
Mshiki kama wewe ndo umemuacha? inakuwaje hapa? maana najua mwenye kuachwa ndo anakua na maumivu

hahahaa Meku, hapa sasa ataamua mwenyewe, akiziweka haya, akizichoma sawa, akizipandika kadamnasi namshitaki....lol
 
Mimi nimeachana GF 3, lakini nguo, picha na baadhi ya vitu vyao ninazo! Siku nikikutana na mmoja wapo namkumbusha tu kuwa kuna mizigo yake aliiacha, basi anabaki anacheka/kulia tu. Wengine ndiyo hivyo tena anakuwa anataka turudiane.
 
Mimi nimeachana GF 3, lakini nguo, picha na baadhi ya vitu vyao ninazo! Siku nikikutana na mmoja wapo namkumbusha tu kuwa kuna mizigo yake aliiacha, basi anabaki anacheka/kulia tu. Wengine ndiyo hivyo tena anakuwa anataka turudiane.

Kwahiyo unaweka ili upate sababu ya kuwakumbusha zamani na kuwaliza wenzako?
 
Mi siku mama alikua anapika makande nikampa
akageuza kuni makande yakaiva vizuri tu ,nilichanganya
pamaoja na kadi za mapenzi ili makande yaive nakulainika.
 
Picha zilichanwa na barua zilichomwa moto(enzi hizo hakukuwa na mobile phones ).zile zilizofaa kurudishw3a zilirudishwa kwa mwenyewe.
 
Kwenye mahusiano/ndoa watu hua wanapiga picha pamoja . . . kwaajili ya ukumbusho.

Kwa wale mlioko facebook mnajua siku hizi hizo picha haziishi kwenye album makabatini tu na ukutani ila mpaka mitandaoni unakuta mmoja ana picha kibao za mwenzake bila kusahau description za ohh huyu ndie. . baby wangu and so so.Nimeona mmoja kajaza kweli za girlfriend wake nikajikuta najiuliza kama siku wakiachana atazifutilia tu mbali au itakuaje.

Swali. . .je ikiwa mahusiano yatavunjika zile picha mlizopeana na kupiga pamoja zinatakiwa zifanyweje?Ni sahihi kuziweka tu?Zinatakiwa zitupwe/chanwe. . . kama jibu ni ndio je za harusi?Ni sahihi kweli kuharibu/tupa picha unayopenda kisa tu uliyeachana nae yumo?Na kama ukiweka kuna madhara?

matendo hukumbukwa kichwani..........uzifute au la lakini ubongo ndiye msema kweli..............
 
Lizzy binafsi if we are done we are done.....
I want nothing to remind me of you, kwanza ili iweje?

Ili ukumbuke B....yaani mtu mmeshare kitanda umsahau hivi hivi tu?

mi nadhani inategemea mmeachana katika mazingira gani....
 
Vitu vingi sana ukiwa binti unasema huwezi vumilia, lakini umri na experience hubadili mitazamo mingi sana hasa watoto wanapokuwa invollved.
I just wish u a happy love life.

Kongosha acheni kunitisha bana. . .
Semeni tu nikue niyaone manini???
 
Back
Top Bottom