Picha. . . .

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,806
59,285
Kwenye mahusiano/ndoa watu hua wanapiga picha pamoja . . . kwaajili ya ukumbusho.

Kwa wale mlioko facebook mnajua siku hizi hizo picha haziishi kwenye album makabatini tu na ukutani ila mpaka mitandaoni unakuta mmoja ana picha kibao za mwenzake bila kusahau description za ohh huyu ndie. . baby wangu and so so.Nimeona mmoja kajaza kweli za girlfriend wake nikajikuta najiuliza kama siku wakiachana atazifutilia tu mbali au itakuaje.

Swali. . .je ikiwa mahusiano yatavunjika zile picha mlizopeana na kupiga pamoja zinatakiwa zifanyweje?Ni sahihi kuziweka tu?Zinatakiwa zitupwe/chanwe. . . kama jibu ni ndio je za harusi?Ni sahihi kweli kuharibu/tupa picha unayopenda kisa tu uliyeachana nae yumo?Na kama ukiweka kuna madhara?
 
nyumbani kwangu nina sanduku maalum linakaa darini,humo nimejaza bad memories zote,siku nikipigwa chepe watakaobaki duniani watajua wenyewe nini walifanyie.Ila hata mimi huwa najiuliza hao mahawara ambao tuki differ huwa tunatelekeza huko nguo (mpaka za ndani) baadae huwa wanazifanyia nini?
 
Mkibwagana unachana chana na kuzifuta zote hata line za simu unavunja vunja hata simu yenyewe unaanza upya.
 
Hahahaha. . . Bishanga umenichekesha na hilo la nguo mpaka za ndani. Wengine wanaweza kuweka kumbukumbu kama bado anakupenda . . wengine wakadekia au mwagia mafuta ya taa na kuchomelea mbali.

Ila sasa wewe hiyo collection yako unaiweka kwa madhumuni gani haswa?Kumbukumbu?
 
Yani mpaka simu ubadili kisa break-up?
Kwanini haswa?Wakati unaweza kufuta tu namba na kuendelea?
 
Kila kitu hata nguo alizo ninunulia nazichoma moto sitaki kabisa kukumbuka tuliko toka yaani naanza upya kabisa nateketeza kila kitu
 
Lizzy binafsi if we are done we are done.....
I want nothing to remind me of you, kwanza ili iweje?
 
Hahahaha. . . Bishanga umenichekesha na hilo la nguo mpaka za ndani. Wengine wanaweza kuweka kumbukumbu kama bado anakupenda . . wengine wakadekia au mwagia mafuta ya taa na kuchomelea mbali.

Ila sasa wewe hiyo collection yako unaiweka kwa madhumuni gani haswa?Kumbukumbu?
Honest sina jibu,ila ukweli ndo huo,situpi ila nazidi ku pile up,picha,zawadi,nguo,vidani,shanga,hirizi nilizokuta chini ya godoro, yaani we acha tu,ni sanduku kubwa.
 
Aaaah wapi mi huwa siruhusu kitu kama hicho mkataba ukikatika basi nahama mpaka mtaa ili kupunguza bugudha
iko siku utakutana na mwanaume wa shoka,kila mki break he will need only one phone call unamrudia mbio,,si unajua kila shetani na mbuyu wake?
 
mamkwe hii imenikumbusha rafiki yangu aligombana na BF wake ikafika kuamua kuchanachana picha zao nyingi pamoja na za kuvalishana pete nilichofanya nilimnyang'anya nikahifadhi waliporudiana alifunga safari kuja kuniomba nimrudishie tena na nilifanya hivyo mpaka leo wameoana na zile picha wanazo.
:focus:hakuna haja ya kuendelea kuzihifadhi kama uwezekano wa kurudiana haupo. unakuwa na mahusiano na mtu mwingine unapoendelea kuhifadhi picha hizo inaweza kuwa moja ya kusababisha ugomvi
 
Ni bora kuzi delete kama zipo kwenye sim, lakini kama ni za kwenye album naziondoa na kuziweka tu kwenye bahasha namtumia. Ataenda kufanya uamuzi yeye wa chochote anachotaka kuzifanyia.
 
Kila kitu hata nguo alizo ninunulia nazichoma moto sitaki kabisa kukumbuka tuliko toka yaani naanza upya kabisa nateketeza kila kitu

Aisee. . .
Hehehehe we ni noma.
Sasa kama alikununulia vingi si kabati litabaki empty?
 
Honest sina jibu,ila ukweli ndo huo,situpi ila nazidi ku pile up,picha,zawadi,nguo,vidani,shanga,hirizi nilizokuta chini ya godoro, yaani we acha tu,ni sanduku kubwa.

hahahaaaa hilo sanduku kuna siku utalikuta limeshuka lenywe darini....
 
Honest sina jibu,ila ukweli ndo huo,situpi ila nazidi ku pile up,picha,zawadi,nguo,vidani,shanga,hirizi nilizokuta chini ya godoro, yaani we acha tu,ni sanduku kubwa.
Bishanga siku ukifa utaacha mzozo duniani lol!
 
Lizzy binafsi if we are done we are done.....
I want nothing to remind me of you, kwanza ili iweje?

Bht nafikiria kama ni picha uzipendazo sana sababu ya kumbukumbu binafsi au hata na ndugu/marafiki zako?

Hehehe au watu wawe wanamchana mhusika?Nimewahi kuona hii mahali.Na kama ni digital unam-crop.
 
mi nilizichana,nikazichoma moto,majivu nikayafunga kwenye kitambaa kichafu,nikatupa porini!
 
Back
Top Bottom