mungu yupo hawataki kumtii
wanagomba ARDHI YA MUNGU NA WANAIACHA HAPAHAPA
SASA WANAWATAABISHA WATOTO KAMA HAWA
WASIO NA HATIA JAMANII INASIKITISHA SANA
HIVI KWANINI WANAWAZAA WATOTO HAWA
NA WANAPATA WAPI MUDA HUU WA KUWATENGENEZA
KWANINI WASITUMIE MUDA HUO KUJENGA NJI YAO KWANZA
AAAH SASA WATOTO HAWA WANAZALIWA
WANATESEKA NA HAWAFIKI POPOTE
WANAIACHA DUNIA HII TENA HATA HAWANA KOSA
AAAAH INAUMA SANA
That is the fact, tushukuru MUNGU kwa kila jambothat is what is called ecosystem. wala hamna la kutisha mbele za mola. omba na kushukuru u may the next component
Ndugu yangu huyo Mungu aliyewanyima hawa ndo kakupa wewe. Tena usisema kabisa, maana laiti ungejua namna ambavyo Mungu alivyo na sera kama za marekani wala usingekaa chini ujivune hivyo kwa kuwa Mungu kakupa wewe mvua. Mungu hana rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu. Leo amekupa wewe mvua, lakini kesho atakunyima, hela utakuwa nayo lakini haitakuwa na uwezo wa kununua chakula kwa kuwa hakitakuwepo. Tuwaombee rehema hawa wenzetu. hawakupenda yawakute hayo. Laiti mvua ingenyesha halafu wakashindwa kulima, tungewalaumu lakini hawana mvua, wafanyaje kuikabili hiyo changamoto. Au watengeneze mvua zao?mungu yupo hawataki kumtii
wanagomba ARDHI YA MUNGU NA WANAIACHA HAPAHAPA
SASA WANAWATAABISHA WATOTO KAMA HAWA
WASIO NA HATIA JAMANII INASIKITISHA SANA
HIVI KWANINI WANAWAZAA WATOTO HAWA
NA WANAPATA WAPI MUDA HUU WA KUWATENGENEZA
KWANINI WASITUMIE MUDA HUO KUJENGA NJI YAO KWANZA
AAAH SASA WATOTO HAWA WANAZALIWA
WANATESEKA NA HAWAFIKI POPOTE
WANAIACHA DUNIA HII TENA HATA HAWANA KOSA
AAAAH INAUMA SANA
Asante kwaposting yako hii dada Judith, umenikumbusha mbaali. Mara zote wanaojificha kwenye vikundi vya kidini vyenye "Msimamo mkali" ni magenge ya wahuni, wezi, vibaka wenye malengo binafsi zaidi kuliko hizo dini wanazodai wanazipigania. El Shabaab kama ilivyo Al Qaeda ni wanafiki na wahalifu wanaostahili kupigwa vita hata na waislamu wenyewe kwa vitendo vyao wanaiaibisha jamii ya kiislamu. Hebu angalia wanavyoua waislamu wenzao bila huruma kinyume kabisa na mafundisho ya uislamu. Wanalipua mabomu ovyo yenye kuwaua waislamu na wasio waislamu, watoto na kinamama wakiwemo wajawazito! Wamesababisha wakimbizi wa ndani na nje ya nchi nakusababisha maafa makubwa ya magonjwa na njaa na mateso yasiyosemekana. Ni kweli Afrika inahitaji mtu shupavu mwenye moyo wa kuthubutu kuidhibiti hali ya Somalia kama JKN (RIP). Naafikiana nawe kabisa kwamba bila ya "Intervention" yake Uganda ya leo ingekuwa kama Somalia. Pamoja na mapungufu yake namheshimu sana Museveni kwa maamuzi yake ya kijasiri yanayoendelea kuipa nchi yake heshima. Tatizo la Somalia lingekuwa limebaki katika vitabu vya Historia kama viongozi wetu wa sasa wangekuwa wakweli na majasiri wa kuchukua hatua. Hebu tujiulize, kama mchango wa nchi mbili tu za Uganda na Burundi zimeweza kuwa "Check" wahuni hawa wa Al Shabaab ingekuwaje kama nchi zipatazo kumi na tano zingejitoa kwa dhati kupambana na kuwadhibiti wahuni hawa?wapendwa simanzi imeuvuja moyo wangu! kwa kuangalia picha hizo nimejisikia kama nakunywa siki! ni nguu sana kuangalia mara mbili! ooh Lord have mercy on your somali people!
matatizo ya somalia yanachangiwa (pamoja na sababu nyingine) na ukame na ukosefu wa amani na usalama. kama nchi jirani ya uganda isingekombolewa kutoka mikononi mwa nduli idd amin, basi nao hali isingekuwa tofauti na somalia ya hivi leo kwani mazingira ya kuwepo vikundi vingi vya waasi vinavyogombea madaraka (kwa wakati huo) ilikuwa sawa na somalia ya sasa. thanks to the late mwalimu nyerere (and TPDF) kuingilia kati hali ya kisiasa huko uganda na kuhakikisha mzizi wake (amini) umeng'oka kabisa na leo waganda wanamtaja daima kama mmoja wa mashujaa wao asiyesahaulika japo hakuwa mganda! pia rais wa sasa museveni anastahili kila la pongezi kwa kumaliza hali ya vikundi vya waasi ambavyo kwa kweli obote licha ya sapoti ya muda mrefu toka kwa mwalimu na OAU alishindwa kuvishughulikia ipasavyo.
likewise, naamini kabisa kama AU ingekuwa na kiongozi mwenye moyo wa uthubutu kama JKN (RIP) somalia ingeishakombolewa siku nyingi kutoka mikononi mwa magaidi waliojificha nyuma ya vikundi vya wanaharakati wa kiislamu.
ooh, Mwenyezi Mungu mwenye upendo na huruma, waangalie watoto wako wa somalia kwa jicho la rehema, ukawapunguzie shida zao na kuiponya nchi yao, amina