Picha: Ziara ya Nape mkoani Kilimanjaro

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Sunday, October 21, 2012


Nape Nnauye, Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi akiweka jiwe la msingi katika ofisi mpya ya CCM ,Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro tarehe 20/10/2012
Wananchi wa kata ya Nanjara Reha wakimpokea Katibu wa NEC ,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye, tayari kwa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM kwa kiti cha Udiwani.
Wanachama wakongwe wa chama cha mapinduzi wakionyesha kukubaliana na hotuba ya Katibu wa NEC,itikadi na Uenezi, Nape Moses Nnauye alipowahutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni za Diwani wa Kata ya Nanjara Reha, Rombo ,mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya Madiwani wakiwa kwenye picha ya pamoja, Madiwani hawa ni kati ya Madiwani 21 ambao kwa pamoja wataweka nguvu zao kuhakikisha kata ya Nanjara Reha inarudi CCM. PICHA ZOTE NA ADAM MZEE




POSTED BY: BASHIR NKOROMO AT SUNDAY, OCTOBER 21, 2012

 
Hatuwezi kulikomboa taifa hili bila kuwabadilisha wanawake kwani inaonekana washabiki wakubwa wa CCM ni akina mama na wasichana kama picha zinavyojionyesha.
 

Adui wa mtanzania ni mtanzania mwenyewe,ebu ona hapo barabara ni ya vumbi lakini wamekubali kuwa hawastahili barabara ya lami.Chini ya uongozi wa chama toka uhuru.Ujinga ni kitu kibaya sana.
 
Gud sana,hii ni ishara ya kukubalika kwa ccm huko kilimanjaro hasa nyumbani kwa mbunge wa rombo
 
We kibogo tutake radhi mabinti,labda wale wanaongojea vitanda maalum.

Hapana huwezi niambia niwatake radhi ninachozungumzia ni uharisia kama picha zinavyojieleza pia fuatilia mkutano wa CCM jangwani asilimia kubwa walikuwa ni akina dada na akina mama, mi ushauri wangu kwako kama umekubaliana na vuguvugu la mabadiriko jitahidi kutoa elimu kwa mabinti wenzio unaoona bado hawajahamasika na kwa pamoja tutajikomboa toka kwa mkoloni mweusi CCM.
 
eti wanachama wakongwe.....kama huo ndio mtaji wa ccm kuelekea 2015 basi ccm kwa heri,
 
Watu wa Kilimanjaro naomba wamhoji nape anazisemeaje kauli zake hatari za kibaguzi zenye misingi ya ukanda na ukabila. aliwahi kusema chadema ni chama cha wachaga.

Sasa aulizwe ana kauli gani kuhusu sera zake hizo za kuwabagua wachaga. Ni lazima abanwe. anawaambiaje wachaga walioko CCM? Je wamefanya makosa kuwa CCM?
 
hawa wanawake ni kikwazo katika kuleta ukombozi coz bado hawajazinduka licha ya wao kuwa wahanga wa umaskini unaofugwa na ccm.
 
Back
Top Bottom