Picha za Watu Sita Waliopandishwa Kizimbani Mjini Singida,Kujibu Shitaka la Mauaji ya Mwenyekiti UV-

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Tuesday, July 17, 2012


[h=1]
Picha za Watu Sita Waliopandishwa Kizimbani Mjini Singida,Kujibu Shitaka la Mauaji ya Mwenyekiti UV-CCM Kata ya Ndago Wilaya Iramba,Yohana Mpinga na Afisa Sera na Utafiti wa CHADEMA Makao Makuu Waitara Mwita Aachiwa Kwa Dhamana
[/h]

Afisa+sera+na+utafiti+CHADEMA+Makao+makuu,+Waitara+Mwita+akifurahi+na+wanachama+wa+CHADEMA,+baada+ya+kupata+dhamana+mjini+Singi.jpg

Afisa sera na utafiti CHADEMA Makao makuu, Waitara Mwita akifurahi na wanachama wa CHADEMA, baada ya kupata dhamana mjini Singinda
Mwita+Waitara+akizungumza+na+wanahabari+mjini+Singida+baada+ya+kuwekewa+dhamana+ya+wadhamini+wawili+kila+mmoja+mwenye+ahadi+ya.jpg

Mwita Waitara akizungumza na wanahabari mjini Singida baada ya kuwekewa dhamana ya wadhamini wawili
Mwita+Waita+%28wa+kwanza+kushoto%29,+akifurahi+na+wafuasi+wa+CHADEMA+mahakamani+mjini+Singida,+baada+ya+kupata+dhamana+ktk+kesi+ya.jpg

Mwita Waita (wa kwanza kushoto), akifurahi na wafuasi wa CHADEMA mahakamani mjini Singida, baada ya kupata dhamana ktk kesi ya mauaji.
VIJANA+sita,+Watuhumiwa+wa+mauaji+ya+Mwenyekiti+UVCCM+Yohana+Mpinga+wa+Kata+Ndago+Iramba+Singida,+wakipandishwa+kwenye+gari+la.jpg
VIJANA sita, Watuhumiwa wa mauaji ya Mwenyekiti UVCCM Yohana Mpinga wa Kata Ndago Iramba Singida, wakipandishwa kwenye gari la polisi.Picha na Habari na Elisante John
--


WATU sita wamepandishwa kizimbani Mjini Singida, kujibu shitaka la mauaji ya Mwenyekiti UV-CCM Kata ya Ndago Wilaya Iramba,Yohana Mpinga, katika vurugu zilizohusisha wafuasi wa CHADEMA na CCM.

Wamesomewa shitaka hilo na mwanasheria mwandamizi wa Serikali, Neema Mwanda mbele ya hakimu mfawidhi mahakama ya Mkoa Singida, Ruth Massam.


Walioshitakiwa ni Manase Daudi (40), Williamu Elia (33), Frank Stanley (20), Charles Leonard (36), Tito Nintwa na Fillipo Edward (30), wakazi wa Ndago, Wilaya Iramba.

Wamedaiwa kufanya kosa hilo Julai 14, 2012 saa kumi alasiri, katika kijiji cha Nguvumali, kwa kutumia mawe na fimbo.

Hawakutakiwa kujibu lolote, kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kusikiliza kesi hiyo na itatajwa tena Julai 30, 2012.

Pia kesi nyingine iliyosomwa na mwanasheria wa Serikali Seif Ahmad, imemhusisha afisa sera na utafiti wa CHADEMA makao makuu Waitara Mwita (37) mkazi wa jijini Dar-es-salaam, akidaiwa kutoa lugha ya matusi mkutanoni.

Waitara anadaiwa kutoa lugha hiyo ya matusi dhidi ya Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, Julai 14, 2012 saa kumi jioni katika kijiji cha Ndago, Wilaya Iramba Mkoani Singida. Yupo nje kwa dhamana ya wadhamini wawili kila mmoja mwenye Sh.800,000 na itatajwa tena Julai 30, 2012.


4.jpg

5996140674267894691-6970018085948223502





 
CCM kilichobaki ni kutumia nguvu za DOLA kugandamiza UPINZANI kwasababu wanaijia CCM kama KIMBUNGA

Sasa MWINGULU MCHEMBA yeye anasema anatishiwa kuuwawa BUNGENI, ni kwanini asipeleke Malalamiko yake POLISI?

Anaona akipeleka POLISI haitakuwa na UZITO kuliko kutangaza akiwa BUNGENI; Kila MTU anasikiliza kwahiyo UMAARUFU

Na ni baada ya Mwanachama wa CCM kuuwawa; Kwahiyo hadi Sasa hana RIPOTI YA POLISI? ILA RIPOTI YA BUNGE?
 
Watanzania tuwe wavumilivu mwisho wa maovu ya hawa mafisadi umekaribia sana 2015 ni karibu. Mauaji yataisha kwa ndugu zetu. Sidhani kwa hawa wageni wafanye fujo na kuua mwenyeji. Hizi ni njama za WanaCCM, kama alikerwa na Mkutano huo kwanini hakuondoka kimyakimya. Siku zake zilikuwa zimetimia na huu ndo mshahara wake asubiri hukumu yake kwa Mwenyezi Mungu.
 
dah!!ama kweli (waitara uliukwaa uenyekiti?hahahahaaaa ama kweli mshkaji noumer long time) ivi ile kesi ya mauaji ya yule mwenyekiti wa chadema arumeru!ivi walishikwa watuhumiwa na walifikishwa mahakamani? update plizz
 
hao vijana wenyewe wanaonekana njaa kali.badala ya kwenda kutafuta riziki halali wanatumika kama .......mu!!!!
 
Back
Top Bottom