Elections 2010 Picha za uzinduzi wa Kampeni ya CHADEMA

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Picha na maelezo kwa Hisani ya blog za Michuzi na Michuzi Jr:


18.JPG


Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dr. Willbrod Slaa akizungumza leo jioni wakati wa uzinduzi wa kampeni na ilani ya chama chao mbele ya maelfu ya watu waliofika kuushuhudia uzinduzi huo katika viwanja vya jangwani. Dr Slaa alisema kuwa akipewa ridhaa ya kuiongoza nchi hii basi atahakikisha ndani ya siku 100 za kwanza,katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafanyiwa marekebisho makubwa na pia kuhakikisha mfumo wa Elimu hapa nchini unabadilishwa kabisa.

6+mgombea+mwenza..JPG

Mgombea Mwenza wa Dr. Willbrod Slaa,Said Mzee akiwahutubia wanachama na wapenzi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliofika katika viwanja vya Jangwani leo.

9+mke+wa+dr.+slaa.JPG

Mgombea Urais wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr. Willbrod Slaa akimtambulisha rasmi mke wake mbele ya maelfu ya watu waliofika kwenye uzinduzi wa kampeni na ilani ya chama hicho jioni ya leo katika viwanja vya jangwani,jijini Dar.

8+makabidhiano.JPG

Mwenyeki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akikabidhi vitabu vya Ilani ya chama hicho kwa mgombea Urais wa chama hicho Mh Willbrod Slaa leo jioni katika viwanja vya Jangwani jijini Dar mara baada ya kuizindua.

19.JPG

Mwenyeki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akionesha vitabu vya Ilani ya chama chao mara baada kuizindua leo katika viwanja vya Jangwani,jijini Dar.

16.JPG

Muasisi wa vyama vingi nchini na Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mabere Marando ambaye pia amejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akionesha kitabu cha Ilani ya chama hicho mbele ya Wananchi waliofika katika viwanja vya jangwani leo.Marando aliongeza kwa kusema kuwa siku ya Jumatatu wataweka pingamizi kwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mh Dr. Jakaya Kikwete kwa kudaiwa kukiuka baadhi ya sheria za Uchaguzi.

15.JPG

Aliyekuwa Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha CCM,na baadae akahamia chama cha CHADEMA hivi karibuni,John Shibuda akizungumza mbele ya wananchi leo jioni wakati chama hicho kilipokuwa kikizindua kampeni na Ilani yake katika viwanja vya Jangwani na kuhudhuriwa na mamia ya watu.

12.JPG

Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya na Mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama cha CHADEMA jimbo la Mbeya mjini,Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II a.k.a Sugu akiimba moja ya nyimbo zake ujulikanao kwa jina la ‘Sugu’ ambao ulionekana kuwachangamsha vijana wengi waliofika viwanjani hapo jioni ya leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chama hicho pamoja na Ilani yake.

4-Tundu+Lissu+akionyesha+mkataba+wa+buliyanhuru.JPG

Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na mgombea Ubunge wa jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lisu akiwahutubia wanachama wa Chadema waliofika katika viwanja vya jangwani jioni ya leo huku akiwa ameshika kitabu alichokisema kuwa ni moja ya mikataba ya migodi.

DSC00602.JPG

Mwenyeki wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe akijaribu kuwatuliza baadhi Wananchi kuwa wawe na utulivu hakuna kitakachoharibika,Mbowe ilibidi awatulize Wananchi mara baada kubaini kuwa shirika la utangazaji la TBC1 lilikatisha matangazo ya uzinduzi wa kampeni ya chama hicho yaliyokuwa yakirushwa LIVE na hata kuthubutu kutaka kumpiga mmoja wa watangazaji wa kituo hicho, na baadae TBC1 waliamriwa waondoke uwanjani hapo kwa usalama wao.

20.JPG

Mgombea Urais kwa Chama cha CHADEMA,Mh.Willibrod Slaa akiwapungia wananchi mbalimbali waliofika kwenye viwanja vya Jangwani leo jioni mara ya kushuka kwenye gari.

DSC00578.JPG

Mtangazaji wa Mahiri wa TBC1 Marin Hassan Marin akisindikizwa na askari ili kujaribu kuzuia lolote baya lisimkute wakati wakielekea kwenye gari kwa lengo la kuondoka kabisa eneo la tukio,hata hivyo baadhi ya wananchi waliokuwa na jazba ya tukio hilo waliendelea kulalama mpaka Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA,Freeman Mbowe aliposimama na kuwasihii wananchi watulie na amani itawale eneo hilo la jangwani,na kweli baadae hali ikawa shwari na uzinduzi wa kampeni ukaendelea.

DSC00702.JPG

maelfu ya wanachadema waliofika katika viwanja vya jangwani leo.

DSC00619.JPG

Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Kawe,Halima Mdee akipitisha bakuri la kuomba msaada kutoka kwa watu mbalimbali waliofika viwanjani hapo,fedha hizo ambazo imeelezwa kuwa zitatumika kwenye mbio za kampeni ambazo wamezindua leo na wanatarajia kuzianza hivi karibuni Tanzania nzima.

DSC00562.JPG

Msanii G- Solo akishambulia jukwaa leo.

DSC00531.JPG

Msanii wa Bongofleva Dani Msimamo akiimba jukwaani.
DSC00526.JPG

Mmoja wa Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Mkoloni ambaye pia ni Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akisoma lisala fupi kwa niaba ya Wasanii wenzake kuhusiana na mambo mbali mbali yanayoikumba anga ya muziki na wanamuziki wenyewe,Mkoloni baadae lisala hiyo aliikabidhi kwa mgombea Urais wa chama hicho Dr.Willbroad Slaa.

DSC00515.JPG

WanaChadema wakiwa juu ya mti ili kuweza kuona na kusikia kila kinachoendelea katika viwanja vya jangwani.

DSC00555.JPG

Askari Polisi wakituliza ghasia zilizotaka kuletwa na wanachama wa Chadema katika gari la kurushia matangazo la Television ya Taifa TBC.

DSC00558.JPG

Gari la matangazo la TBC baada ya kuwekewa ulinzi ili lisiletewe fujo na wanachama wa Chadema.

DSC00521.JPG

Mkutano ukiendelea.

DSC00459.JPG

walielekea jukwaa kuu.

DSC00437.JPG

gari lililommbeba mgombea urais wa Chadema likiwasili katika viwanja vya jangwani leo.

DSC00417.JPG

moja ya vioja vilivyokuwepo katika viwanja vya jangwani leo

DSC00413.JPG

DSC00506.JPG


umati wa wanachadema leo.


2.jpg

Pichani mmoja wa wananchi akionekana kung'aka kwa hasira na kuanza kumfokea mtangazaji wa TBC1,Marin Hassan Marin mara baada ya kubainika kukatizwa kurushwa kwa matangazo ghafla ya uzinduzi wa kampeni na Ilani ya chama hicho yaliyokuwa yakirushwa LIVE kupitia shirika hilo jioni ya leo.

1.jpg

Katika hali isiyo ya Kawaida,Mpiga Picha na Mtangazaji mahiri wa shirika la Utangazaji la TBC1,Marin Hassan Marin walijikuta ndani ya wakati mgumu kwa baadhi ya wananchi waliokuwepo uwanjani hapo wakati wa uzinduzi wa kampeni na Ilani ya chama cha CHADEMA leo jioni,mara baada ya kubaini shirika la utangazaji la TBC1 kukatisha matangazo ya uzinduzi wa kampeni ya chama hicho yaliyokuwa yakirushwa LIVE na hata kuthubutu kuleta fujo ya kutaka kuharibu mitamb0 ya Shirika hilo huku wakitishia kumpiga mtangazaji huyo.
 
Hivi kwa nini CHADEMA wanavaa hayo magwanda? Na yanauzwa wapi kama mtu anataka kuyanunua?
 
Marina Hassan alistahili kuchapwa, kavaa gwanda lina ki-Tom and Jerry kukejeli CHADEMA

DSC00578.JPG
 
Idadi ya watu waliohudhuria kwa kweli inatia moyo sana, ukizingatia hawakusombwa na magari wala kuhongwa pesa ya nauli kama watani wetu walivyofanya. Kuna tumaini kubwa kwa CHADEMA mwaka huu. Mungu awatangulie.
 
picha na habari kwa hisani ya MICHUZI


Hakika kwa hili Michuzi apewe sifa, na wale waliokuwa na wasiwasi kuwa hatatoa habari za uzinduzi wa Kampeni ya CHADEMA bila ya shaka watakuwa wameziona picha hizi.
 
Chama cha Kidini na kikabila kimeamua kumvalia mgombea mwenza vazi la kiislam ili wafiche udini. Siku hii ndio anatakiwa kuvaa uniform za chama hatakama designer wetu kawadhalilisha, inabidi mzivae tuu!

M/Kiti kaishia 1V

N/Mwenyekiti STD 7 na

Katubu mkuu kasomea, Bible studies

Kweli hiki chama kitatupeleka wapi ? kwa nini wasijiunge na atleast na chama cha wasomi CUF ilimlete upinzani wa kweli ?
 
Chama cha Kidini na kikabila kimeamua kumvalia mgombea mwenza vazi la kiislam ili wafiche udini. Siku hii ndio anatakiwa kuvaa uniform za chama hatakama designer wetu kawadhalilisha, inabidi mzivae tuu!

M/Kiti kaishia 1V

N/Mwenyekiti STD 7 na

Katubu mkuu kasomea, Bible studies

Kweli hiki chama kitatupeleka wapi ? kwa nini wasijiunge na atleast na chama cha wasomi CUF ilimlete upinzani wa kweli ?


Madrasa al Sul
 
DSC00578.JPG

Mtangazaji wa Mahiri wa TBC1 Marin Hassan Marin akisindikizwa na askari ili kujaribu kuzuia lolote baya lisimkute wakati wakielekea kwenye gari kwa lengo la kuondoka kabisa eneo la tukio

Huyo aliyevaa kofia ya CHADEMA nae ni askari? Wa chama gani?
 
Kuweni makini na watu wanaohubiri udini wakati huu wa kampeni, WAMETUMWA. Ushauri wangu ni tusiwasikilize maana hata kama yeye angetaja majina yake kamili utakuta lazima anadini. Na ukiangalia hata KARUME na NYERERE WANA DINI, MWINYI NA SALMIN WANA DINI, MKAPA NA AMAN WANA DINI, KIKWETE NA SHEIN WANA DINI, LIPUMBA NA SEIF WANA DINI, SLAA NA MZEE WANA DINI, etc. na kama kuna mgombea ambaye hana dini aseme maana si hatuangalii dini, tunaangalia UPEO NA UJASIRI alionao. Mimi nafikiri serikali ingetoa tamko kuhusu hawa watu wanaozungumzia masuala ya dini hadharani wachukuliwe hatua kali.

Najua kuna watu wanahofu kuwa akishinda mtu mwenye msimamo watakosa ulaji. Ndo sababu wanahutubia mambo ya dini wakidhani watanzia wachagua kwa kuangalia dini au Rangi.

Wafahamu muda wa kuwadanganya watanzania umekwisha. Kama wagombea wakihubiri dini kama hawa mafisadi wanavyotaka unafikiri nani atapita mbona jibu unalo. unafikiri huyo unayemtenga ana kundi dogo au unajidanganye.

Mwisho hawa wote wanaotaja dini za wenzie ni mafisadi. Tusiwasikilize
 
Kutoka kwenye kimeo changu. Jangwani hatukuenda tu kwa kupakiwa kama mizoga bali tulikwenda kwa maandamano. Huwezi kuamini tulipo pita kariakoo njisi watu walivyokuwa wanafuraha na kushangilia. Yaani hapa inahitajika nguvu kidogo tu tuwabinue hawa watu

675tog.jpg


2r3wep2.jpg


2r3aurn.jpg


jue6hd.jpg

2hxtwud.jpg
 

Attachments

  • DSC03310.JPG
    DSC03310.JPG
    35.4 KB · Views: 83
  • DSC03323.JPG
    DSC03323.JPG
    62.8 KB · Views: 81
  • DSC03314.JPG
    DSC03314.JPG
    53 KB · Views: 76
  • DSC03317.JPG
    DSC03317.JPG
    49.1 KB · Views: 81
  • DSC03322.JPG
    DSC03322.JPG
    63.4 KB · Views: 74
  • DSC03320.JPG
    DSC03320.JPG
    53 KB · Views: 76
  • DSC03326.JPG
    DSC03326.JPG
    44.5 KB · Views: 83
  • DSC03325.JPG
    DSC03325.JPG
    47 KB · Views: 89
Hivi kwa nini CHADEMA wanavaa hayo magwanda? Na yanauzwa wapi kama mtu anataka kuyanunua?
nafikiri hilo ndiyo lingekuwa swali lako zuri sana, lakini kwa nini wanavaa hayo magwanda,
naona kama hujaisumbua sana akili yako kabla ya kuuliza au ungeli editi kwanza
 
Hakika kwa hili Michuzi apewe sifa, na wale waliokuwa na wasiwasi kuwa hatatoa habari za uzinduzi wa Kampeni ya CHADEMA bila ya shaka watakuwa wameziona picha hizi.
ongera michuzi kwa picha hizi
 
Marina Hassan alistahili kuchapwa, kavaa gwanda lina ki-Tom and Jerry kukejeli CHADEMA

Huyu ni miongoni mwa vibaraka wakuu wa Kikwete.
Alikuwa analalama kiunafiki.
washukuru watanzania waliokuwa pale walizituliza sana hasira zao. Ukichangia ushauri wa Mbowe, mzuka ukapoa.
Hawana maana katika hili TBC.
 
pole sana marini h marini, hiyo ndo kazi kaka

Huwezi kumpa pole na kusema ndiyo kazi wakati tatizo amelsababisha yeye mwenyewe.
Halafu alikuwa ana-lugha mbovu hata kwa waandishi wenzake(wasio wa TBC)
Anaondoka kwa huzuni ni kwasababu ameaibika kutokana na uovu wao.
 
Back
Top Bottom