Picha za tv

MBUTAIYO

JF-Expert Member
Nov 15, 2010
681
391
Wana JF,
Naomba msaada wa wataalam wa picha na TV.
Kuna kitu kwenye picha kinaitwa "aspect ratio", hii ni ratio ya urefu na upana wa picha ili picha ionekane katika uhalisia wake.Katika TV za kizamani (mitungi) hili linadhihirika na picha iliyorushwa inaonekana katika uhalisia wake, lakini katika TV za kisasa (flat screen) picha inaonekana bapa, yaani urefu unapungua na upana unazidi. Hii imenifanya nisinunue flat screen na siku zote natumia mtungi.
Naomba mnijuze kwamba flat screen ndivyo zilivyo au ninaweza kupata iliyo na ratio sahihi?
 
Back
Top Bottom