Picha za Simba anayekufa kutokana na ujangili Tanzania zashtua Dunia.

Ambiente Guru

JF-Expert Member
May 21, 2012
2,596
1,071
Picha za Simba anayekufa kwa njaa na maumivu kwa kunyongwa na nyaya za Majangili ndani ya Hifadhi moja ya wanyama hapa Tanzania zimeishtua Dunia.
Picha hizi zilizoonyeshwa majuzi katika Mtandao wa Daily Mail Online zimeshtua dunia kutokana na maoni yaliyotolewa na wasomaji..
Tazama: Lion with poacher's wire around neck in Tanzania | Mail Online ya tarehe 21 na 22 May 2012.
Swali ni Je Tanzania tunatumia elimu ya umma zaidi kuelimisha jamii badala ya kupambana ana kwa ana na majangili kulinda Wanyama wetu?. Hii ni changa moto kwetu Wana JF na Watanzania wote.

Doomed to die: The wire was twisted so tight that the lion was unable to eat
Tufanye nini wadau kunusuru wanyama hawa???

Soma zaidi au Read more: Lion with poacher's wire around neck in Tanzania | Mail Online

Nawakilisha
Candid to My Country

Richard Mazingira
 
Serikali na jeshi la polisi kupitia wizara husika zinatakiwa ziwajibike kutokana na ujangili huu. Ni vizuri kwa nchi kama tanzania kulinda rasilimali zake ili kuendelea kupata pato la taifa. Hata hivyo sioni sababu ya kuweka picha hizo katika mitandao kana kwamba ni kitu cha ajabu sana mbona watu wanauawa kila kukicha na hamuweki hizo picha?acheni usanii bandugu
 
Huyo jamaa aliyefanya shooting aliona ni busara kupata taarifa ya kuuza yenye kumpatia umaarufu lakini hakuona ni busara kureport kwa relevant authorities ili wa take charge ya kumuokoa huyo simba??!

That is the best they saw in our national parks??!
 
Aliyepiga picha hana kosa, kwake ni biashara.
Hao tunaowalipa mishahara kulinda wanyama wetu mwisho wa mwezi wataenda kupokea mishahara?
Kuna askari wa wanyama pori, tuna TANAPA na taasisi kibao, hawakuona?
 
Serikali na jeshi la polisi kupitia wizara husika zinatakiwa ziwajibike kutokana na ujangili huu. Ni vizuri kwa nchi kama tanzania kulinda rasilimali zake ili kuendelea kupata pato la taifa. Hata hivyo sioni sababu ya kuweka picha hizo katika mitandao kana kwamba ni kitu cha ajabu sana mbona watu wanauawa kila kukicha na hamuweki hizo picha?acheni usanii bandugu

Huoni ajabu kwa vitendo kama hivi?
Wenzetu wanaendelea kwa sababu ya kufuatilia vitu kama hivi ili hatua stahili zichukuliwe!
 
article-2147630-13358727000005DC-595_634x423.jpg

huyu ndio simba mwenyewe.....
 
imeniuma sana kusikia kua alikufa ,nilidhani wangemuwahi kabla hajafa kwani nasikia askari wanyamapori walishaenda kumsaka ili wamuokoe.so sad,wanachuma hela kuneemesha matumbo yao alakini kuangalia chanzo na kukilinda hawana akili hiyo.pumbavu zao limaige limenenepa mpaka nyoro kwa kutafuna pasipo kulinda ,dhulma yao itawatafuna tu.
 
hiyo dunia inashtuka simba kufa?
Kwa nini isishtuke vifo vya wajawazito?
Inaacha kushtuka adhari za ukame na njaa huko vijijini inashtuka simba kufa....
 
Aliyepiga picha hana kosa, kwake ni biashara.
Hao tunaowalipa mishahara kulinda wanyama wetu mwisho wa mwezi wataenda kupokea mishahara?
Kuna askari wa wanyama pori, tuna TANAPA na taasisi kibao, hawakuona?
Kama mnaangalia TBC kuna vipindi vya TANAPA walionyesha Madaktari wa TANAPA wakimshughulikia simba huyu baada ya kupata taarifa toka kwa mtalii aliyepiga picha
 
hiyo dunia inashtuka simba kufa?
Kwa nini isishtuke vifo vya wajawazito?
Inaacha kushtuka adhari za ukame na njaa huko vijijini inashtuka simba kufa....

Afadhali nawe umeona ..Wanyaruanda walikufa zaidi ya 800,000 hawakushtuka .Kweli ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni
 
Afadhali nawe umeona ..Wanyaruanda walikufa zaidi ya 800,000 hawakushtuka .Kweli ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni

Hawa wazungu + watu wanaojiita conservationist ni manyangau. Wanaspend alot kwa kulinda, kutetea na kupanua hifadhi za wanyama at the expense ya watu wanaozunguka hifadhi kuwa marginalised. Kwao wanyama ni bora kuliko binadamu?!. They need to be rational otherwise a few of us will care.
 
Hiyo Dunia ikishastuka kifo cha simba mla watu, wastuke pia na jinsi madini na rasilimali zetu zinavyotoroshwa na kupelekwa Ulaya.
 
Wanajeshi wa JWTZ wapewe kazi ya kulinda wanyama kwenye mbuga zetu zidi ya majangili sio kukaa makambini tu na kuota vitambi vya bia na nyamachoma.
 
Yaani we ndo bure kabsaaaaaa, unanikumbusha wale wapigapicha waliokuwa wanapiga picha nyumba inaungua moto,badala ya kuwaokoa watoto waliokuwa ndani wanateketea, eti walikuwa wanataka kupiga picha nzuri za kuweka kwenye gazeti kesho yake.
Aliyepiga picha hana kosa, kwake ni biashara.
Hao tunaowalipa mishahara kulinda wanyama wetu mwisho wa mwezi wataenda kupokea mishahara?
Kuna askari wa wanyama pori, tuna TANAPA na taasisi kibao, hawakuona?
 
Kama mnaangalia TBC kuna vipindi vya TANAPA walionyesha Madaktari wa TANAPA wakimshughulikia simba huyu baada ya kupata taarifa toka kwa mtalii aliyepiga picha
YULE ANAEONYESHWA TBC ni wa Serengeti na ajaumia hivi,na sio Clip ya mwaka huu.angalia vizuri na sikiliza maelezo mkuu
 
Binadamu ana haki zake na mnyama vile vile!
Sioni sababu kwanini tusizungumzie ukatili kwa wanyama eti kwa kuwa tu wapo Binadamu wanaofanyiwa ukatili kila kukicha.
Mnyama anaongozwa na kusimamiwa na mwanadamu,lakini hilo halihalalishi kumtendea uovu mnyama!
 
Back
Top Bottom