Picha za miili ya Wanafunzi 12 walio ungua kwa moto Idodi

Jamani jamani ,machozi yananitoka,jamani this must be stopped,wahusika wa mashule ,majengo etc,jamani wawe makini,mimi huwa naamini sometime wanatake for granted kwakuwa hawajaexperience haya mauchungu,ingetokea kw mmojawapo ,action ingetake place mapema,kuna wataaalamu hapa wa moto jamani fanyeni kazi ,hawa wanafunzi ni watoto wa watu,pia ni viongozi wa baadae sasa kama tukiwapoteza kwa njia hii athari ni kubwa sana hata kwa wanaobaki,please please serikali do something.
 
uwiiiii kizazi kimenicheza, jamani wazazi wenzangu poleni sana yaani mnavyojickia kwa sasa mungu ndio anaejua......jamani unamuhangaikia mwanao unajinyima kwa kila kitu anakuja kukutoka kwa dizaini hii? inaumaaa sana tena sana.....
 
Emergency Evacuation Plan
  • Draw your building’s floorplan, then draw your evacuation
  • routes and a meeting place.
  • Make one drawing for each story of the building. Keep in a safe place and review often with your people.
  • Have maps ready for the following:
  • Closest evacuation centers.
  • Main and Alternative routes for leaving the area in North, South, East and West directions.
  • Meetup spots outside the affected areas. For example: I live approximately 50 miles east of a nuclear power plant. Should there be an accident or an attack and the wind is blowing in an Easterly direction, our plan is to head north and meet up in a town approximately 60 miles north of my area.
You should have at least two (2) escape routes from each room.
You should mark the locations of any escape ladders, or other special equipment.
You should mark the locations of fire extinguishers, smoke detectors, first aid kits, disaster 72 hour kit.
You should mark the locations of the shutoffs for gas, water, and electricity.
For people with medical conditions or disabilities, mark their location as well as the location of any special equipment they will immediately need

Government should think of such issues!!!!!!!!!!!!

Action required, and this should be mandatory during and after school registration. Wakaguzi wa shule wasiangalie tuu mitaala, lazima usalama wa watoto wetu utiliwe maanani na isisitizwe hivyo. Inauma sana poleni sana wafiwa na mungu awajaalie majeruhi wapone haraka.
 
kwa mujibu wa taarifa ya waziri maghembe,marehemu wote wamechukuliwa vipimo vya DNA ili kuwatambua ni akina nani na majina yao yataandikwa katika makaburi yao hapo baadae baada ya zoezi la utambuzi kuisha.na pia watajenga mnara wa kumbukumbu mahali hapo,na pia watafanya kila linalowezekana kuweka vifaa vya utambuzi wa moshi/moto.
 
Dah inasikitisha sana na kutia uchungu kumbe bweni lilikuwa na uwezo wa kubeba wanafunzi 170 tamaa za uongozi wa shule ukabebesha wanafunzi 450
 
Eeee!! Mungu wa rehema uwarehemu marehemu wote wapumzike kwa amani. Uwasaidie majeruhi wapone haraka.
Inasikitisha kwa kweli na kutoa machozi, watoto wasio kuwa na hatia kufa na kifo cha namna hii.
 
Tatizo letu watanzania tunadhani kuwa Safety is luxury! Tatizo likitokea ndio tunachukua hatua, while it's too late!

Precautions zipo wapi?
 
Hivi serikali inashindwa kuweka mikakati kila bweni liwe na fire xtingisha 2 na ninakumbuka kuna somo lipo jinsi ya kujiokoa pindi majanga yanapo tokea sijui somo lile linaitwaje.
Suluhisho inabidi lianze na wabunifu wa majengo (labda ushauri wao haufuatwi) lakini majengo mengi ya jumuiya, hasa shule za wasichana, yanajengwa kama mtego fulani hivi, kinacholengwa ni kuona watoto hawaruki ukuta, lakini inapotokea balaa kama hizi, ndipo upande wa pili wa shilingi unapoonekana. lakini mbaya zaidi ni kuwa hata tukibaini mabaya haya, hatukawii kusahau
 
This is so frustrating... Inauma na zaidi inatia hasira. Kwanza jengo lina Capacity ya kuchukua watoto 170, unaweka watoto 450, utafikiri ni mahindi kwenye Godown?? pili, bweni kubwa kama hilo lina mlango mmoja tu, no emergency exit, tatu, nimesikia mtoto mmoja akihojiwa kwenye BBC anasema kuwa waishaingia kulala "Madam" (sasa sijui kama ndio Matron au la) anafunga mlango kisha anaenda kulala some kilometres kutoka kwenye bweni alolifunga kwa nje (kwenye nyumba za waalimu), jama hebu fikirieni, hawa ni binadamu, sio wanyama, serikali itaunda tume kuchunguza lakini kama kawaida hakuna kitakachotokea, Shule ya ShauriTanga iliungua mara mbili, wamechukua hatua gani. Lakini kinachonishangaza zaidi ni kuwa moto wa Mshumaa unaweza kuunguza kiasi hicho? au hilo bweni liliezekwa kwa makuti?
 
mungu awalaze marehemu wote mahali pema peponi, amen.ni kifo cha mateso na mahangaiko makubwa.
raha ya milele uwape ee bwana , wapate rehema kwa mungu wapumzike kwa amani.amina
 
Bado tunaomboleza huu msiba mzito maana vijana walikuwa taifa la kesho walipenda kwendelea kuishi lakini ndo hivyo tena maisha yao yamekatishwa kwa moto.
 
Poleni sana wazazi, ndugu jamaa na marafiki kwa msiba mkubwa huu,,,,
Inatubidi tubadili utamaduni wa mabweni ya wanafunzi ili uwe wa kisasa, kwa kubadilika tutaepuka majanga kama haya ambayo mengine kuyazuia inawezekana.
 
Poleni sana kwa wazazi na marehemu wote jamni inasikitisha sana Mungu awapumzishe mahali pema peponi!!
Wameteseka sana mpaka mauti yamewakuta jamni
 
Ni kifo cha mateso makubwa, poleni sana ndugu, jamaa na wote walioguswa kwa karibu na msiba huu. Kwa mara nyingine tena Taifa tumeingia katika majonzi makubwa ambayo yangeweza kuzuilika, na mara zote tunastuka baada ya tukio. Hii inaonyesha ni jinsi gani tusivyoweza na kujali kuwatumia wataalam wetu, kama Taifa tunao wataalam wa mioto hata kama si wengi. Swali ni je, wanatumikaje?. Najua kwa haraka tutawatupia lawama waalimu au wenye shule, lakini hawa kama hawana utaalam wowote wa majanga si rahisi kuweza kuhisi mazingira hatarishi. Kwao usalama ni kuona wanaweza kuzia watoto wasipate mimba n.k. Tunahitaji kutumika kwa wataalam wa wetu wa majanga kwenye ujenzi wa mashule na maeneo yote ya mikusanyiko.
 
Back
Top Bottom