Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,319
Mwanakijiji napingana na wewe kabisa.
Kununua nguo ni garama. Nguo zenye rangi ya bendera ya CDM au CCM au magwanda ya CDM ni garama.
Pamoja na garama hiyo, lakini nguo na hapa naongelea sare, lazima zivaliwe, kwani ni kama ishara.
CCM (mathalani kwa huyo mtoto uliyemwonyesha) wana uwezo wa kugaramia sare kwa washabiki wao (tembea maeneo ya vijijini, uangalie ni watu wangapi wana t-shirts zao).
CDM, hawana uwezo wa kugaramia sare kwa washabiki wao. Kama nilivyosema awali, kama ishara ya haiba na mwonekano wa chama (naamini unajua maana ya magwanda kwa CDM) ni lazima ivaliwe japo kwa wale wenye uwezo.
Ukifananisha na jeshi, unajua kuwa hata uwe na uwezo mkubwa kiasi gani kifedha, hauruhusiwi kujinunulia na kuvaa nishani za vyeo ambavyo hauna. Ila kwa CDM, mtu yeyote, anaruhusiwa kununua na kuvaa gwanda hata kama ni kali kuliko la Mbowe, kama ana uwezo.
Kuhusu staili ya kuzungukwa na watu walioshikana mikono, naamini ni staili tu ya kurahisisha ulinzi kwa viongozi wao. CDM wamefanya maandamano mengi sana nchini, wamekutana na changamoto nyingi, wamekabiliana nazo kwa staili tofauti, na naamini pengine kwa sasa wanaona staili hiyo ndiyo yenye inayofanya kazi pengine kwa garama ndogo wanazoweza kuzigaramia.
Hiyo Ulowashauri, nayo ni nzuri, lakini nahisi inaweza kuwa na garama zaidi, kwani unajua kuwa kila mtu anaruhusiwa kuvaa magwanda, na kama ukisema walinzi wavae sare tofauti na watu wengine, tayari unajenga haiba fulani ya kulindwa na watu ambao 'sio wenzetu'.
Ahsante