hawajamaa washone na suti za kwendea ikulu wamepita bila kupingwa
hawajamaa washone na suti za kwendea ikulu wamepita bila kupingwa
Dah, si kuna watu walisema hapa kwa Tanga Chadema hawakupata watu?
Ila kwa ushauri 'security' system iangaliwe kwa namna ya kipekee. Kwa namna Zitto alivyozongwa hapo chochote
chaweza kutokea. Sijui ni namna gani nzuri ya kiongozi kusalimiana na wananchi bila kuzongwa hivyo lakini ni vyema
mfumo wa ulinzi ukaangaliwa upya. Ni ushauri tuu lakini.
Uuu...CDM ilikoswa watu Tanga...Sasa yako wapi?!...CCM endeleeni kujifariji ila ukweli mko katika hali mbaya sana inawabidi mjipange upya...2015 haiko mbali.
Jana Mkuu wa Mkoa (ambaye kikatiba ni kada wa CCM) wa Tanga, Bi Chiku ..., alikuwa na kikao kizito na wakuu wa wilaya za Tanga na watendaji wengine na ajenda kuu ilikuwa juu ya namna ya kuboresha zao la MKONGE mkoani kwake kwa kauli mbiu ya "Mkonge ni Tanga na Tanga ni Mkonge".
SOURCE: Radio One - Nipashe [Leo].
Wana JF hebu tujiulize:-
(i) Je, yawezekana mikakati hii "mipya" ya watendaji wa mkoa ikawa na uhusiano na hoja binafsi ya Mh. Zitto Kabwe (MB) Bungeni na hatimaye ziara ya wabunge wa CHADEMA mkoani Tanga hivi karibuni?
(ii) Kama jibu ni ndiyo, hivi watendaji hawa wataendelea kusubiri kuamshwa au kusukumwa hususan na wapinzani au jamii hadi lini? Hivi tangu mwanzo hawakujua kwamba wanapaswa kuchukua hatua kuhakikisha zao la mkonge halifikii hatua mbaya lililo nayo hivi sasa badala ya kusubiri hadi wakurupushwe na hatimaye "kuiteka hoja"?