Picha ya Mwigulu Nchemba na Mwanae yazua mjadala mitandaoni

Nani anataka mwanae kuwa wa 'majaribio' ili hali uwezo wa kutokumfanya wa 'majaribio' anao? Nahisi hata kwangu ingekuwa ngumu...Cha msingi sisi tupambane waboreshe mazingira ya hizo za serikali, kuwapiga mikwara wawatoe wa kwao huko, ni njozi tulivu...
 
View attachment 321828
Picha ya Waziri wa Kilimo na Mifugo na Mbunge wa Iramba Mashariki imezua "hisia" tofauti na mijadala mitandaoni.Picha hiyo inamuonyesha Mh.Mwigulu akiwa na mwanae wa kiume,na "Caption" ya picha inayosomeka elimuniufunguo. Kikubwa kilichozua mjadala ni nembo katika fulana ya mtoto yenye maandishi ya FEZA SCHOOL.

Maswali na mijadala ya wengi ni kuwa,itakuwaje na moyo wa kuimarisha elimu ktk shule za umma kama sehemu ya mawaziri ambao ni watekelezaji wa sera ya Elimubure na Uboreshwaji wa elimu katika shule za umma wanakimbiza watoto wao katika shule binafsi? Kwanini Mawaziri ambao ni sehemu ya utekelezaji wa sera wanaoamini katika elimu bora katika shule za umma wao hawawapeleki watoto wao huko?

Picha hii imezua mijadala tofautitofauti na wapo wanoona Mh.Mwigulu yupo sahihi kupeleka watoto shule binafsi sababu ukweli ni kuwa shule za serikali elimu yao ni duni na isiyo na ushindani.

Hivyo mawaziri kuwapeleka watoto shule binafsi na zenye ubora kama FEZA SCHOOL ni kuwaepusha na elimu duni inayotolewa na serikali
ungekuwa wewe ungempeleka st kayumba? acheni kulalama sivyo sema huna pesa!
 
Sasa baba yake alikuwa anatafuta pesa za kazi gani? Kwa yoyote ya kibepari matabaka ni kitu kisichoepukika

Tukisoma katika biblia tunsona Yesu akishirikiana na masikini ila yeye hakuwa masikini wa mwisho katika nchi yake
 
Kweli kabisa #Mwana.
Comrade ameonesha upungufu
Hapa ni suala la mgongano wa kimaslahi. Ni ngumu mno kwa Waziri kwa sababu yeye tu ana alternative kusimamia suala la kuboresha elimu inayotolewa na Public hiyo ndiyo issue!!
 
Family first..mfano kam mtu kipato chake zaid 5M per month,siwez mpeleka mwanang shule za school fees elfu.20 per year..
Naamka saa 12 asubuh naenda kazin narud nyumbani saa 12 jion,tabu hizi zote ni kwa ajili familia yangu waishi mazingira bora,mm nlisoma kayumba na mwanang nae asome kayumba mmmmmmh siwez aseeh
 
Shida ya watz tuliowengi tunafanya mambo kwa bahati mbaya tuliowengi tukiulizwa vipi mbona unawatoto watatu unasema huyu wa Tatu alikuwa nahati mabaya sasa kama umezaa kwa bahati mbaya utegemee kusomesha kwa mipango?.huyu bwana mwiguli ni msomi na kwa nafasi aliyonayo alijiandaa kwa ada ya gharama yoyote kusomesha mwanae kwani kwanafasi yake aliyonayo angeshindwa kumwandalia mwanae mazingira bora yakupata elimu binafsi ningemshangaa sana na ningemwona elimu yake haija mkomboa.hii bure inayosemwa na serikali nikwaajili yawatu ambao hatukuwa na maandalizi sasa serikali inabidi ijiande kwaajili yetu .hainiingii akilini kama ulijiaandaa ushindwe kulipa elfu ishirini kwa kijana uliyemzaa mwenyewe bila shuruti alafu uendelee kushupalia mtoto wa mwenzio ambaye alikuja kwa maandalizi
 
Anaweza kuwaambia kama hamuwezi kwenda Feza, nendeni IST.

Kwa mshahara wa mtumishi wa umma anawezaje kumpeleka mtoto wake kwenye shule hizi?

Ana kipato gani zaidi?
 
Pale shule ya msingi Bunge kuna tatizo gani kwani?
Nchini Ujerumani wafanyakazi /Mawaziri wa serikali ya nchi hiyo watoto wao hasa wa umri mdogo usoma katika shule ambazo ziko karibu na ofisi za wazazi wao. Hii husadia kuwapa nafasi ya ziada kuangalia watoto wao na kuwahepusha na "stress " zinazo weza kuathiri utendaji wao unaogusa usalama na maslahi ya nchi.

Tukirudi Tanzania. Ikiwa nasi tunataka mawaziri wetu wasiwe na stress katika utendaji wao, je tumawajengea utaratibu huo wa wajerumani? Hivi hiyo Feza School iko umbali gani na ofisi ya Waziri wa Mifugo na Kilimo? Je kuna shule ya karibu zaidi ya "St.Kayumba " ambayo mtoto wa waziri wetu angempelekwa ili kumuondolea stress waziri kufuatilia mtoto wake? Nipeni majibu!
 
Naunga mkono Hoja kwa 100%!​
Ni unafiki mkubwa sana anaounyesha Waziri Mwigulu kama ni kweli kwani akiwa kama Kiongozi ambaye anapaswa kuboresha maisha ya Mtanzania na hii ikiwa ni pamoja Elimu alipaswa awe mfano, kwa yeye kutokupeleka mtoto wake Shule ya Serikali in maana hana Imani na Shule za Serikali ambazo yeye amepewa jukumu la kuziboresha!


Kabla sijasoma maelezo nikajua amembeba mtoto wa Patel
 
Naunga mkono Hoja kwa 100%!​
Ni unafiki mkubwa sana anaounyesha Waziri Mwigulu kama ni kweli kwani akiwa kama Kiongozi ambaye anapaswa kuboresha maisha ya Mtanzania na hii ikiwa ni pamoja Elimu alipaswa awe mfano, kwa yeye kutokupeleka mtoto wake Shule ya Serikali in maana hana Imani na Shule za Serikali ambazo yeye amepewa jukumu la kuziboresha!
Usiunge mkono ndugu yangu. Waziri ana uwezo na haiingii akilini awafanyie majaribio wanawe kwa kuwapeleka shule ambazo hazikidhi. Uelewe kuna wananchi wanafanya biashara japo ni ndogo lakini wanaishi kwa kujinyima angalau watoto wapate elimu safi angalau hata akiwa ni moja. Mwamko wa elimu bora uko kwa kila mzazi. Hao mawaziri wawajibike tu ili elimu iwe bora lakini si lazima watoto wao wasome shule ambazo hazikidhi ati waonekane wako sawa na wadogo. Hata hivyo Mungu hakuumba watu wote sawa.
 
Niliwahi kutembelea shule moja ya msingi ya serikali hapa Dar es salaam, nikakuta mwalimu mkuu wa shule hiyo wanae wanasoma kwenye shule ya private!! Nikamuuliza ana maana kiwango cha elimu anachotoa kwa watoto wa wenzie ni duni kiasi hakubali wanae wasome shule anayoisimamia...akabaki anacheka.
yuko mkuu wa wilaya mmoja ameapa waziwazi kwamba watoto wake hawatasoma kwenye shule yoyote nchi hii , achilia mbali hizo shule zenu za kata .
 
LAKINI KAMA ANAMLIPIA ADA KWA MSHAHARA WAKE,MI KWA UPEO WANGU NAONA HAINA TATIZO,,,TENA SHULE YENYEWE IPO NDANI YA NCHI,INGEKUWA AMEMPELEKA LABDA NJE YA NCHI HAPO KWELI INGEKUWA NONGWA,,NA PIA INGETEGEMEA NA MSHAHARA WAKE, LABDA KAKOPA HELA ILI TU AMSOMESHEE MWANAE,OR WANAE,,,,,CHA MUHIMU NADHANI WAKUMBUKE KUTUBORESHEA SHULE IZI ZA KATA ILI NA SISI WATU WA HALI YA CHINI TUPATE ELIMU BORA,TUSIINGIE GHARAMA KUBWA KUPELEKA WANETU KTK SHULE AMBAZO ZINAKWANGUA KIPATO CHETU DUNI,,

Lakini linapokuja suala la Uzalendo jee unalionaje hapo?
 
Naunga mkono Hoja kwa 100%!​
Ni unafiki mkubwa sana anaounyesha Waziri Mwigulu kama ni kweli kwani akiwa kama Kiongozi ambaye anapaswa kuboresha maisha ya Mtanzania na hii ikiwa ni pamoja Elimu alipaswa awe mfano, kwa yeye kutokupeleka mtoto wake Shule ya Serikali in maana hana Imani na Shule za Serikali ambazo yeye amepewa jukumu la kuziboresha!

Kuunga mkono hoja ndiyo unafki wenyewe....We all know CCM imeivuruga nchi na mifumo yote ya huduma za jamii.....

ni mjinga gani mwenye pesa zake atampeleka mwanae kwenye shule ya darasa moja watoto mia kisa tu yeye ni mtumishi wa uma???

Imeandikwa wapi ukiwa mtumishi wa umma hutakiwi kuwa na maisha binafsi....kwamba hata ukiwa na uwezo basi nawe uishi maisha duni....hayo waliyaweza manabii na mitume...akina yakhe siye ni kujidanganya....
 
Ukereketwa (radicalization) wa viongozi wa Tanzania awamu ya tano kwa kuvaa scafu,kucheza ngoma jukwaani ,kunywa kahawa vijiweni, timuatimua na maneno ya elimu bure, huduma za afya bure kwa watoto/wazee n.k hauwezi kuwa wa vitendo na hamasa ya kiimani toka moyoni kuwajali wanyonge kama ilivyo kwa Mwanamapinduzi Fidel Castro :

soma
Fidel Castro facts:

RADICALIZATION OF THE CUBAN REVOLUTION
The early Cuban revolutionary regime developed a threefold strategy: a progressive redistribution of income, a radical change in the property system, and a lowering of major daily costs (such as food, rent, transportation, and public services) to benefit the lower classes. This resulted in broader political support among the lower classes and a reduction of the income and wealth of the upper classes, thus diminishing their available resources for counterrevolutionary activity.

As this radicalization advanced, the moderates within the revolutionary coalition joined the opposition or went into exile. Many members of the professions did the same. As the country lost skilled personnel, the state further centralized political, administrative, and economic resources. Facing a shortage of expertise, the revolutionary regime relied on the politically trustworthy, usually people who were radical, including Communists. Such trends further exacerbated the political climate and relations with the U.S. government.


Since 1959 resources have been concentrated in the rural areas and small towns, and the city of Havana has suffered. An ideology of inherent rights and entitlements has developed with a system that provides universal education, health and dental care, child care, and burial service free of charge. The state also assumes the responsibility of providing employment or giving the unemployed financial support.

Cuba is one of the most educated countries in the third world, with a life expectancy of 77.5 years and an infant mortality rate of 6.5 per 1,000 live births (as of January 2007). Education and health claim 23 percent of the gross internal product. The number of libraries, schools, hospitals, and dams increased dramatically from1959 to the mid-1980s.

Food has been subsidized since 1962, but it has been rationed as well. Just as libraries lend books, there are also centers that lend musical instruments at no cost. Every municipality has computer clubs where access is free. Thirteen percent of the population benefits from universal social security, and 4.2 percent receives social assistance checks.
Source: Fidel Castro Facts, information, pictures | Encyclopedia.com articles about Fidel Castro
 
Back
Top Bottom