Picha ya Mwigulu Nchemba na Mwanae yazua mjadala mitandaoni

watanzania wengi wana angalia mambo kijamaa zaidi.Hata shule za serikali zikiboreshwa hadi kuwa kama zilivyo shule za ST MARYS bado kutakuwa na shule za watu wenye pesa mingi.Nenda Uingereza public schools ni nzuri lakini huwezi mkuta mtoto wa waziri yeyote anasoma kule.
Teeeeeeeeh teeeeeeeeh teeeeeeeeeh teeeeeh teeeeeeeeeh, we jamaa kwani hapa ni uingereza?
 
Naona kuna baadhi ya wachangiaji hoja wanakubali kuwa ''mwenye nguvu ya kipesa/madaraka'' apate chochote kwa nguvu hiyo.

Hiyo ni sawa sawa na kusema ''mwenye nguvu kipesa/madaraka'' ruksa kutumia uwezo wake kufanya chochote mfano '' kumchukua kwa ''nguvu'' mke/mume wa mtu''.

Viongozi bora hujiwekea kanuni za msingi za kimaisha kuhusu watu anaowaongoza kwa kujiuliza je ninachofanya ni sahihi kwa umma niliopewa kuuongoza ikiwemo huduma bora za elimu/afya kwa wote na kuheshimu utu-wa-mtu?



Hivi watu wenye akili kubwa kama wewe wanajificha au basi tu serikali haitaki kuwatumia au hata tu kuwasikiliza?

Hii nchi inaongozwa na chama kinachokwenda shaghalabaghala, katiba iliyoko shaghalabaghala,uchumi ulioko shaghalabaghala, mipango iliyoko shaghalabaghala ,mawaziri na watendaji wenye misimamo ya shaghalabaghala. Mfumo wa Elimu ulioko shaghalabaghala.Bunge linaendeshwa shaghalabaghala.
Kwa kifupi kila kitu chini ya utawala wa CCM ni shaghalabaghala.

Watanzania walioipigia kura CCM na kuirudisha Madarakani chini ya katiba na mfumo ule ule walikosea sana hasa kwa kuwarudisha wabunge 72% toka CCM.
Viongozi wa CCM ni wanafiki na wabinafsi kuliko hata marehemu shetani.

Umeona Rais alifuta sherehe za uhuru ili kubana matumizi lakini Mwenyekiti wake na uongozi wa CCM akiwemo Mwigulu ambaye ndiye mwenye dhamana ya fedha wakaamua kumwonyesha Rais kuwa wao ndio vinara wa Matumizi kwa kuandaa bonge la sherehe zilizoadhimishwa kwa wiki nzima tangu uzinduzi kule Zanzibar.
Hapa kuna dhamira kweli kwa Chama tawala kumsaidia Magufuli kutimiza ndoto zake au ni unafiki tu?

Hizi zile pesa wanazotumia kumweka Shein Madarakani na kufanya masherehe ya kueneza chuki na ubaguzi zingetumika kule Zanzibar kuimarisha Mashule kwa kaeneo ka Zanzibar pekee tungeshindwa kuwa na shule bora za awali.

Serikali inajua kabisa kuwa Elimu ni ghali kwa shule binafsi na watu wanataka watoto wao wajue kingereza tangu shule za awali lakini mpaka sasa hawana mpango madhubuti wa kuimarisha shule za awali kwa kuanzia.
Kwa nini kila kata isiwe na shule ya awali ya English medium ambayo itatumia majengo ya serikali lakini wazazi wachangie angalau laki tatu kwa mwaka ni kama elfu 30 kwa mwezi.Ili wafanyakazi wa kule vijijini nao wapate shule za kusomeshea watoto wao kwa gharama nafuu.
Tofauti na ilivyo sasa shule bora ni za binafsi na gharama zao ni kubwa mno kwa mfanya kazi wa chini kumsomesha mtoto wake ni vigumu sana.
Hapa suala la Hapa kazi tu litakua limefanikiwa kwa kila mfanyakazi kwa uwezo wake kuweza kumsomesha mtoto wake kwenye shule bora.
Na isiwe ni mawaziri pekee kutokana na mishahara yao kuwa mikubwa.

Kudanganyana Elimu bure bila maandalizi na mikakati ni kuiua Elimu zaidi. Na watakao umia ni watu wa chini wenye mishahara halali lakini midogo.

Mawaziri wapo lakini wengine ni mizigo michafu inayovujisha uchafu.
Wanashindwa hata kujua jamii ya kitanzania inahitaji kufanyiwa nini?
Je,wamewahi kufanya utafiti wakagundua kuwa tanzania kuna walevi na wazinzi wangapi nchi nzima na wengi wao wana familia lakini nao wanaaminishwa kuwa hawawezi kulipa ada hata elfu kumi kwa mwaka mzima!! Sasa nao wanafundishwa kutamba kuwa elimu ni bure kabisa?
Badala ya kufundishwa kuwa wawe wanajiuliza maswali kama vile ;Je,ulevi wao unatumia sh. ngapi kwa mwaka? Wanahonga mahawara sh.ngapi kwa mwaka?
Mbona wanasiasa hawatuahidi kwamba wakiingia madarakani tutapiga simu au kutumia umeme bure?
Mbona hata kanisani kuna michango ya sadaka?
Elimu bure na duni isiyo mnufaisha mtanzania ni ya nini?

Je,Utafiti ulifanyika lini wa kugundua kuwa ni watanzania wangapi wasioweza kulipa hata ada ya elfu tano kwa Mwaka?
Na ni wananchi gani walishirikishwa?

Hivi imeshindikana kabisa kuweka mpango mzuri wa watu wa kipato cha chini kuchangia Elimu?
Mfano Ada iwe ni sh. 30000/ kwa mwaka halafu kila mzazi apewe muda wa kulipia kidogo kidogo kama hana pesa zote. Yaani hata akiamua kulipa kila mwezi 3000/ aruhusiwe na mtoto asome alimradi mwisho wa mwaka amalize.
Pesa hizo zitumike kuimarisha mipango ya ufundishaji tu ikiwemo posho za kuwalipa walimu kutoa majaribio au mitihani na kusaisha na kupanga matokeo kila katikati ya mwezi na mwisho wa mwezi ili kupima uelewa wa jumla wa wanafunzi kwa kile walichofunzishwa.

Elimu bure ni ngumu mno ,walimu hawana overtime ikiwa na maana mwisho wa kazi ni saa tisa na nusu. Darasa lina watoto mia nne. Atafundisha sa ngapi na kutoa jaribio sa ngapi na kusahihisha madaftari hayo sa ngapi?Ukizingatia pia walimu hawana nyumba karibu na shule ili hata apeleke madaftari nyumbani akasahihishe!!

Haya hao wasomi na watawala hawawezi kuyaona mana watoto wao hawasomi huko kwenye shule za bure.
 
Tundu Lisu alishasema hawezi kumpeleka mwanae kwenye shule ya Kata aka community schools. Je kipi cha ajabu kwa Mwigulu?

Hata hivyo kilichovaliwa no T-shirt tu ambayo MTU yeyote anaweza kuvaa sio lazima awe mwanafunzi wa shule husika.
 
waziri mzima hajui kwamba ni kosa kisheria kumuanika mtoto mitandaoni>
 
Ona vijana wa ukawa wanavyo ropoka hapa!!

Wamesahau kwamba Tundu Lisu amewahi kusema hawezi kupeleka watoto wake kwenye shule za kata, wakatokwa povu sana kumuunga mkono Leo tena sijui wanaongea nn hawa??
Tundu hayupo serikalini na aliongea vile kwa maana elimu upande wa shule za serikali ziboreshwe!!
 
Mwigulu na wengine walio wengi ni wasaka tonge tu. Maskafu ya bendera ya taifa na tai ni usanii tu.
Chezea kuwa mzalendo wa kweli ni ngumu kama ilivyo kuwa mlokole wa kweli.
 
Tanzania yote ni JIPU.
View attachment 321828
Picha ya Waziri wa Kilimo na Mifugo na Mbunge wa Iramba Mashariki imezua "hisia" tofauti na mijadala mitandaoni.Picha hiyo inamuonyesha Mh.Mwigulu akiwa na mwanae wa kiume,na "Caption" ya picha inayosomeka elimuniufunguo. Kikubwa kilichozua mjadala ni nembo katika fulana ya mtoto yenye maandishi ya FEZA SCHOOL.

Maswali na mijadala ya wengi ni kuwa,itakuwaje na moyo wa kuimarisha elimu ktk shule za umma kama sehemu ya mawaziri ambao ni watekelezaji wa sera ya Elimubure na Uboreshwaji wa elimu katika shule za umma wanakimbiza watoto wao katika shule binafsi? Kwanini Mawaziri ambao ni sehemu ya utekelezaji wa sera wanaoamini katika elimu bora katika shule za umma wao hawawapeleki watoto wao huko?

Picha hii imezua mijadala tofautitofauti na wapo wanoona Mh.Mwigulu yupo sahihi kupeleka watoto shule binafsi sababu ukweli ni kuwa shule za serikali elimu yao ni duni na isiyo na ushindani.

Hivyo mawaziri kuwapeleka watoto shule binafsi na zenye ubora kama FEZA SCHOOL ni kuwaepusha na elimu duni inayotolewa na serikali
 
Sio kosa wala dhambi... kipato chake kinatosheleza labda kama kingekua hakitoshelezi tungejiuliza maswali.. Kama ada ni 5m kwa mwaka hiyo ni karibu sawa na 417,000/ kwa mwezi ambazo ukitenga kwenye mshahara wake na posho hicho ni kiasi kidogo sana. Uzalendo sio kuvaa viraka kisa watanzania wengi wanavaa viraka
 
Tatizo unavamia tuu bila kuangalia muendelezo wa maongezi kuna mtu alidai kwamba walimu wa shule duni hawajui ''kingeleza'' nikamwamwambia wao wanajua Kiingereza ila hicho ''kingeleza'' hawakijui ..alafu hakuna kitu kinaitwa ''Kingereza'' labda ni mtaa wenu huko kwenu acha kufyatuka kama ushuzi Mkuu before criticizing take your time and read
Kingeleza = Kingereza.

Huyu ndiyo msomi wa lugha anayejisifia humu JF.

Teh teh teh
 
Kingeleza = Kingereza.

Huyu ndiyo msomi wa lugha anayejisifia humu JF.

Teh teh teh
''Kiingereza nm [ki-] English (language)'' hiyo ni kwa mujibu wa kamusi ya TUKI sijui ulikuwa unajichekesha nini? hizi fani za watu ndugu yangu
 
NCHI HII TUNADANGANYANA SANA ..NA NDIO MAANA HIZI SHULE ZA KATA HAZIBORESHWI WANASEMA ELIMU NI BURE WAKATI WATOTO WAO WANAWAPELEKA SHULE GHALI KULIKO ZOTE ..FEZA ADA YA MWAKA TU INAKARIBIA DOLA 15,000...WAKATI SHULE ZETU WANAKADIRIA WATOTO WETU DOLA 10 TU KWA MWAKA
 
Wafanyakazi tu wa kawaida bank wanapeleka watoto private schools, itakua waziri.
Hebu
 
Tatizo liko liko kwenu kuchelewa kuelewa..... Hizo shule za St Kayumba zinaanzishwa ili kuwasaidia watanzania wa kawaida wawapeleke watoto wao kule ili waendelee kutawaliwa. Hizi nyingine zinaandaa "Watawala"
 
Wafanyakazi tu wa kawaida bank wanapeleka watoto private schools, itakua waziri.
Hebu
Naona mkuu umeweka vizuri hapa kuwa waziri 'sio mtu wa kawaida' kama ilivyo kwa wafanyakazi wa benki.
Issue kubwa hapa sio mtu wa kawaida na 'asiye wa kawaida' bali ni ule msingi ulioleta maendeleo na mabadiliko duniani kote from time memorial kwamba "practice what you preach".
Kama ni hivi basi huyu bwana aache kutudanganya eti anaweza kutuletea ufanisi kwa vile ni 'mzalendo'.
 
View attachment 321828
Picha ya Waziri wa Kilimo na Mifugo na Mbunge wa Iramba Mashariki imezua "hisia" tofauti na mijadala mitandaoni.Picha hiyo inamuonyesha Mh.Mwigulu akiwa na mwanae wa kiume,na "Caption" ya picha inayosomeka elimuniufunguo. Kikubwa kilichozua mjadala ni nembo katika fulana ya mtoto yenye maandishi ya FEZA SCHOOL.

Maswali na mijadala ya wengi ni kuwa,itakuwaje na moyo wa kuimarisha elimu ktk shule za umma kama sehemu ya mawaziri ambao ni watekelezaji wa sera ya Elimubure na Uboreshwaji wa elimu katika shule za umma wanakimbiza watoto wao katika shule binafsi? Kwanini Mawaziri ambao ni sehemu ya utekelezaji wa sera wanaoamini katika elimu bora katika shule za umma wao hawawapeleki watoto wao huko?

Picha hii imezua mijadala tofautitofauti na wapo wanoona Mh.Mwigulu yupo sahihi kupeleka watoto shule binafsi sababu ukweli ni kuwa shule za serikali elimu yao ni duni na isiyo na ushindani.

Hivyo mawaziri kuwapeleka watoto shule binafsi na zenye ubora kama FEZA SCHOOL ni kuwaepusha na elimu duni inayotolewa na serikali
halafu hiyo tai aliyo vaa inahitaji mjadala!; manake sijawa kuona kuanzia JN hadi Magu kuining'iniza shingoni..
jee inakubalika?
 
Back
Top Bottom