Picha ya Mbowe walipokutana na JK: Je unajifunza nini kwenye picha hii?

mbowe-jk.jpg


mbowe.jpg


Je kweli mbowe kapandikizwa na CCM chadema? mbowe katumwa nini nini na ccm kwa chadema?
 
jeykeywaukweli

welcome back.....nilidhani this time utabadilisha nafaka zinazozalisha pumba ..... lakini naona pumba zinaendelea kuwa ni zile zile tena zimechanganyika na upupu
 
Kwa muelekeo wa gazeti la Tanzania Daima na hasa kwenye Dowans Scandal naanza kuwa na wasiwasi sana. Ipo siku wanaoegemea sana CDM wanaweza wasiamini macho yao.

Don't say i didn't warn you!
 
Jamani wadau kuna kosa gani hapo Mbowe kuhudhuria hafla hiyo? Mbowe kahudhuria kama kiongozi wa upinzani bungeni.Je kweli asimsalimie JK? Kwanza nampongeza kwani kavaa kombati kama heshima kwa makamanda wote na wapiganaji
 
JK ameonyesha kutojiamini na ushindi wake...kama ni Rais wa kweli angeendelea kukaa maana yeye ndio supreme halafu Mbowe apige magoti!...halafu Rais hashikwi bega kihivyo..

ANGEWEZA KUBAKI AMEKAA KAMA ANAVYOFANYA KWA WENGINE....LAKINI BESIDE SIASA LAZIMA UJUWE KUWA JK NA MBOWE NI PERSONAL FRIENDS ...urafiki umepungua siku hizi kwa ajili ya urais..miaka yote kikwete amekuwa mteja mkubwa wa Mbowe Club [enzi za mzee Aikael] hadi CLUB BILICANAS [much more/mamaz]....and they used to share GIN and JUICE ......

Mbowe ...amekuwa mtoto wa mjini muda mrefu tangu enzi za mwalimu hasa kutokana na baba yake kuwa na ile CLUB na utashi wake wa kuwa karibu na vijana wenzake wa enzi hizo......kwenye starehe hakuna siasa ..watu kama kina IPPIYANA MALECELA, MAURICE WAMBURA, ABDUL MSOMALI, MAKONGORO NYERERE... JOSEPH KUSAGA etc...walikuwa permanent members kwenye Mbowe club....na watu kama Kikwete ambaye hata kabla ya kwenda jeshini alikuwa mtoto wa Magomeni Kota

...THEY HAVE SOMETHING IN COMMON.....Nadhani Mzee FIELD MARSHAL ES akiona hii atachangia vizuri..
 
Baada ya muda mrefu sjaandika kwenye jamvo hili
jana nimeziilisha kuwa mbowe sio wa chademu mana
inaonekana kama ana rangi mbili

mbowe sasa imeiziilisha umma kuwa yye sio chademwa ana mapenzi
na rais wetu jk

je mbowe katumwa?
 
Ha ha ha haaaaa, kweli hakuna upinzani wa kweli Tanzania. Hapo Mbowe na maneno yake yote anaonyesha utiifu na unyenyekevu kwa Mh. Rais , Dr. Jakaya Mrisho Kikwete
 
Wamatumbi ni kitu kimoja regardless wanatofautiana kiitikadi, this is only in Tanzania. Changamoto ni kwa viongozi hawa kupeleka ujumbe huu kwa wafuasi wao ambao uwelewa wao kidogo unahitaji miongozo kutoka kwa viongozi wao.

Kali kuliko zote ni wafuasi wengi wana mawazo mgando (imani kali) ambayo wakati mwingine wanadiriki hata kusema uwongo kulinda yale waliyolingania, mfano ni wachangiaji hapo juu ambao hawaamini kama hili limetokea baada ya 2010 election.
 
mbowe-jk.jpg


Wanasiasa siku zote hawatabiriki!

Wasalaam

Kwa watanzania wataona jambo la ajabu lakini nje ya siasa kuna maisha ya kawaida.Mbowe hata angepanda kwenye jukwaa la kisiasa baada ya kusalimiana vizuri bado angebaki na misimamo ya chama chake.Bado angesema hawajaridhika na mchakato uliompatia Raisi madaraka hayo,bado angesema kwamba-maandamano ya kupinga ulipwaji wa dowans bado yako pale pale.Ndivyo ilivyo.John Mc Cain wakati anatafuta uraisi wa marekani katika moja ya kampeni zake aliibuka mshabiki mmoja wa republican alieanza kusema kwamba Obama ni mweusi ni mwislam n.k maramoja Mc Cain akamwambia unakosea na Obama ni mmarekani mwenzake anaeishi vizuri na familia yake.Hivyo kupingana katika misimamo ya kisiasa haiwezi kunyima watu kupigana chenga japo kusalimiana.
 
Ni miezi kadhaa imepita tangu CHADEMA wakatae kumtambua JK kama raisi halali wa Tz, leo tunaambiwa kwamba mwnkt wa chadema Freeman Mbowe kamtambua JK kama raisi halali wa Tz, najiuliza ni kipi kimefanyika kudhibitisha uhalali wa huyu Mheshimiwa na wakamtambua? Kwangu mimi huu ni undumilakuwili na ukengeukaji! Haiwezekani ukawa mtu kigeugeu namna hiyo. Bwana Mbowe itabidi awashawishi wenzake nao wamtambue coz aliwaongoza kutoka nje ya Bunge na kutokumtambua JK kama raisi halali wa Tz. Wadau mna mawazo gani kuhusu hili jambo? Kuna uhalali wa Mbowe kufanya alichofanya? Haya ni mawazo binafsi hayana chuki na Mbowe ila nasikitika kuwa viongozi wengine wa Chadema kama wao wataendelea na msimamo wao ili hali Mwenyekiti wao ameshauvunja. Nakaribisha majadiliano Wadau.

Ndugu yangu nadhani umepotea kidogo, Chadema hawajawahi kusema hawamtambui kikwete kama rais, walichosema walipinga 'process' iliyomweka kikwete madarakani, na jana alichosema mbowe anamtambua kikwete kama rais 'halali kisheria', kwa kuwa alitangazwa na tume ya uchaguzi kama mshindi kama sheria inavyotaka lakini si rais halali kidemokrasia (haya ya italics ni ya kwangu).
Lakini adui unaweza kumdhibiti vizuri ukiwa karibu yake acha amtambue, nafikiri haitakuwa na impact kwenye struggle ya kulikomboa taifa hili.
 
02_11_hqbpgc.jpg
Rais Jakaya Kikwete (kulia) akisalimiana na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe wakati wa sherehe za Siku ya Sheria zilizoanyika Mahakama Kuu, Dar es Salaam. (Picha na Freddy Maro).

"Will you endorse my presidential bid comes 2015?" Queried Mbowe.........................................
 
nimejifunza kwamba;- Hata ukichakachua matokeo, WEWE NI JAMAA YANGU... ila matokeo yaliyokuweka madarakani SIYATAMBUI
 
inaonyesha siasa in its true color, wakati wananchi wa kawaida mnatolewa muhanga huku kwa kupigwa risasi wao wakikutana wanacheka na kunywa chai pamoja.
 
Huu ndiyo uzuri wa Tanzania, kupishana kiitikadi kupo lakini huo sio uadui , kipindi kile Dr. Slaa alipoanguka bafuni na kuumia mkono JK alipigia cm na kumpa pole. mi nafurahi sana kuona hari ya namna hiyo. isitoshe mbowe na jk wanafahamiana hata kabla ya wote kuwa viongozi.

binafsi kwa mara ya kwanza nilishangaa zanzibar wakati wa utawala wa komandoo Salmin Almuru walikuwa na uhasama ukubwa na CUf na ikatokea Malim Sef anaoza binti yake na alituma kadi ya mwaliko kwa salmin naye akahudhuria wakaa pamoja wanacheka wakaagana na kila akaendelea na ya kwake. kutoka pale nikaingalia siasa kwa jicho la tatu na kugundua kuwa aina ya mchezo fulani ambao sio uwadui. na kwa taarifa yako Dr slaa ndiye aliyemshauri Samweli Sita asijitoe ccm
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom