MduduWashawasha
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 1,653
- 601
Huyu Kyalesi ufalme utausikia kwenye bomba tu.Mama akidedi hapo ni mtoto ndo anakamata kitu
wakati sisi tunauangamiza utamaduni wetu kwa ufinyu wa kufikiri na kutaka kuhakiksha maslahi yetu binafsi hayapati kikwazo, wenzetu wanauendeleza kwa nguvu zote, Uingereza, Norway, Sweden n.k. nchi hizi ni tajiri sana na zinaongoza kwa kutupa misaada, ila hata ukienda kwao, wamehifadhi vya kutosha zile kumbukumbu za mila na desturi an bado wanajitahidi kupractice mila kila inapowezekana.
Mkuu Sangara, ndiyo maana pamoja na kuiunga mkono hoja yako ya nyumba bora, ila siafikiani na dhana ya kutokomeza nyumba za udongo na makuti, iwapo zitaboreshwa, nyumba hizi hata waingereza wanazo leo, hazina kelele, haziingizi baridi wala joto na ni very comfortable afrodable kwakuwa ni organic no chemicals za paints kama lead n.k. Hebu fanya utafiti kule South Africa uone jinsi wanavyozitengeneza nyumba hizi, pia kule Usambara nimeona, wanazipaka rangi zitokanazo na udongo na mimea, zinapendeza kwelikweli. Elimu ya kuziboresha ili zisibebe magonjwa na zidumu mda mrefu inahitajika.