Picha: Wengi wajitokeza kuuaga mwili wa kamanda Liberatus Barlow leo Nyamagana

Imekuwa neno RPC liko midomoni mwa watu tangia kifo cha Mwangosi kitokee ........... alizungumzwa sana RPC Kamuhanda.... ikatokea kifo cha RPC Barlow...... R. I. P. DAUDI MWANGOSI.... R. I. P. LEBERATUS BARLOW
 
NOTE:

NI ACP (Assistant Commissioner of Police - Kamishna Msaidizi wa Polisi) siyo SACP (Senior Assistant Commissioner of Police - Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi)... ACP Liberatus Lyimo Barlow.

Natanguliza shukrani.

ahsante Mentor kwa ufafanuzi wako. Hata mimi ckuwa naelewa hlo.
 
Last edited by a moderator:
hata picha huwezi kuangalia??

Mkuu, si lazima ujibu hata kama huelewi mantiki

Media, Jeshi la polisi na hata JF tumekuwa mbele sana kuangalia mazingira ya kifo na kupitiwa kuangalia kwamba as a human being and a father/husband, he had a family life too.... and what he fought against majambazi ni ili tulale sana sisi na familia zetu

an appreciation for his family kwa kuendelea kuwa nae hadi mwisho wa maisha yake si kitu kibaya

Sidhani kama jibu ulilotoa lina-make sense; but you are entitled to your responses

thanks
 
Nilikuwepo eneo la tukio.
1. walianza makamanda wa mkoa kutoa salamu za rambirambi, na walitoa kila kamanda na pesa kama sehemu ya kusaidia shughuli za kuhani. wengine milion, wengine laki kadhaa wengine milion 2.
2. Wakafuatia viongozi wa dini, nao na umoja wao wakatoa 300,000/
3. Wakafuatia CCM mkoa wa mwanza, isiyo na mbunge wa kuchaguliwa bali yupo wa kuteuliwa, zikatoka 1,000,000/-
4. Ikafuatia CCM mkoa wa geita, pamoja na uchanga wao, lakini wameshukuru kufanya kazi na kamanda wakati Geita ikiwa sehemu ya Mwanza, nao wakatoa 1,000,000/-
5. Wakakaribishwa CCM B a.k.a CUF, mwakilishi hakuibuka, alikaa kimya.
6. Wakakaribishwa CHADEMA, chama chenye wabunge wawili hapa mjini na wabunge wengine wako wilyani, alzungumza mambo mazuri, akawaasa wananchi kuendeleza ushirikiano na WATUMIE Dhana ya PEOPLES POWER kuwafichua waliohusika na mauaji ya Barlow, na waendeleze ushirikiano. Yeye tofauti na wengine wote waliotangulia, waliomalizia kwa kutoa RAMBIRAMBI, yeye alitaja jina lake tu. Watu walinung'unika, wakionesha wanataka kusikia CHADEMA wamechangia bei gani kwenye msiba huo.
7. Wakakaribishwa wajumbe wa kuzuia uhalifu mwanza, nao wakatoa 2,000,000/-
8. Wakafuatia chama cha wenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro ambapo Balow alikuwa ni mwanachama mzuri nao wakatoa 2,000,000/-.

Ta Muganyizi Huoni kuwa CHADEMA hawakujiandaa?

wewe umetoa tsh ngap? Utu ni bora kuliko pesa.
 
R.I.P kamanda.

tunasubilia uchunguzi wa hiki kifo,DCI manumba na interpol watatupa ukweli.
 
mimi nachowaza hivi wale wanachi wanaouwawa huwa wanawekwa upande gani na serikali kumbe mtu angekuwa akiuwawa mambo yachukuliwe uzito namna hii mauwaji yangepungua
 
NOTE:

NI ACP (Assistant Commissioner of Police - Kamishna Msaidizi wa Polisi) siyo SACP (Senior Assistant Commissioner of Police - Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi)... ACP Liberatus Lyimo Barlow.

Natanguliza shukrani.

Yupi mkubwa hapo?
 
wewe umetoa tsh ngap? Utu ni bora kuliko pesa.

nimetoa, siwezi kwenda kuhani kuwaongezea mzigo wafiwa. Tumefundishwa kuwapunguzia mzigo wafiwa, mzigo wa kuwatunza waombolezaji kwani kwa stress walizonazo wao hawawezi. Sasa nilitegemea chadema wawe mfano katika hili. Badala ya kupeleka faraja, wanapeleka mzigo wa kuwatunza waombolezaji.
 
Kweli unategemea kuwa na jeshi la polisi lenye ufanisi kwa kuwa na askari wa aina hii? R.I.P Kamanda Barlow

8.jpg
 
Hata angekuwa SSP hayatuhusu, mbinguni hakuna cha OCS wala IGP

Mkuu PhD that wasn't my point. I was rather tryng to enlighten those of you who didn't know the difference (or ddin't even know there was a difference). I believe knowledge is power. You never know when you will need it.
it was jus one of those FYI notes...it actually didn't require any response. But thanks for displaying to us your wisdom.
Greet them brothers in Houston.
PhD.
 
Last edited by a moderator:
Uliiba mke wa mwenzio...Mungu akulaze panapostaili

Una uhakika alikuwa ni mke wa mtu, biblia inasema usihukumu usije ukahukumiwa. Ulikuwepo huko mwanza?? Acha unafiki wewe, hope ya kwako yamekushinda if you don't have a true source of information it is better to keep quite
 
Maundumula, mkubwa ni SACP.
huwa anaanza;
IGP
CP
DCP
SACP
ACP
SSP
SP
ASP
INSP
A/INSP
SM
S/SGT
SGT
CPL
PC
RC.

Tafuta thread moja ilianzishwa na mdau mmoja anajiita Thanda utapata uelewa zaidi. au kina SAMITI na Polisi wanaweza kukusaidia.


Polisi hawana rank kama hiyo.Mtiririko uko sawa.Pia hicho cha mwisho pia kina utata kwani ni ka-cheo ambako kwa mujibu wa PGO hakakutajwa na hakapo so nafikiri busara tuanzie na PC tu period
 
Last edited by a moderator:
Ntamaholo, kwani kulikuwa na kujipanga? Vipi nyinyiem mlijipangaje na mwanandoa wenu C*F? Halikuwa tukio la kisiasa, wewe unatokwa na mapovu kwamba CDM hawakujipanga. Ukilala unaota CDM ukiamka unawaza CDM. Kweli mmeshikwa patamu.
 
Back
Top Bottom