Picha - Traffic Polisi wakipokea Rushwa hadharani

Unaambiwa waendesha bodaboda hukusanya michango kuwapatia traffic wasiwabughudhi! Inasikitisha kweli.Ndio maana boda boda na bajaj wanatenda makosa kama hawana akili nzuri bila woga wowote! SHAME!
 
Mnawaandama trafiki wa nini mbona vigogo mmewacha na matumbo yao kila mbuzi na urefu wa kamba yake bwana ukipata kamua tuu ila uwe makini usikamatwe
 
Kila mtu anakula ofisini kwake. wabunge wanajipitishia posho kubwa, hawa hawana mahali pa kupata posho. Posho yao ni hiyo!!!! ni sahihi kabisa. Songa mbele polisi kula rushwa kwa kwenda mbele!!!!!

Sawa kabisa Trafiki zali likikupitia kamua maana mshahara wako wazee wanakula kwa siku moja gari bure mafuta bure. ndio nini hiyo we kula tuu ikija
 
Sasa wale nini na maisha magumu kama mawe?
Kwa namna maisha yalivyo ghali watu wenye kipato kinachoweza kuitwa cha chini lazima wafanye mipango mingine ili kutosheleza mahitaji ya familia. Inasikitisha ila hiyo ndio hali halisi. . .

Vitu vingine hata kama ni hali ngumu siyo vya kuvifagilia. Ina maana mtu akikuomba wewe nanihii kama rushwa utampa kwa sababu ni hali ngumu?
 
rushwa.JPG


Traffic waliopo barabara kuu eneo la Bwawani Chalince-Morogoro wakipokea rushwa. Raia mwema aliyesafiri na kuwanasa hawa traffic wakipokea rushwa alikaa kwa muda katika eneo hili na kuwapiga picha. Vijana walioandaliwa wakijishughulisha kama wanasafisha gari ili kuwa kizingizio huku wao wakiendelea na zoezi la kukabidhiana rushwa. Askari hao baada ya kubaini mdau huyo amewapiga picha walimfuata ndani ya bus alilokuwemo na kuanza kupambana naye lakini mpiga picha aliwazidi ujanja na kuwashinda. Kairusha picha hii kupitia mdandao wa Michuzi.

Can you believe the source?
Picha haithibitishi maneno yaliyo ktk thread.
Any way, traffic polisi wa Tanzania ni 'janga la kitaifa!'
Hivi TAKUKURU wanafanya kazi gani?
 
Kwa picha hiyo hakuna kitendo chochote kinachoonyesha transfer ya cash au kitu chochote cha aina ya rushwa kati ya traffic na hao raia! Mleta mada umejuaje kuwa rushwa ilitolewa hapo?...au unahisi tu kutokana na default value juu ya tabia ya hawa ndugu? Ni rushwa gani inatolewa mbele ya kundi la watu namna hiyo? Halafu kwani traffic police hawana ndugu na jamaa zao wanaoweza kuongea nao kama hivyo pichani? Mi naona ni shughuli za kawaida tu zinaendelea hapo, kuna kijana anaosha gari, wengine wanachati tu na maafisa hao, lakini hakina m'badilishano wowote wa pesa hapo! Mleta mada alitakiwa apige na picha labda inayoonyesha gari fulani imepaki kwa kukamatwa, hapo ndipo ingeleta ushawishi wa kuamini kuwa madereva wake ndiyo wanamsaundisha traffic, lakini kwa mazingira hayo. hakuna dalili hizo!
Nakubaliana na Paka jimmy kwa asilimia 95.9 sioni kama stori inaendana na picha
 
Hii kapiga Gerry Muro nini?
Gerry Muro kwa mtindo huu alisukiwa zengwe karibu atemeshwe uhuru wake aitwe mfungwa!!!! Vitu vingine kuweni realistic issue iweze kueleweka vizuri!!! Lakini kwa mazoea ya Trafic wa TZ mtu anaweza kutafsiri picha hiyo vyote apendavyo!!!

 
rushwa.JPG


Traffic waliopo barabara kuu eneo la Bwawani Chalince-Morogoro wakipokea rushwa. Raia mwema aliyesafiri na kuwanasa hawa traffic wakipokea rushwa alikaa kwa muda katika eneo hili na kuwapiga picha. Vijana walioandaliwa wakijishughulisha kama wanasafisha gari ili kuwa kizingizio huku wao wakiendelea na zoezi la kukabidhiana rushwa. Askari hao baada ya kubaini mdau huyo amewapiga picha walimfuata ndani ya bus alilokuwemo na kuanza kupambana naye lakini mpiga picha aliwazidi ujanja na kuwashinda. Kairusha picha hii kupitia mdandao wa Michuzi.

kichwa cha habari hakiko sahihi,acha dhana mbovu,sio kila uambiwacho kina ukweli ndani yake sasa rushwa iko wapi hapo ikitolewa na ukipokelewa?,mnyonge mpe haki yake kwanza kisha umnyonge
 
Hivi mtu akishakua traffick haruhusiwi kupewa au kushika pesa tena?
Hivi nikiwa na ndugu traffick hawezi kupokea michango ya harusi, au kuletewa hela na nduguze kwa ajili ya kitu fulani? Mbona sisi tunaletewa pes makazini kwetu na sio rushwa?

Sitetei rushwa lakini lazima tuwe makini. Hii picha haionyeshi mazingira ya rushwa

:A S-coffee:
 
Kwa picha hiyo hakuna kitendo chochote kinachoonyesha transfer ya cash au kitu chochote cha aina ya rushwa kati ya traffic na hao raia!
Mleta mada umejuaje kuwa rushwa ilitolewa hapo?...au unahisi tu kutokana na default value juu ya tabia ya hawa ndugu?
Ni rushwa gani inatolewa mbele ya kundi la watu namna hiyo?

Halafu kwani traffic police hawana ndugu na jamaa zao wanaoweza kuongea nao kama hivyo pichani?
Mi naona ni shughuli za kawaida tu zinaendelea hapo, kuna kijana anaosha gari, wengine wanachati tu na maafisa hao, lakini hakina m'badilishano wowote wa pesa hapo!

Mleta mada alitakiwa apige na picha labda inayoonyesha gari fulani imepaki kwa kukamatwa, hapo ndipo ingeleta ushawishi wa kuamini kuwa madereva wake ndiyo wanamsaundisha traffic, lakini kwa mazingira hayo. hakuna dalili hizo!

Kwa upande mwingine wa shilingi waweza ukawa sawa ila in actual sense traffic wetu wakikushika hao wa Camera huwa mwaongelea wapi si kwa gari lao na kama ni kosa kwanini wasiku adabishe hapo hapo barabarani mchana kweupe kuliko kunivuta chemba na unajua fika traffic wetu ndio wanaongoza kwa kula mrungula nje. PJ kama wewe ni mtu wa safari na hutumia gari lako binasfi hii hali unaijua me naijua fika hawa huwa hawana cha kukupeleka kituoni wao wanataka chao.

Mfano hao Trafici wako kwa gari watuhumi ndio wako kulia kwa mrango wa tarffic mwingine traffic yuko kushoto mtuhumiwa tu kwakumwangalia mpaka ameshika kichwa sijui anajikuna hapo baadaya kuambiwa kosa lake kwanini hao traffic wasisimame mbele ya boneti ya gari na kumwandikia huyo bwana makosa yake??


 
Tatizo la viongozi wetu kujilimbikizia marupurupu na mishahara mikubwa ndio chanzo kikubwa kwa watu kama hawa kuchukua rushwa,maana atawezaje kuziba nakisi ya kipato chake na upandaji wa maisha?maana watu wa namna hii hawawezi kuwa na maisha magumu kwa msamiati uliopo ni wabunge na viongozi wakubwa wa mashirika ya umma na tasisi za serikali ndio wanao tambua kuwa gharama za maisha zimepanda,watu wachini watatafuta njia zao za kuziba pengo sasa ndio kama unavyoona Traffic hapo wanaziba pengo la kupanda kwa maisha,wako sawa.
 
Sioni kitu kwenye picha hiyo kinacho dhihirisha upkeaji wa rushwa. Bali najua kuwa polisi na mahakimu ndion walaji wakubwa - watu wanaotegemewa kuwa wa kwanza katika kusimamisha misingi ya haki na usalama.
 
kwani hujui rushwa ni mradi wa serikali? sserikali injua kila konaambapo rushwa imekubuhu, lakini sababu ni mradi wa kuinua kipato, wanaifungia macho.
 
tofauti kabisha ingawa yule jamaa wa pembeni kuna kitu anaa ngalia kwa gari la police sijui nini....angepatikana huyo angetuambia nini kinaendelea...

na
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom