PICHA: SPIKA ANNA MAKINDA akihudhuria Mkutano wa MASPIKA WANAWAKE DUNIANI huko INDIA

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
THURSDAY, OCTOBER 04, 2012
BUNGE LA TANZANIA MFANO WA KUIGWA KATIKA KUWASHIRIKISHA WANAWAKE



Mapema akihutubia katika mkutano wa Saba wa Maspika wanawake duniani Spika Anne Makinda aliwaambia wajumbe kuwa wabunge wanawake Tanzania ni 36% jambo ambalo lilifanya Tanzania kusifiwa na kushauriwa kusonga mbele hadi 50%.

Rais wa Inter-Parliamentary Union (IPU), Bw. Abdelwahad Radi (wa pili kushoto) na Katibu Mkuu wa IPU Bw. Anders Johnsson ni miongoni mwa viongozi mashuhuri waliohudhuria mkutano huo unaosisitiza wanawake kupewa nafasi zaidi katika vyombo vya maamuzi.

Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) akiongozana na Balozi wa Tanzania nchini India, Engineer John Kijazi, wakati wakuingi a katika ukumbi wa utamaduni wa Kihindi katika viwanja vya Bunge la India mjini New Delhi.

Wakiwa kwenye vazi maalumu waliloandaliwa, kutoka kulia ni Spika wa Bunge la India na mwenyeji wa mkutano wa Saba wa Maspika wanawake duniani Mhe. Meira Kumar, Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda na spika wa Bunge la Swaziland Mhe Gelane T. Zwane.

Picha ya pamoja ya baadhi ya maspika wanawake wa IPU ndani ya vazi maalumu waliloandaliwa.

THURSDAY, OCTOBER 04, 2012 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG









 

Spika wetu ni Mtembezi haswa... hapishani na Rais wetu... yaani naona ni SPIKA MTEMBEZI kuliko wote
Nchi yetu iliokuwa nao na pia ndie Mvivu kufanya kazi kuliko Maspika wote tuliokuwa nao; lakini ndio spika Mwenye NYUMBA SWAFi ya SPIKA kuliko Maspika wote DODOMA na DAR - zina SWIMMING POOL... Jamani Kweli ANNA MAKINDA ndani ya SWIMMING costume kuogelea ? si tumepoteza PESA za SERIKALI ?
 
Huyo ni mlezi wa ufisadi wala hana jipya kwetu. Nchi ndiyo kwanza inadidimia na CCM inawafia with no cost!
 
Back
Top Bottom