PICHA: Rais Kikwete katika ziara rasmi Ottawa, Canada

attachment.php


Amenikumbusha Idd Amini aliposhika dola akawashikisha adabu wazungu kumchukua mzegamzega, hapa wazungu pekee wanamvuta Kikwete kwenye farasi. Duh, hujaumbwa hujaumbika.
 
Maraisi wa Africa Huko Kwa Wazungu Wanazarauliwa sana, Mfano USA OBAMA kwa Bara la Africa anaweza enda Uwanja wa Ndege Kumpokea Raisi wa South Africa Pekee, Hao wengine wanapokelewa na Watu wa Kawaida tu
Kwa itifaki ya Marekani, rais haruhusiwi kwenda uwanja wa ndege kumpokea mgeni wake hata kama ni ziara ya kiserikali. Hiyo ni kazi ya Secretary of State. Rais anamsubiri mgeni wake kwenye South Lawn ya White House ambako gwaride rasmi la mapokezi hufanyika, na baada ya hotuba, wanaingia ndani ya White House kwa mazungumzo rasmi.
 
Kwani linatofauti gani na yale yakwetu Shinyanga yanayo kokotwa na PUNDA? au kwa kuwa wao wameweka gurudumu za ghuta sisi tunaweka magurudumu ya gari yaliyo tumika.kumbe shy kama ulaya!!!!!!!!!!!!!!
 
Wakati Mkulu ana-enjoy kuendeshwa na polisi wa ughaibuni, huku nyumbani Polisi wanatorosha wauaji. I do not get it
 
Anapokewa na waziri wa mambo ya nje, kiongozi mkuu wa nchi kasafiri, au ndio wamemchoka JK
Ni utaratibu wa nchi nyingi tu unapofika uwanja wa ndege unapokewa na waziri au mkuu wa itifaki. unapofika ikulu ndio unapokewa rasmi na mkuu wa nchi. Hii inapunguza foleni za kwenda airport na kurudi na kiongozi wao hapotezi muda mwingi kupokea wageni. In fact marekani nadhani kwa mwaka ni kama viongozi watatu tu ndio huwa wanapokewa kwa gwaride ikulu wengine mnakutana na Rais ofisini kwake
 
Mkandara nadhani ni sawa tu kutoza hio pesa, inategemea nani kaandaa, kama serikali basi hapo ndio utata ila kama ni watz wanaoishi CA basi ni kawaida
 
Last edited by a moderator:
Ndio alichoenda kufanya huko kupewa heshima na kupanda farasi, Rais kweli tunae na tuna safari ndefu sanaaaaa

Hawa viongozi wetu wanachekesha sana ,wakiwa ughaibuni wanakubali kupandishwa kwenye matolori lakini huku kwetu kwa watu waliowapa mamlaka hata bajaj wanaogopa kupanda kwa usalama wao na badala yake wanatumia magari ya kifahari ili kuwakoga walalahoi!! Najua kuna mjinga atakuja kusema eti ni protocol ; wa URUGUAY nchi tajiri kuliko bongo rais anatumia volkswagen; nyie vilaza mna habari hiyo?
 
Si ndo nchi inayo vuna almasi za watanzania!(kahama mining) hapo baada ya kupanda hao farasi madini yatachotwa bure wakati PAYE zinatumaliza watanzania, mpaka Mungu arudi tutabakia mifupa.

Mungu ameenda likizo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom