Picha: Rais JK atembelea na kukagua jengo la bunge kuangalia jinsi wabunge wa katiba 600 watavyokaa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

October 24th 2013

zzzz1.jpg

Rais Kikwete akikaribishwa kutembelea Jengo la Bunge mjini Dodoma na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai leo Oktoba 24, 2013.

View attachment 118157

Rais Kikwete akiangalia sehemu ya viti ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013.

View attachment 118158

Rais Kikwete akitembelea Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013.

View attachment 118159

Rais Kikwete akisindikizwa na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai na Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila baada ya kutembelea Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013.

zzzz5.jpg

Rais Kikwete akizungumza na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai na Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila baada ya kutembelea Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Oktoba 24, 2013 ametembelea na kukagua Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma kujionea maandalizi ya jinsi Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba watakavyokaa katika Ukumbi wa Bunge hilo.

Bunge hilo Maalum la Katiba litakuwa na Wabunge 600 tofauti ya Bunge la sasa lenye Wabunge 354 ambao ni pamoja na Wabunge 239 wa kuchaguliwa kutoka majimboni, Wabunge Wanawake Viti Maalumu 102, Wabunge wa kuteuliwa toka Baraza la Wawakilishi Zanzibar 5, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Wabunge 7 (kati ya 10) wa kuteuliwa na Rais.

( PICHA NA IKULU )

Kuna tofauti ipi kati ya ukumbi huu Bunge la kawaida na bunge la Katiba?Ama mleta haoja anataka aonekane naye ana uzi kaweka jamvini?Aibu tupu!
 
Inaonyesha ni kweli Mapendekezo ya Rais yalifuatwa... Unakumbuka Wenyeviti wa Vyama vya Upinzani walikuwa wanataka kuandamana na pia kuonana na Rais...

Baada ya Rais kuongea nao Walifuta yale Maandamano na Wako Kimya hawajasema chochote walichosikia toka kwa RAIS lakini tunaona kinachoendelea... kwamba KATIBA itajadiliwa na Wananchi wapatao 600 wa kona mbalimbali ndani ya hilo bunge...

Utofauti pia ni hizo Nafasi 300 zilizoongezwa... kwa kipindi hicho kifupi...
 
Wishful thinking!pengine weye ni mtabiri utakayechukua nafasi ya Maruhum Shekh Yahya!
 
I don't believe in those thoughts... Naimani na Wananchi wa NCHI yangu na Serikali yake...
 
Sikulaumu uko kazini Lumumba ili watoto wapate choo kwa malipo ya Buku 7.unajitekenya kisha unacheka kama zuzu vile!

Mimi ni critic wa serikali sana; lakini kama kuna zuri wanalolitenda sichelewi kuwapongeza sababu ni SIASA sio UADUI wa KUUANA... SIASA sio NYARA za KUVUNJA UHUSIANO tu kwasababu ya ITIKADI tofauti...

Kwahiyo Kama unasema LUMUMBA wanatoa hizo BUKU 7; haziwezi kunisaidia sababu nina ishi nje ya nchi hizo buku 7 is nothing 2 me...
 
sio humu maana hao 357 wapo wanaokaa nje na old desk wachongewa za mbao ndo ije iwe600? watafanyia u dom
 
Hii picha ya zamani alitembelea jengo hilo lilipokuwa ndio kwanza linafunguliwa.
 
Mimi ni critic wa serikali sana; lakini kama kuna zuri wanalolitenda sichelewi kuwapongeza sababu ni SIASA sio UADUI wa KUUANA... SIASA sio NYARA za KUVUNJA UHUSIANO tu kwasababu ya ITIKADI tofauti...

Kwahiyo Kama unasema LUMUMBA wanatoa hizo BUKU 7; haziwezi kunisaidia sababu nina ishi nje ya nchi hizo buku 7 is nothing 2 me...

Mkwala uliopigwa nini?

Ok ok all the best!
 
Kuna tofauti ipi kati ya ukumbi huu Bunge la kawaida na bunge la Katiba?Ama mleta haoja anataka aonekane naye ana uzi kaweka jamvini?Aibu tupu!

Kusoma huelewi basi hata picha huoni?

Umeambiwa kwa sasa wabunge ni 354 (tazama viti vyekundu), Bunge la katiba watu 600, tazama viti vyeusi.

Upo hapo ulipo?
 
Inaonyesha ni kweli Mapendekezo ya Rais yalifuatwa... Unakumbuka Wenyeviti wa Vyama vya Upinzani walikuwa wanataka kuandamana na pia kuonana na Rais...

Baada ya Rais kuongea nao Walifuta yale Maandamano na Wako Kimya hawajasema chochote walichosikia toka kwa RAIS lakini tunaona kinachoendelea... kwamba KATIBA itajadiliwa na Wananchi wapatao 600 wa kona mbalimbali ndani ya hilo bunge...

Utofauti pia ni hizo Nafasi 300 zilizoongezwa... kwa kipindi hicho kifupi...
Kwamba hoja yao ilikuwa ni Watanzania kutoka kona mbalimbali; SIDHANI! Hoja ya Wapinzani ilikuwa ni namna ya kuwapata wale wabunge wa ziada (mbali na hawa sasa!) Kwamba, wakati utaratibu uliowekwa ni kwamba hao wa ziada (about 300) watateuliwa na Rais baada ya kuwa ameletewa majina matatu! Kwamba, SAY Jamiiforums ingekuwa nasi tunataka mwakilishi wetu, basi sisi wenyewe tunachagua/tunateua majina matatu na kuyapeleka IKULU kisha JK anateua moja kati ya hayo matatu! Hii ndiyo hoja ya msingi; hususani kwa CHADEMA! Haya ya kwamba Wazanzibari hawakushirikishwa ni porojo tu za kisiasa....anyway, this's like war; no war without propaganda! Hawakuosea kuleta suala la kutoshirikishwa Wazanzibar ili kutafuta uungwaji mkono!

So, vyama vya upinzani hawoni kama ni sahihi kuachia JK kuteu hao watu! Hofu yao ni kwamba, baada ya majina kupelekwa IKULU, huenda wana-mikakati wa CCM waka-scrutinize na kujua kwamba among the Three Names brought foward; X and Y wanweza kutetea maslahi ya CHADEMA wakati Z anaweza kutetea Z na hivyo Mkulu akakata shauri la kumteua Z!! Katika stahili; ikiwa wanachanga karata sawa sawa; basi si ajabu out of (say) 300, basi 200 wakaenda Mjengoni kutetea maslahi ya CCM na hivyo ukichanganya na wale waliopo; CCM wakawa na mtaji wa angalau WATETEZI 400 huku 200 wakienda pale kutetea upinzani (CHADEMA?) Nafahamu, huku mitaani watatupiga fix kwamba ni Katiba ya Watanzania lakini Si mwanachama wa CCM wala CHADEMA ambae ataweka maslahi ya Watanzania kwanza!

Sasa basi, issue ipo hapo kwenye kuwapata hao wabunge; itumike njia gani? Ikumbukwe kwamba wanaohitajika kutoka kwenye hivyo vikundi ni takribani wabunge 300 wakati taasisi husika zipo zaidi ya mia tatu!! SWALI: Kama idadi ya taasisi/NGOs, CBOs ni kubwa kuliko idadi ya wabunge wanaohitajika; Sasa kama uteuzi ufanyike kutokana na hoja ya Upinzani; kwanini ni Taasisi A ndiyo iwe na mwakilishi na sio B? By the way, ni nani huyo atakayeteua hiyo taasisi A itakayotoa mwakilishi? Sina uhakika kama nimeeleweaka; assume kuna CBOs/NGOs/and the Like 400 ambazo collectively wanatakiwa kupeleka wawakilishi 300; so, ni nani huyo atakayechagua taasisi 300 out of 400? Tuamini kwamba hawa watakutana kisha wakapiga kura? Anyway, sisemi kwamba haiwezekani inawezekana kabisa lakini ninachotaka kusema ni kwamba WAPINZANI WAMEPIGWA CHANGA LA MACHO! JK alichowakubalia ni kwamba hoja irudi Bungeni! Siamini kwamba CCM wata-vote against exclusive right ya President katika kuteua mtu mmoja out of the THREE! Unajua itakavyokuwa?
Itakuwa hivi; baada ya mjadala mkali, hatimae kura zitapigwa! Wanaosema ndiyo; NDIYOOOOOOO, wanaosema siyo; SIYOOOOOOO! Mnyika atasimama tena na kusema tuhesabu kura moja moja na mwisho wa yote Waliosema NDIYOOOOOO (CCM) wameshinda! Hapo sasa; CHADEMA na wenzao wakitoka tena ukimbini; wataonekana KUMBE KWELI CHADEMA WAKOROFI! Rais amewasikiliza; hoja imerudishwa bungeni; Wengi wameamua lakini BADO CHADEMA HAWATAKI!

Ole wao ambao wanaomwa-undermine JK!
 
Je wataalamu, naweza fahamishwa kwa nini hivyo viti ni vyekundu? nitashukuru kupata historia kidogo.
 
Sasa huyu Ndugai ujanja wote akikutana na Kikwete anakuwa hoi!! Yaani picha zote mkono kaweka tumboni utafikiri mtoto wa shule, yaaani hadi anaboa, kama ni heshima; heshima gani hiyo khaaaaaaaaa!

October 24th 2013

Rais Kikwete akikaribishwa kutembelea Jengo la Bunge mjini Dodoma na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai leo Oktoba 24, 2013.

View attachment 118157

Rais Kikwete akiangalia sehemu ya viti ndani ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013.

View attachment 118158

Rais Kikwete akitembelea Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013.

View attachment 118159

Rais Kikwete akisindikizwa na Naibu Spika Mhe. Job Ndugai na Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila baada ya kutembelea Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo Oktoba 24, 2013.

View attachment 118160

Back
Top Bottom