PICHA: Ndege mpya za Fastjet hizi

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,532
KLM-25.jpg
Kampuni ya ndege ya Fastjet imepanga kuingiza nchini ndege moja jamii ya Embraer 190 ili kukabiliana na hali ngumu ya sasa ya kibiashara.

Jana Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, John Corse amesema ndani ya wiki mbili zijazo wataingiza ndege mpya katika safari zake ikiwa ni sehemu ya majaribio ya kutekeleza mkakati wa mabadiliko C&P MCL.
_MG_5995n.jpg
58.JPG
 
Interesting.....

tuone 'mapanga shaa' na hizi nani zaidi
Tatizo ATCL wanateuana kwasababu ya kuwa na kadi ya CCM.
Utaalamu unawekwa pembeni.
Pamoja na kuwa na jeuri ya fedha, UAE walimchukua Clark kuisimamisha Emirates ambayo leo ni moja ya shirika linalokuja kwa kasi sana duniani.
Walianza na mtaji wa $10Milion na ndege moja ya kukodi toka Pakistani mwaka 1985. Leo hii wana ndege walau 200+ na wapo kwenye destinations almost 150+.
Biashara ya ndege sio mchezo.
 
Embraer 190, E190, Embrear 170, ya Brazil ni hottest cake... in aviation hasa ktk regional flights.. !! Yaani hiyo inaua biashara ya ndege za turbo props kabisa... na ni special for regional flights.. medium and short ranges..!!

Sijui kama Serikali yetu inajua hili..!!

1021984.jpeg
1077066.jpeg
JetBlue ERJ 190-100 N334JB (10-Barcode)(Grd) RDU (KP)(46)-M.jpeg
1021984.jpeg
1077066.jpeg
JetBlue ERJ 190-100 N334JB (10-Barcode)(Grd) RDU (KP)(46)-M.jpeg
1000-upload-iblock-a4e-embraer-190_com.jpeg
750x500-embraer-190-1.jpeg
750x500-embraer-190-1.jpeg
750x500-embraer-190-1.jpeg
EMBRAER-190-195.jpeg
 
Hao ni vimeo tu wali cancel safari za route ya Kia- Mwanza sijui ndo nini walifanya sasa
 
Naam, ndege imeenda shule hii. Kitu kimetulia. Ni jet engine. Yale mapanga shaaaa hata kwa bure sipandi.

Mkuu;
Tuseme hupandi kwa kuwa haipai juu yatembea ka vw au ni kwa kuwa imenunuliwa na serekali. Ushauri wangu wa bure kwa watu wa sampuli yako;
Acha ziletwe kwa wingi nchini. Bei (Nauli) ishuke, wenye safari za ndani tuepuke mabas haya yanayowachinja ndg zetu kila siku. Ndege zipae juu na kutua salama. Nadhani la msingi tungeli iomba serekali hii sikivu, iangalie uongozi unaowekwa. Tusiangalie kadi ya chama, Biashara itakufa kabla haijaanza wakiweka chama chao mbele. Gazeti la uhuru halisomeki kwa sababu bila habari ya sendeka haliruhusiwi kuuzwa. Matokeo yake linapelekwa maofisini tu nako hawalipi.
Wekeni wataalam wa biashara waongoze shirika sio mainjinia. Injinia asimamie karakana
 
Fastjet wanaijua hii biashara wameona yale madege yao hayataweza kutua dodoma wakasema isiwe tabu ngoja tukalete ndogo itakayoweza kutua dodoma pia sasa ATCL na PRECISION zijiandae maana huwa zinamkimbia huyu jamaa kwa visingizio tele mara ooh hakuna mafuta mara sijui ukungu kama walivyokimbia Songwe, hii safi ushindani ukiwa mkubwa nauli inakuwa chini, wapandaji tunaongezeka, muda unalindwa,pesa inaingia fasta. Huku mapanga shaa huku za vichungu nani ni nani!! let's watch ze game.
 
Sijui kama biashara kuyumba ni sababu ya kubadili ndege kutoka A319 mpk E190,mi naona jamaa wanajiandaa kimkabili 'mapanga shaaa' a.k.a ATCL maana hizo ndege za sasa za fastjet A319 zinatua viwanja 4 tu Dar,mwanza,Kilimanjaro na mbeya(songwe),ila hizo E 190 zinaweza kwenda Bukoba,Arusha,Mtwara,Tabora,Kigoma,Musoma na Dodoma kwahiyo mapanga shaa wajiandae.
 
Back
Top Bottom