Picha - Nape siku alipokula matapishi yake

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,883
6113984.jpg

Napenda kuongelea na kuchambua mambo ya siasa lakini si mfuasi wa siasa, maana ukiamua kuingia kwenye siasa unatakiwa uwe kama wale vijana wa unga uwe stimulated na kitu fulani, la sivyo utaonekana you staggering jukwaani bila ushawishi kwa hadhara. Kwa vyo vyote kama u mdini utaiendekeza dhambi ya wongo, kwani mara kadhaa mtu anaongea kitu asichokiamini bali ni propaganda za kisiasa, ambazo kesho atazikana hadharani kama Nape anavyofanya.
 
Hii nadhani ni kipindi kile uhususiano wa nape na watu wa chadema haujaanza kulega lega wenyewe chadema wakimwita mpiganaji,siku tukimwita mpigaji watu wananuna...
 
6113984.jpg

Napenda kuongelea na kuchambua mambo ya siasa lakini si mfuasi wa siasa, maana ukiamua kuingia kwenye siasa unatakiwa uwe kama wale vijana wa unga uwe stimulated na kitu fulani, la sivyo utaonekana you staggering jukwaani bila ushawishi kwa hadhara. Kwa vyo vyote kama u mdini utaiendekeza dhambi ya wongo, kwani mara kadhaa mtu anaongea kitu asichokiamini bali ni propaganda za kisiasa, ambazo kesho atazikana hadharani kama Nape anavyofanya.
Nape Chadema wamemteka wee shauri yako SiSim watakufukuza uwaulizi wenzako wewe cheka tu hahahahahahahahh
 
Hii nayo walimphototoshop? bahati mbaya siku hizi kakimbia JF

Kwa mtazamo wa Nape atakataa kwamba hakuwako katika mkutano huu ambao aliwakilisha Chama cha CCM na yeye kuvikwa bendera ya Chadema. Ndio maana nasema siasa unatakiwa ufanye kama huna akili timamu vinginevyo uropokaji unakutia kitanzi usipojua namna ya kuchepusha uwongo kuwa ukweli.
 
Hata wachezaji wa timu pinzani hubadilishana jezi, hata Messi aliwahi kuvaa jezi ya REAL
 
Hapa lazima nimtetee Nape mtani wangu.

Hii picha ilipigwa wakati wa mkutano wa Chadema, siku kadhaa nyuma kabla uchaguzi haujaanza.

Hata mkutano wa CCM kule Dodoma wa kumtangaza Kikwete kuwa mgombea, CHADEMA walipeleka kiongozi kuwakilisha CDM kwenye mkutano huo na alipewa MIC kabisa kumwaga salamu zake.

Nape pia alikaribishwa vizuri na kupewa MIC na wakati akifika, ndiyo akapigwa hiyo picha.

Bendera ni bendera tu na unaona kabisa mtu kaishikilia na mtu huyo ni Chadema.

Tuwe wakweli wakati mwingine kwa maswala ambayo hayana umihimu wowote kwa Taifa.

HERI YA MWAKA MPYA KWENU NYOTE.
 
Nepi ana upara nini?!

Teh teh hahahahahahha

Bwana anaitwa Nape sio Nepi bana
haha hahaha umenifurahisha sana, ila kwa mambo anayoyafanya huyu bwana naanza kuona sababu ya kumwita NEPI maana amekaa ki nepi nepi ya mtoto, tena ile iliyochafuliwa na mtoto tayari.

Nepi nepi
 
Hapa lazima nimtetee Nape mtani wangu.

Hii picha ilipigwa wakati wa mkutano wa Chadema, siku kadhaa nyuma kabla uchaguzi haujaanza.

Hata mkutano wa CCM kule Dodoma wa kumtangaza Kikwete kuwa mgombea, CHADEMA walipeleka kiongozi kuwakilisha CDM kwenye mkutano huo na alipewa MIC kabisa kumwaga salamu zake.

Nape pia alikaribishwa vizuri na kupewa MIC na wakati akifika, ndiyo akapigwa hiyo picha.

Bendera ni bendera tu na unaona kabisa mtu kaishikilia na mtu huyo ni Chadema.

Tuwe wakweli wakati mwingine kwa maswala ambayo hayana umihimu wowote kwa Taifa.

HERI YA MWAKA MPYA KWENU NYOTE.

Hili ni jukwaa la picha, tunajaribu kuleta baadhi ya kumbukumbu ya mambo ya kihistoria, na unapoweka chungu jikoni huinjiki juu ya moto utakokaje? hapana budi kuweka mafiga na chungu kuinjia kwenye mafiga ili kutoa mwanya wa kuchochea moto chini ya chungu kuivisha matoki na ndizi mbivu kwa ajili ya mbege ya kusherehekea mwaka mpya.
 
hii picha alipigwa siku alipo hudhuria mkutano mkuu wa chadema kama mwakilishi wa ccm. huyo aliyesimama mbele yake na magwanda Akimvisha joho anaitwa shitambala ambaye alikuwa mwenyekiti wa chadema Mbeya. sasa hivi kashahamia ccm. Mia
 
Back
Top Bottom