Jamani nyie acheni tu!! Mchana tulipigwa mabomu Furahisha lakini bado jioni tukarudi tena Magomeni., Mngeona watu walivyokuwa wanamsubiri kwa hamu,, alivyoingia kwenye saa kumi na mbili hivi watu wakawa wanimba Raisi raisi raisi yaani inaleta rahaaaaaaaaaaa. Alivyouona ule umati wetu akasema, "jamani watu wa Mwanza, mnanifanya nitokwe machozi kuuona umati wenu". Jamani watu walimshangilia na ilikuwa akitaka kuongea watu wananyamaza kimya, akiongea pointi wanashangilia na kunyamaza ili kumsikiliza. Ama kweli tuombe MUNGU wapige kura wote kwa hakika ushindi wa Slaa mwaka huu utakuwa ni wa kishindoooooooooo!!